Je, Taasisi na Mashirika wafanye saili kama kipindi cha Kikwete?

Je, Taasisi na Mashirika yafanye saili kama kipindi cha Kikwete?

  • Ndiyo

    Votes: 29 49.2%
  • Hapana. PSRS iendelee kukanda tu 🀣

    Votes: 30 50.8%

  • Total voters
    59
  • Poll closed .
Majobless na mabest losser wote kaeni mkao wa surprise kwanzia j5 mpaka jmosi kutakuwa na TU PDF za halmashauri ni mwendo TGS D Yan πŸ˜‚
 
Ni kweli kufundisha ni kipaji, unaweza kuwa ni genius lakini kufundisha mtu Huwezi,
Lakini Huwezi kumpata tutorial assistant Kwa panel ya siku Moja,
TA inahitaji maandalizi ya Muda kumchunguza muhusika
 

Huyu mleta mada hata uongozi haumfai kwasababu ni mbinafsi hata akipata kama bado atafanya ubinafsi na ndio watu kama hawa huwa wakiwa vitengo kwasababu ya ubinafsi wanaingiza ndugu zao kazini. Mimi hapa nina rafiki yangu juzi tu hapo kapata kazi za LGA zile alikuwa getto hana mchongo wowote lkn PSRS imefanya haki kapata kazi hana connection yoyote na mimi mwenyewe nilifanikiwa kwenda kufanya oral ya TRA Bila connection yoyote. Mtoa mada pambana na interview za PSRS usitegee back up ya connection kupata kazi falaaa wewe
 
Big no
 
Kuna wakati huwa tunarejea ya zamani sio kujifanya tunaenda mbele huku tunabomoa
 
Kuna wakati huwa tunarejea ya zamani sio kujifanya tunaenda mbele huku tunabomoa
Ni kweli Mzee, PSRS hawawezi mudu kusimamia saili zote za taasisi na mashirika ya Serikali,
Kwa sababu ya ubunifu wa rasilimali fedha,watu, na uzoefu NA VIFaa
 
Kitenge umemsikia shangazi, ameseme mulete report ya CAG , ijadiliewe bungeni, kazi kwako Mzee 🀣🀣
 
inasemekana wachaga wamejimilikisha ile
Kumbuka wachaga na wahaya ndio walikuwa ndio wasomi wengi kuliko sehemu nyingine,.

Hata Nyerere alikuwa sometimes anawaacha wahaya na wachaga, nakuchagua watu ambao hawakwenda shule, Ili kuweka usawa
 
Iendelee PSRS, Kwenye hizi ajira za Waalimu na Madaktari zilizotangazwa umemsikia kabisa waziri wa wizara husika akisema amepokea simu na vimemo kutoka kwa waheshimiwa wengi wakiomba ndugu zao waangaliwe unategemea bila kua na mfumo wa kusimamia zoezi hilo hali itakuwaje???
 
Hata kitenge naye anapΓ ta vimemo na sms au ww ni mgeni PSRS
 
Oya wazee Kuna taarifa nimepewa aisee daa,
Chawene amesha honga wabunge million 3, direct deposit kupitia equity, Ili waje kutetea bajeti yake, ikiwemo ishu ya Ukosefu wa ajira na PSRS.

Yan badala matatizo ya PSRS yabainishwe , ikiwemo upungufu wa wafanyakazi,uhaba wa vitendea kazi, bureaucracy, kuungezewe POSHO πŸ™„,

na kutatuliwa Kwa haraka kwa ubunifu ulio mzuri pasipo kuumiza jobless.

Wao wako bize Kufanya makosa zaidi, daa hii nnchi Ina viongozi wa baya sana.

