Je, safari hii CCM hamjakubaliana?

Je, safari hii CCM hamjakubaliana?

uko sahihi, uko makini na uko chonjo mbaya sana, comrade

Yes hicho ndicho.

bila ccm imara na madhubuti inchi itayumba....
Kwa ushetani mwingi unaofanywa na CCM, serikali na viongozi wake, utulivu wa Tanzania unasababishwa na uvumilivu wa kupindukia wa wananchi.

Ujinga, uharamia na ushetani mwingi uliowahi kufanywa na CCM, kwa nchi nyingine ingekuwa tayari ni sababu ya nchi kutokukalika.
 
Ikiwa miaka yote wao ndiyo wako Madarakani na nchi haikuyumba, kwanini wakiwekwa pembeni nchi iyumbe kama siyo wao CCM watakaoyumbisha??
Mfano CCM ikae pembeni. Unafikiri kwa Tanzania ya Sasa, chama gani kinaweza kuongoza nchi? Kwa mfano tu!?
 
kwa kweli hii ccm ya sasa ni dhaifu, wazee wake wapo ila kuna vijana wahuni wamewaamini chamani na kuwapa madaraka ila hao vijana wanakiharibu chama na kuwa dhaifu badala ya kuwa imara
CCM Ina utamaduni wa kuwalea vijana na Kisha kuwakasimu madaraka muda unapofika. Pia CCM Ina tabia ya kwenda na wakati yenyewe pamoja na viongozi wake ndio maana ipo madarakani Jana, Leo na kesho. Madam vijana wameaminiwa na chama basi jua wameiva.
 
Kwa ushetani mwingi unaofanywa na CCM, serikali na viongozi wake, utulivu wa Tanzania unasababishwa na uvumilivu wa kupindukia wa wananchi.

Ujinga, uharamia na ushetani mwingi uliowahi kufanywa na CCM, kwa nchi nyingine ingekuwa tayari ni sababu ya nchi kutokukalika.
jamani nyie watakatifu mmekaa upande gani ili jamii ijoin pande izo asseeee
 
Mfano CCM ikae pembeni. Unafikiri kwa Tanzania ya Sasa, chama gani kinaweza kuongoza nchi? Kwa mfano tu!?
Nani kakuambia lazima Tanzania iongozwe na chama? Watanzania wenye uwezo wamejaa tele, ila hawataki kujitokeza kuhofia siasa za kipuuzi za vyama hususani ccm.
 
Mwalimu alikuwa sahihi. CCM imara ni ile inayoongoza kwa kuzingatia haki. Siyo hii CCM matapeli isiyo na ushawishi, iliyobakia kupora kura kama njia ya kubakia madarakani. CCM ya sasa ni mkusanyiko wa wahuni na majambazi.
Pole sana Dogo kwa kuamini hivyo.
 
alaaah,
sasa elekezeni jamii elekee wapi sasa kuepuka janga 😀
ili iwe salama
Rasimu ya Warioba ila matakakwa yetu wananchi. Ila genge haramu lijiitalo ccm limechezea matakwa yetu. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi yatapelekea maoni Yale ya wananchi kutengeneza katiba Yao.
 
Nani kakuambia lazima Tanzania iongozwe na chama? Watanzania wenye uwezo wamejaa tele, ila hawataki kujitokeza kuhofia siasa za kipuuzi za vyama hususani ccm.
Kama wewe vile sio? Kwa maandishi hayo unayopost hata Mamaako HAWEZI kukuachia genge lake umuuzie sembuse nchi!? Ahahahahaha!!!
 
Kama wewe vile sio? Kwa maandishi hayo unayopost hata Mamaako HAWEZI kukuachia genge lake umuuzie sembuse nchi!? Ahahahahaha!!!
Huu ujinga wa ccm kuamini hicho chama haramu tu ndio kinaweza kuongoza nchi, hata KANU ya Kenya walijidanganya hivyo hivyo, Leo hii KANU haipo, na Kenya ina uchumi mzuri kuliko wetu.
 
