Je, Rais Magufuli alikuwa na Pacemaker au Defibrillator? Ilidukuliwa?
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke
Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa;
Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

Ayubu 14:1-2
 
Aliidharau COVID-19 na COVID-19 haikufanya ajizi ikalala naye mbele kwa mbele.
 
hakuna lawama kwa yeyote sababu alikuwa katiri... there is no contry for old man
 
Vyombo vya dola ndivyo pekee vinaweza kutoa jawabu hilo.

Lakini kwa mazingira ya kawaida na kwa imani kubwa kutoka kwa wananchi wa kawaida hali iliyopelekea yeye kuwa mtetezi wa wanyonge jambo ambalo wenye kupenda kutumikisha na kuwaibia wananchi kamwe hawakulipenda.

JPM si tu alijitengenezea maadui wa ndani lakini pia aliwakwaza wakubwa huko Duniani kwa misimamo yake Thabiti hasa ya kuisimamia vyema rasilimali za Taifa pasi na kuyumbishwa.

Kwa muktadha huenda Magufuli aliuawa?!
We Mataga,

Kwani kufa ni jambo la ajabu au yeye ndiye wakwanza kufa?
 
Kuna makaburi ambayo ukihitaji kuyafukua inabidi uwe tayari kufukiwa nayo kwanza. Upo tayari mkuu
 
Ukiona mtu anataka ugomvi na kila mtu ujue wengine atawashinda na wengine watamshinda tu... hakuna malefu yasiyo na ncha, na mbio za sakafuni huishia ukingoni.
 
hivi kwa akili yako, na kwa ulinzi wa Rais, unafikiri ni rahisi tu kumuua Rais? si huwa unaona hata akitembelea mtaani pako tu mtaa mzima unabadilika hali ya hewa, ulinzi hadi vyooni, unafikiri kweli ni rahisi kiasi hicho? mambo mengine acheni kupoteza muda kupotosha watu. Rais ni Rais wewe usifanye naye mchezo.
 
Nasikia faili la mwendazake liliitwa kwa dharura baada ya kujiinua na kuanza kuwafundisha maparoko & maaskofu kipi cha kuhubiri
 
Nimejiuliza na kufikiria sana sana kuhusu kifo cha Rais Magufuli kilichosababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator.

Kujiuliza na kufikilia kwangu kumetokana onyo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani (Department of Homeland Security-DHS) lililotolewa mwaka 2019 linaloonya makampuni yanayotengeneza pacemaker/defibrillator kuhusu hatari ya kifaa hicho kudukuliwa na wataalam wa udukuzi na kupelekea hata kifo kwa watu waliopandikizwa kifaa hicho.

Ukitaka kusoma onyo hilo unaweza kugonga hapa;
Link>>> Pacemakers and Hacker Dangers

Wizara hiyo ilibainisha kuwa wadukuzi wanaweza kuingilia mifumo ya pacemaker/defibrillator na kuweza kubadilisha mawasiliano yake ambapo inaweza kupelekea mtu aliyewekewa kifaa kufariki.

Wizara hiyo ilienda mbali zaidi na kusema hata wadukuzi ''mwenye uwezo mdogo'' wanaweza kudukua pacemaker/defibrillator na kufanikiwa kuleta madhara makubwa kwa watu waliopandikizwa vifaa hivyo kwa sababu vifaa hivyo havina mfumo wa uhakiki au idhini (authentication or authorization) ambao ni kinga ya mwanzo dhidi ya udukuzi.

Onyo hili lilipelekea watoa huduma ya afya nchini Marekani kuwaita wananchi wa Marekani zaidi ya nusu milioni waliopandikizwa vifaa hivyo na kuwaeleza ukweli wake.

Kama kifaa hiki kinaweza kudukuliwa hata na wadukuzi wenye uwezo mdogo na kuleta madhara au kifo, inafikirisha sana kusikia kifo cha Rais Magufuli kimesababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator. Bear in mind, Rais Magufuli amekuwa na hii pacemaker/defibrillator kwa zaidi ya miaka 10. Why now?

Inafikirisha zaidi baada ya kusoma makala iliyoandikwa na Tundu Lissu kupitia gazeti la Afrika ya Kusini liitwalo Maverick akidai alidokezwa kuhusu hali ya Rais Magufuli na chanzo cha ''uhakika'' kutoka Marekani tarehe 6 Machi.

