Wakati niko olevel form 4 na necta ndio hiyo imekaribia nilikuwa najifanya mgumu, sina muda na mademu hadi siku moja wakati niko prepo pembeni yangu akakaa msichana mmoja wa form 3, kujaribu kumchunguza alikuwa serious na msuli ile mbaya, wakati prepo imeisha nikapata nguvu za ajabu nikanyanyuka na kumfuata hadi tukafika sehemu yenye giza (hapo yeye hana idea kama namfuata) kisha jikajikaza...
"mambo?
"poa
"hivi unaitwa nani?
"Rehema
"ahaa, sawa.
Nikajiona shujaa kumbe ni failure nyingine tuu. Yaani nauliza maswali kama polisi!?
Nikaona isiwe kesi
Nikaanza kuuliza wasichana wa darasani kwetu kuhusu msichana wa form 3 anaitwa rehema.
Naambiwa hakuna mtu kama huyo. Dah, basi bwana!
Zikapita kama wiki 2 hivi akaja tena kusomea darasani kwetu. Dah kila nikimuangalia halafu nikiangalia vitabu vyangu sielewi nasoma nini kabisa.
Wakati prepo imeisha akaondoka na rafiki yake kwenda bwenini, nikanyanyuka na kuwafuata, nilipowakuta.
"Mambo zenu?
(Wakacheka)halafu wakajibu...
"Poa
Angalau safari hii nikaweza kuongea nao mambo kadhaa halafu nikajitambulisha kisha nikamuuliza yule targeted jina lake.
This time akasema anaitwa Happy.
Nikamuuliza mbona ulisema unaitwa rehema? Akadai ni jina lake jingine.
Baada ya pale kila nikimuona namuangalia kwa kuibia hadi akawa kama anasanukia mchezo. Akawa anakuja darasani kwetu mara moja moja lakini mara hii na yeye akawa ananiangalia kwa kuibia.
Kiufupi sikujua baada ya pale nifanye nini lakini nilitokea kumpenda sana. Basi akaanza kutuma salamu kupitia wasichana wa darasani kwetu. Mimi nikaona siwezi chochote nikawa kama nimekata tamaa kabisa.
Basi siku moja kabla ya necta, yaani Jumapili kesho civics nikaletewa barua na msichana wa darasani kwetu.
Baada ya barua akaniambia yule pale kaniambia nikupe, nikanyanyua kichwa nikakutana uso kwa uso na Happy aliyekuwa anaongea na wasichana wengine pale mlangoni, dah moyo ukapiga paaah.
Kufungua nakuta best wishes na mambo mengine kama hayo mwisho kabisa I LOVE YOU. Kidogo nizimie.
Nikajikaza nikanyanyuka nikamfuata kisha nikamvuta hadi nje ya darasa kwenye giza.
Kwa sauti ya chini yenye msisitizo nikadeclare upendo wangu kwake.
Akaniambia anafeel the same kwangu.
Tukaongea wee mwisho tukawa tumeegemea ukuta, nikajikuta nakula mate. (Kesho necta!).
Ikabidi niage nikaendelee kusoma. Kufika darasani hakuna kitu kinaingia kichwani. Yaani hakuna.
Necta Nikafanya vizuri tuu. Kasheshe likaja kwenye kumuaga baada ya kumaliza shule...
Shule ilikuwa na utaratibu wakati wa form four kumaliza shule wasichana wanawekewa ulinzi wa hali ya juu. Basi nikakosa namna ya kumuaga face to face nikaandika ujumbe nikautuma ukiwa na contacts zangu na kila kitu lakini hadi leo hajawahi kunitafuta.
Tangu nizaliwe sijawahi penda kama vile, nakiri ni uzembe wangu uliofanya nimpoteze Happy hadi leo.
Samahani kwa uandishi mbovu.