Rasimu ya Warioba ila matakakwa yetu wananchi. Ila genge haramu lijiitalo ccm limechezea matakwa yetu. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi yatapelekea maoni Yale ya wananchi kutengeneza katiba Yao.

machafuko ya hali ya hewa au mchafuko wa tumbo?
jeshi la wokovu 😀

kama mnataka katiba ya warioba si muende akawapatie, si yupo mzee huyu ambae sote tunampenda na tunamuheshimu sana....

2026 tuaanza mchakato wa kupata katiba mpya ya wananchi wa Tanzania wote sio ya fulani....
 
Uhai wa CCM ndio usalama wa Tanzania

Ndani ya CCM kuna kitu kinaitwa kukubaliana bila hicho hakujawahi kuwa na ustawi. Mfano wana CCM walikubaliana Mzee Mwinyi awe Rais baada ya Nyerere

Kipindi cha Kiba Ben Akiba JK, Salim walikuwa na nguvu ila walikubaloana Ben aongoze. Ben alimpenda sana Sumayi ila wakakaa walikubaliana JK aongoze. JK nae alimpenda sana Membe amwachie kiti lakini walikaa wanakubaliana achukue JPM

Sasa JPM hayupo yuko Samia. Utaratibu wa kukubaliana usizarauliwe kwa kuwa ustawi wa CCM ndio maendeleo ya Tanzania. Kuna vitu vinaendelea inaonesha hamjakubaliana, ndio maana ups and down,

Namshauri Mama Samia akae na wakubwa wenzie wakubaliane amalize 30 kisha awape mtu wanayemtaka

Makundi hayana afya ya muda mrefu
Tukubaliane kumfukuza Paul Makonda a.k a DAUDI ALBERT BASHITE
 
machafuko ya hali ya hewa au mchafuko wa tumbo?
jeshi la wokovu 😀

kama mnataka katiba ya warioba si muende akawapatie, si yupo mzee huyu ambae sote tunampenda na tunamuheshimu sana....

2026 tuaanza mchakato wa kupata katiba mpya ya wananchi wa Tanzania wote sio ya fulani....
Warioba Hana katiba, yeye alikuwa Mwenyikiti wa kamati ya kukusanya maoni ya wananchi, kisha yakawekwa kwenye rasimu. Usichanganye katiba na rasimu. Maoni Yale yalikusanywa kisheria, na ulikuwa mchakato halali na huru. Unaposema katiba ya mtu unaonekana umekijita kwenye siasa za Hila zaidi.

Nasema hivi, machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatatupa katiba ya wananchi, sio ya genge hatari la ccm.
 
2026 unaanza mchakato wa katba mpya upya.

maoni ya watanzania yatakusanywa kwa uswa, uwazi na weledi mkubwa sana, yatachakatwa kwa umahiri sana katika hatua mbalimbali mahususi za kisheria na hatimae katiba mpya ya waTanzani wote itapatikana, na Inshaalah itafanyika sherehe kubwa sana, siku ya kuanza kutumika.

hiyo ya fulani, sijui eti alikua nani bakini nayo kwaajili ya refference na accademic purposes kama inafaa...

😀 unanichekesha sana eti machafuko, hayo ufanya humu mtandaoni na kwako na ni hapohapo nyumbani tena ndani ya fensi. Huku inje wananchi wanfanya shughuli zao kwa bidii na vyombo vya ulinzi vikihakikisha amani...

hiyo ya mapinduzi ya jeshi la wokovu right?
 
kukubaliana kutofautiana ni Jambo zuri sana kwa mustakabali wa uimara na uhai wa Taasisi
JK alikuwa anamtaka membe lakini wazee walikataa wakamtaka JPM JK angeamua kutumia nafasi yake kama Mwenyekiti ni dhahiri membe angakuwa mgombea wa CCM lakini walipokaa na kukubaliana hata kama hakufurahishwa JPM akawa mgombea na Rais wa JMT
 
Back
Top Bottom