Je, Rais Magufuli alikuwa na Pacemaker au Defibrillator? Ilidukuliwa?
Kwa Matendo ya huyu Mama yakiendelea zaidi nitajua pengine ana uroho wa madaraka na ndie aliyehusika.. time will tell us
 
Wasalaamu!
Kiukweli kifo cha JPM kimeniumiza sana kisaikolojia.
bado naendelea kutafuta ukweli juu ya kifo chake ndani na nje ya JF.
Kifo chake kinaweza kuwa sio cha kawaida!
So much informed but so much careful to conclude!

RiP Magufuli.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
ningefanikiwa kumjua aliyesaidia kumuondoa huyu hayawani ningempa zawadi
 
Wasalaamu!
Kiukweli kifo cha JPM kimeniumiza sana kisaikolojia.
bado naendelea kutafuta ukweli juu ya kifo chake ndani na nje ya JF.
Kifo chake kinaweza kuwa sio cha kawaida!
So much informed but so much careful to conclude!

RiP Magufuli.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Na ulinzi ule unakufaje? Labda kama kajiua mwenyewe hapo sawa maana hakukuwa na mtu duniani analindwa kama yeye
 
Dr Janabi anajua exactly kuhusu issues za pacemaker.

Nadhani hata kama kuna details basi ziko full classified..

Nadhani kuna eneo kama nchi tulikwama na hakukua na namna ya kujikwamua zaidi ya kuchukua table solutions za kipindi hiko.

Namanisha nn??...namanisha kwa nini watu wa screening ya Presidential candidates walijua kuwa Marehemu Rais ,JPM alikua ana issues za moyo na bado wakampitisha awe Rais japo wanajua changamoto zake za afya?

Je hata mpendwa wetu JPM nae hakujionea huruma kwenye hii changamoto yake ya kiafya ya moyo???

Au ndo alijua changamoto zake za kiafya ya moyo ambazo wote tunajua ukiwa na hizi issues za moyo hata mambo hayatikiwi kuwa mengi lakini bado aka opt kufanya kazi ngumu ya Urais?

Au tuikumbuke anaposema "Nime SACRIFICE maisha yangu kwa ajili ya watanzania "????

Au tulikwama pale chamwino kumpata Rais ikabd huyo huyo mwenye changamoto crucial za kiafya ndo awe Rais.???

Sasa watu walio na changamoto yeyote ya kiafya Hawafai kuongoza?

Labda wewe hapo ulipo ni uko fit 100%?

Tuwe na akiba ya maneno binadamu.
 
Nimejiuliza na kufikiria sana sana kuhusu kifo cha Rais Magufuli kilichosababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator.

Kujiuliza na kufikilia kwangu kumetokana onyo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani (Department of Homeland Security-DHS) lililotolewa mwaka 2019 linaloonya makampuni yanayotengeneza pacemaker/defibrillator kuhusu hatari ya kifaa hicho kudukuliwa na wataalam wa udukuzi na kupelekea hata kifo kwa watu waliopandikizwa kifaa hicho.

Ukitaka kusoma onyo hilo unaweza kugonga hapa;
Link>>> Pacemakers and Hacker Dangers

Wizara hiyo ilibainisha kuwa wadukuzi wanaweza kuingilia mifumo ya pacemaker/defibrillator na kuweza kubadilisha mawasiliano yake ambapo inaweza kupelekea mtu aliyewekewa kifaa kufariki.

Wizara hiyo ilienda mbali zaidi na kusema hata wadukuzi ''mwenye uwezo mdogo'' wanaweza kudukua pacemaker/defibrillator na kufanikiwa kuleta madhara makubwa kwa watu waliopandikizwa vifaa hivyo kwa sababu vifaa hivyo havina mfumo wa uhakiki au idhini (authentication or authorization) ambao ni kinga ya mwanzo dhidi ya udukuzi.

Onyo hili lilipelekea watoa huduma ya afya nchini Marekani kuwaita wananchi wa Marekani zaidi ya nusu milioni waliopandikizwa vifaa hivyo na kuwaeleza ukweli wake.

Kama kifaa hiki kinaweza kudukuliwa hata na wadukuzi wenye uwezo mdogo na kuleta madhara au kifo, inafikirisha sana kusikia kifo cha Rais Magufuli kimesababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator. Bear in mind, Rais Magufuli amekuwa na hii pacemaker/defibrillator kwa zaidi ya miaka 10. Why now?

Inafikirisha zaidi baada ya kusoma makala iliyoandikwa na Tundu Lissu kupitia gazeti la Afrika ya Kusini liitwalo Maverick akidai alidokezwa kuhusu hali ya Rais Magufuli na chanzo cha ''uhakika'' kutoka Marekani tarehe 6 Machi.

Ukitaka kusoma makala hiyo gonga hapa;
Link>>> OP-ED: Tanzania’s five years of devastation under the presidency of John Pombe Magufuli

Ukiyachanganua maelezo ya Tundu Lissu utagundua kuwa chanzo cha ''uhakika'' walijua wamefanikiwa ''mission'' ya kudukua hasa baada ya Rais Magufuli kwenda katika hospitali ya Muhimbili tarehe 6 Machi kutibiwa ambapo inaonekana daktari/madaktari walitoa siri hiyo nje lakini baada ya kutoka Muhimbili siku ya pili hawakujua yuko wapi kutokana na usiri wa hali ya juu wa ulinzi wa Rais Magufuli.

Hata gazeti ya Kijasusi liitwalo Africaintelligence halikuweza kujua aliko na likadai habari zinazosema yuko Kenya au India sio za kweli kwa sababu limefanya uchunguzi na kugundua sio kweli.