Natumai kunguru wa chamwino watampatia Intel prezdaa
 
Ila naona malengo mazuri kabisa ya mkuu wa nchi, vibali vinatolewa ila usimamizi wa mchakato wa ajira na namna ya kuingia kwenye system kuna watu wamefanya kama kilakitu chakwao, wanaweka watu wao, hawafuati kanuni zinazo waongoza, wanafanya kazi kimazoea hawajui kuwa kuna kesho wao umri umeenda ndg zao wataingiaje kwenye asali baada ya wao kutoka hawafikirii. Wenzetu mataifa mengine wapo serious na ajira ambae anasifa anapewa bila konakona. Sasa ajira ilitangazwa mwaka jana tena may na june hii ni April na itafika july watu hata kazini hawajaitwa huu ni uzembe na ni magumashi ambayo Psrs hawana majibu ya kutupa tuwaelewe.Mambo ni nyoronyoro kama jongoo, yaani mwaka mzima wa fedha unasubiria kazi daah inaunmiza sana.
Hawa jamaa ifike sehemu wawe reliable mambo sijui paper limevuja, cjui nani alikuwa na maswali kabla ya interview, mara mnasubiri placement mwanka mzima tatizo ni nini.Mnajua data zote ni taasisi gani, wilaya gani zinataka watumishi kibali kipo tayari sasa siasa yanini kwenye hayo mambo,mkielemewa mseme muongezewe wataalam, nina hofu PSRS hamana wataalam wakutosha, Miundo mbinu na procedure zenu bado sana.
Maana kama una wataalam, professionals na watu wenye uzoefu hamuwezi enda hivyo. Hapo nimezungumzia wataalam wakutosha
Watu wa ICT tena Cerified IT ambao wapo current, watu wa mitihani maana hata paper zenu hazieleweki kesho hivi kesho vile ni vile mnajisikia kufanya au mtu kaamka anasema hii paper iwe hivi hamna utaratibu, tuna taka ethics za kazi yenu zizingatiwe.
Punguzeni mlolongo, mambo ya vikako kila siku vikao mambo yapo wazi yanawapunguzia ufanisi wa kazi.
Data base Data base ifanye kazi ,vijana tumechoka kurudi kufanya mausaili kila muda bila sababu. Leo mmetangaza wataalam wa maendeleo ya jamii lakini mnao wengi kwenye data base si walifanya mwaka jana usaili mmewaita wale wote, wapeni kazi madogo mtu kama amefaulu chuo na anaweza kujieleza kamati ya usaili imempa atleast passmark ya 50 mpeni kazi huo ndo utaratibu na ndio sheria, na kanununi inataka, tena mapaka waishe wote kwenye kanzi data ndio mtangaze..kuita kwenye usaili watu wanatoka tunduma, rombao, tarakea mwingine mbjnga, mwingine sengerema, nduta, nyasa, ludewa mnawatesa watoto wa watu provided hawana kazi za msingi za kuwainguzia kipato cha hayo magharama.
Hayo lazima tuongee na tutaongea mpaka kieleweke maana hiyo ni haki ya kila mtanzania .
Linswena
 
Mashirika na taasisi za umma ziajiri zenyewe sababu sekretarieti ya ajira imeshindwa kufanya jambo hili kwa ufanisi.
 
Bunge la Wananchi
 
Kijana mwaminifu
 
Mimi binafsi naona PSRS kuna urasimu wa hali ya juu..huwez ukaset kwamba kazi ya uhasibu lazima mtuu awe na CPA wakati watu wapo wenye uwezo wa utendaji wa kazi Hali ya juu..CPA haifanyi kazi..kazi za uhasibu na procurement ziwe neutral..sio kila mtuu akimalza chuo ana uwezo au mdaa wa kufanya Hizo mambo..mm naona hizi kazi za kuajir ziludshwe kwa wahusika
 
Apa upo sahihi sikupingi. Ni mambo ya ajabu kabisa ajira za MDAs & LGAs nafasi 1,769 tangu zitangazwe zimetimiza mwaka sasa. huu ni uzembe wa hali ya juu.
 
Huenda wakawa wanafanya kazi nzuri,ila hakuna uwazi haswa upande wa Oral interview,hawatoi result za oral interview ili msailiwa aone kabisa kama ameshindwa au amefanikiwa hata kuwepo kwenye database.
Pia kuwepo uhusiano wa result za written na oral interview.
Pia wanatumia muda mrefu sana kurelease majina ya waliofanikiwa kupata ajira,mpaka msahiliwa unajiuliza hivi hakuna uhitaji wa nguvu kazi wa haraka kwenye taasisi zilizo toa tangazo la ajira?
-Pia ukifanikiwa kuongea nao,jibu lao kubwa ni kua wapo wachache sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…