Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Shetani ni nafsi yako inapotenda kinyume na matakwa ya Mungu. Jiangalie ulivyo ujue ukitenda kinyume na makusudio ya Mungu basi Shetani ndivyo alivyo ni wewe.Ni dhahiri asilimia kubwa ya wanaofanya makosa huyahusianisha na kitu kisichoonekana na kinachokinzana na Mungu kiitwacho shetani. Je, shetani kweli yupo? Anaishi mazingira yapi na kwa nini Mungu anashindwa kumdhibiti ili binadamu waishi kwa ustaarabu na kutotenda dhambi kabisa? Je, nani anaweza kuzithibitisha theologies za huyo shetani kiumbo, mtazamo, mnyumbuliko na kiakili bila kuhusianisha imani?
Learning has no boundaries......