CCM ipewe lawama kwa kuwapa vyeo wale mayuda walionunuliwa toka upinzani. itakuwa wanahusika na kifo cha JPM.
 
... afya ya mtu ni siri kati yake na daktari wake! Ni ajabu CCM kuweka kipengele kama hicho kama mojawapo ya "sifa" za mgombea. Nadhali walikuwa na nia ovu ya kuja kukitumia baadaye kum-eliminate mgombea fulani kihuni na walifanikiwa hadi kwenye kampeni. Ila bahati mbaya Mungu alikuwa na jambo lake!
 
John kijazi KMK nani atabeba lawama?
 
Rais siyo mtu bwashee!
 
Na tumlaani pia kwa mabaya aliyotenda pia! Never ever again!
 
Nyerere hakufa madarakani,Mkapa hakufa madarakani.Wote hao walifariki wako nje ya madaraka.
 
Kwa maslahi mapana ya nchi tujiulize;
Je alikuwa asset au liability?
Je alikuwa bearable au unbearable?
Huwa ni kawaida ya nyumbu kuona yuko salama mbele ya mdomo wa Simba.

Rais Samia wanyooshe tena.
 
Sasa yeye kama alijua ana matatizo yote haya, alikuwa anatafuta nini kwenye nafasi kubwa kama ile? Mnajua tunachoshana tu, Ina maana Mamlaka za vetting zilishindwa kujua kwamba jamaa anatumia jenereta?

Huyo bana alienda tu zilifika zake. Aliwekwa ili maandiko yatimie na alikuwa anaongea lakini hakuwahi kuamini waweza kufa muda wowote hata ukiwa ikulu Mungu akiruhusu hauna ujanja.
 
" Na nyie Vijana akina GENTAMYCINE ifike muda muwe mnafanya sana Utafiti na Kutumia Akili pia. Hivi kwa Akili ya Kawaida tu kweli Mgonjwa wa Moyo akiwekewa Pacemaker anaweza kuwa na Ratiba nyingi ambazo hasa Marais ( Viongozi ) huwa wanazo? "

" Ukiona umewekewa hiyo Pacemaker jua hata Uhai wako kwa 99% uko shakani na huwezi ukamaliza hata Miezi 6 sasa tunajua jinsi Marais wa Afrika walivyo na busiest Schedules zao hivi kama kweli yupo aliyekuwa nayo angeweza hata tu Kufanya Kampeni au Kusafiri huku na kule kwa Gari au hata Ndege? "

" Kuna Watu unaweza kukuta labda wana Uadui wao na Wewe hivyo wakata Kufanya yao Kwako ili Ndugu zako wasijue na wakishakifanikisha tu na Wewe GENTAMYCINE kuwa Historia hapa duniani wanakimbilia Kueneza Uwongo na Uzushi kuwa uliwekewa hiyo Pacemaker Moyoni mwako "

Huwa napenda sana Kukutana na 'Wataalam' mbalimbali na 'Kuwachokoza' na Maswali yangu ya 'Mitego' ambayo usipokuwa makini nayo unaweza kujikuta unanipa na mengineyo ambayo huenda sikupaswa kuyajua ila ukajikuta unashawishika na kufurahi tu Kuniambia ( Kunielezea ) huku Mimi nikikuchora Kiuweledi.

Ama kweli Mission Accomplished 100%
 
Upepo mbaya unaanza kuvuma kuelekea Msoga wiki hii!
K-vant nimeacha kwasababu ya kufuta kumbukumbu za mtumiaji!
 
Sasa sisi tumedanganywa na nani!?
Ila mbona nasikia manji anayo na anadunda?
Nilifikiri ungekuja na masuala ya kitaalamu zaidi
Kumbe ni maneno ya kanga tu
Ngoja tuendelee kufanya tafiti zaidi ili kujua ni sosi ipi ya habari waliotoa hio unaosema hakuna orodha yeyote ya rais tena wa afrika aliewahi kuwekewa pacemaker!
 
Kila upande na sehemu mbalimbali watu wanaendelea kuamini JPM hakufa kifo cha kawaida!

Binafsi naisihi Serikali iunde jopo la wataalamu wa afya wachunguze kifo cha huyo bwana Hayati Magufuli.

Kuiacha hiyo dhahania iendelee kuishi ndani ya mioyo ya watu ni sawa na kulea bomu ndani ya nyasi zenye ute ute wa petroli.

Ni muda mwafaka sasa Serikali ichunguze kifo cha JPM na itoke matokeo wazi.
 
Jiulize Tanzania kuna CORONA (COVID-19) na kama Ipo iliingia lini? Pili Jiulize je COVID-19 inawaondoa Watu wenye umri gani na wale wenye Matatizo yapi nyemelezi ya kiafya. Then Kifo ni Mungu tusipoteze Muda,Maisha Yaendelee hata Sisi Tutakufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…