Kama chanzo cha kifo cha Rais Magufuli kitakuwa ni kudukuliwa kwa pacemaker/defibrillator, hii itakuwa ni aibu na udhaifu mkubwa kwa vyombo vilivyopewa mamlaka ya ulinzi na usalama wa taasisi ya Urais nchini Tanzania. Taasisi ya Ulinzi na Usalama inawezekana ilikuwa imejikita katika ulinzi wa mwili(Physical security ) pekee bila kujiandaa kwenye ulinzi wa saibenetiki(cybersecurity).

Kuna baadhi ya watu watajiuliza, kwa nini pacemaker/defibrillator ya Rais Magufuli idukuliwa kwa sasa?

Mtu mwenye upeo mkubwa atajua muda huu ndio ulikuwa ni muda mwafaka kiujasusi baada ya uchaguzi mkuu 2020 kwa sababu nguvu zilizokuwa zimewekezwa katika Uchaguzi Mkuu 2020 ili kumuondoa Rais Magufuli madarakani kwa njia ya sanduku la kura au maandamano kupitia kwa Tundu Lissu kutofanikiwa.

Ukisikiliza sauti ya tatu utagundua kuwa Tundu Lissu aliwaaminisha ''majasusi'' ana uwezo wa kumtoa Rais Magufuli madarakani kwa kura au maandamano.

Ieleweke kuwa, katika baadhi ya misheni hasa za kijasusi zenye changamano na tata huwa kuna mpango(plan) zaidi ya mmoja. Baada ya mpango wa kwanza kushindwa, mpango wa pili ulichukua nafasi yake na kufanikiwa!

Nadhani hoja za kinadharia kutoka kwa baadhi ya wanasiasa hasa wabunge za kutaka kubadilisha katiba ya Tanzania ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa Urais pia zimeharakisha sana ''mission'' hii kabla hawajaanza kuandika ''miswaada binafsi'' na kupeleka bungeni kwa sababu ungepitishwa bila kikwazo chochote!

Mission accomplished, the rest is history!

NOTA BENE.
Kwa wasiojua, pacemaker/defibrillatorni ni kifaa kidogo cha umeme chenye ukubwa kama kiberiti ambacho hufuatilia na kudhibiti wimbo wa moyo ambacho huingizwa kwenye kifua ili kufuatilia na kudhibiti sauti ya moyo isiyo ya kawaida ili kusukuma damu kwa kiwango kinachotakiwa.
View attachment 1733899
Kukisikia kifaa kinaweza kudukuliwa ujue yupo anaye miliki mamlaka ya kukiendesha sasa ulitakiwa kujua kua maadui wakubwa wa magufuli walikuwa wazungu wenye mamlaka na kamili ya hicho kifaa inawezekana akikudukuliwa ila mamlaka husika ndiyo iliyo fanya figisu kwa kupewa muongozo kutoka kwa wakubwa wa dunia ,jinsi wewe ulivyo andika umemaanisha wanao kimiliki hicho kifaa ni malaika awawezi kutumika kumuangamiza mtu. Mfano Osama angekuwa anatumia hicho kifaa na wamarekani kugundua basi kusinge kuwa na haja ya kukidukua zaidi wange wasiliana na waundaji ili kukiujumu tu
 
Hiyo makala niliisoma vizuri.

lakini kuna point moja umeruka sehem. kifaa hicho mawimbi yake ni mafupi mno kiasi kwamba mtu lazima awe so close kuweza ku access hiko kifaa.

Nut in real sense. the way rais alifichwa. ilikuwa ni ngumu sana. kama PM na mawaziri hawakujua, nani angemsogelea rais zaid ya walinzi wake na madkatari wa usalama?

Plus Tanzania hatufikia uwezo wa hacking kiasi hiko. bado tuna safari ndefu.

All in all our late president aliondoka kwa tatizo la moyo. hizi theory sijui ilikuwa hivi ilkkuwa vile hazimrudushia uhai.

Wanausalama walishatoa sababu. Apumzike kwa amani
Kwani waliokuwa wanamchukia magu ni watz tu ? Je watz na wazungu waliokuwa wanaona influence ya magufuli kwa bara la africa inaweza kuathili maslai yao hao awawezi kuhusika pia hicho kifaa waliokiunda awawezi kutumiwa na mamlaka za kidunia kumdhuru mtu na mawimbi kuwa mafupi ni swala la kiinjinia unajuaje kama ndani ya icho kifaa kuna namna ya kuongeza hayo mawimbi
 
Kama hamtakuwa wakweli kuhusu Corona mtawapoteza wengi.
Siyo korona iliyo muua magu kwa sababu angekufa kwa korona ingetangazwa na ingekuwa Wimbo wa taifa maana waliotamani magu kufa na korona ni makada ila haikuwa hivyo wewe huoni wanavyo angaika kushabikia chanjo na njia za magharibi kupingana na magu sasa ingekuwa kafa na korona ingetangazwa ili kufanikisha mikakati yao kuhusu covid
 
Kwani waliokuwa wanamchukia magu ni watz tu ? Je watz na wazungu waliokuwa wanaona influence ya magufuli kwa bara la africa inaweza kuathili maslai yao hao awawezi kuhusika pia hicho kifaa waliokiunda awawezi kutumiwa na mamlaka za kidunia kumdhuru mtu na mawimbi kuwa mafupi ni swala la kiinjinia unajuaje kama ndani ya icho kifaa kuna namna ya kuongeza hayo mawimbi
Serikali imeshalitolea ufafanuzi hili suala. kifo kimetokana na nn. the rest are just conspiracy theory tu.
 
Back
Top Bottom