Wasalaamu!
Kiukweli kifo cha JPM kimeniumiza sana kisaikolojia.
bado naendelea kutafuta ukweli juu ya kifo chake ndani na nje ya JF.
Kifo chake kinaweza kuwa sio cha kawaida!
So much informed but so much careful to conclude!
RiP Magufuli.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Pole sana, inaeleweka kwa mtu kama wewe.
Lakini katika hili ngoja nikusaidie pa kuanzia utafiti wa maswali yako.
Kwanza tafuta taarifa hii: Je, alipimwa na kuonekana hakuwa na chembe zozote za COVID-19?
Lingekuwa jambo la kushangaza sana kama hawakupima chochote juu ya hilo wakati gonjwa hilo likiwa limeshika kasi.
Wakikwambia kwamba hawakufanya vipimo vyovyote juu ya ugonjwa huo, basi anzia hapo na nadharia yako uliyonayo kichwani.
Ni sababu zipi zilizowazuia wasipime kuondoa uwezekano wa ugonjwa huo kuwa sehemu ya mauti yake.
Watu wake wa karibu, kama yule Katibu wake Mkuu, walipima akaonekana hana ugonjwa huo? Kama hawakupima, hapo bado kutaonyesha 'pattern' ya mambo ambayo hayakuwa ya kawaida.
Kwa bahati (nzuri), Maalim alijitangaza mwenyewe kwamba alipima akakutwa na COVID-19, kwa hiyo kifo chake hakina utata; lakini kinaweza kuunganishiwa hapo na cha Magufuli na Katibu wake Mkuu, kwa sababu Maalim na Dr Mwinyi walikuwa na kikao na Magufuli wiki chache tu kabla ya Maalim kulazwa hospitalini.
Labda kona nyingine uanze kupiga picha: ilikuwaje Kikwete achukue tahadhari za kuvaa barakoa katika mikusanyiko iliyofuatia kifo cha Katibu Mkuu, yeye alikuwa na taarifa tofauti na wengine?
Hata uwaze vipi: Magufuli aliuliwa na COVID-19 kwa kiburi chake tu!
Sasa mnataka kutafuta visababu vya uongo na kweli vya kuwachanganya navyo waTanzania na kupotosha madai ya katiba mpya.