Ukitaka kusoma makala hiyo gonga hapa;
Link>>> OP-ED: Tanzania’s five years of devastation under the presidency of John Pombe Magufuli

Ukiyachanganua maelezo ya Tundu Lissu utagundua kuwa chanzo cha ''uhakika'' walijua wamefanikiwa ''mission'' ya kudukua hasa baada ya Rais Magufuli kwenda katika hospitali ya Muhimbili tarehe 6 Machi kutibiwa ambapo inaonekana daktari/madaktari walitoa siri hiyo nje lakini baada ya kutoka Muhimbili siku ya pili hawakujua yuko wapi kutokana na usiri wa hali ya juu wa ulinzi wa Rais Magufuli.

Hata gazeti ya Kijasusi liitwalo Africaintelligence halikuweza kujua aliko na likadai habari zinazosema yuko Kenya au India sio za kweli kwa sababu limefanya uchunguzi na kugundua sio kweli.

Kama chanzo cha kifo cha Rais Magufuli kitakuwa ni kudukuliwa kwa pacemaker/defibrillator, hii itakuwa ni aibu na udhaifu mkubwa kwa vyombo vilivyopewa mamlaka ya ulinzi na usalama wa taasisi ya Urais nchini Tanzania. Taasisi ya Ulinzi na Usalama inawezekana ilikuwa imejikita katika ulinzi wa mwili(Physical security ) pekee bila kujiandaa kwenye ulinzi wa saibenetiki(cybersecurity).

Kuna baadhi ya watu watajiuliza, kwa nini pacemaker/defibrillator ya Rais Magufuli idukuliwa kwa sasa?

Mtu mwenye upeo mkubwa atajua muda huu ndio ulikuwa ni muda mwafaka kiujasusi baada ya uchaguzi mkuu 2020 kwa sababu nguvu zilizokuwa zimewekezwa katika Uchaguzi Mkuu 2020 ili kumuondoa Rais Magufuli madarakani kwa njia ya sanduku la kura au maandamano kupitia kwa Tundu Lissu kutofanikiwa.

Ukisikiliza sauti ya tatu utagundua kuwa Tundu Lissu aliwaaminisha ''majasusi'' ana uwezo wa kumtoa Rais Magufuli madarakani kwa kura au maandamano.

Ieleweke kuwa, katika baadhi ya misheni hasa za kijasusi zenye changamano na tata huwa kuna mpango(plan) zaidi ya mmoja. Baada ya mpango wa kwanza kushindwa, mpango wa pili ulichukua nafasi yake na kufanikiwa!

Nadhani hoja za kinadharia kutoka kwa baadhi ya wanasiasa hasa wabunge za kutaka kubadilisha katiba ya Tanzania ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa Urais pia zimeharakisha sana ''mission'' hii kabla hawajaanza kuandika ''miswaada binafsi'' na kupeleka bungeni kwa sababu ungepitishwa bila kikwazo chochote!

Mission accomplished, the rest is history!

NOTA BENE.
Kwa wasiojua, pacemaker/defibrillatorni ni kifaa kidogo cha umeme chenye ukubwa kama kiberiti ambacho hufuatilia na kudhibiti wimbo wa moyo ambacho huingizwa kwenye kifua ili kufuatilia na kudhibiti sauti ya moyo isiyo ya kawaida ili kusukuma damu kwa kiwango kinachotakiwa.
View attachment 1733899
Watu wanacheza na sayansi marehemu aliwekeza kwenye matunguli na ushirikina akawapa nafsi wanasayansi kufanya yao, imebaki historia
 
Baada ya miaka 20 mbele ukweli utawekwa wazi, ndio dunia ilivyo. Si mmesikia mbowe alipanga njama za kuuwa viongozi,inawezekana wanataka kumpa kesi ya kumuua Jiwe
 
Kwanza kabisa vifaa vinavyo weza kudukuliwa ni vifaa vya generation 4 au G4. Kama JPM aliwekewa kifaa hicho miaka ya 80, hakiwezi kuwa na uwezo wa kudukuliwa kwani hakina mfumo wa mawasiliano.

Sasa hivi ndo kuna vifaa hivi vipya ambavyo vimeongezewa mfumo wa mawasiliano unao mwezesha daktari kufuatilia afya ya moyo wako muda wote..na kutoa alert pale ambapo mambo hayaendi vizuri. Hivi vyenye mfumo wa IP ndo vinaweza kudukiliwa
 
Ninachofahamu kwa uhakika kabisaa ni kuwa hicho kifaa kwel kinaweza kudukuliwa lakini sina comment yoyote kwenye kifo cha muheshimiwa
 
Back
Top Bottom