Je, TRA wamesikia kilio chetu cha Ushuru wa kuingiza magari?

Je, TRA wamesikia kilio chetu cha Ushuru wa kuingiza magari?

Mama SSH nimemkubali sanaa,kuna gari wakati wa JIWE kodi ilikuwa 6m ila sasa nimeona ni 4.5m....#SSH_MIKUMI_TENA_MATHA(MAKE TANZANIA HAPPY AGAIN).

JIWE alikuwa hataki watu wapate raha,alikuwa anataka watu waishi kama mashetani.
Umeona sasa??? Na mimi ndo nilikua nauliza hili swala kama kuna mtu alishacheki gari Fulani kabla hapo aangalie kama kuna mabadiliko au ni kwamba system ina matatizo. Sijaamini hata mimi aisee

SSH misaba tena😂😂
 
Si kweli. Usitumie mfano mmoja tu kutaka kuwapa matumaini watu. Ushuru uko vilevile.
Kula mtori nyama ziko chini( Soma maoni ya watu wengine mkuu)

Mimi nimeuliza swali kwa gari niliyokua na kumbukumbu nayo. Na leo naenda kuiagiza kabisa manaake hela ilikuwepo nilikua naongeza ongeza.Ila saivi inatosha na chenji inabaki
 
Hoja hapa ni kwamba ushuru wa magari umepungua. Nenda kafanye trials kwenye calculator kama wewe ni mágica magari utaona tofauti tu.

Ila kama umedandia treni kwa mbele hutaelewa chochote kwenye hii mada.
Kadandia treni huyo sidhani kama hata alielewa jinsi calculator inafanya kazi mkuu. Ndomaana hapa tunaelimishana. Na mimi nimeuliza swali kama kuna mtu kaona hayo mabadiliko pia. Sasa naambiwa bangi hahahaaa
 
Kikokotoo kinaonesha ushuru kushuka kwa magari yote au hayo makubwa kubwa wanayoyaita ya "kifahari"
Ngoja tusubiri kama kuna mtu ana kumbukumbu ya gari nyingine. Mimi nimeweka hiyo ninayojua nilikua nihifadhi kumbukumbu
 
Mm nasoma nabaki nacheka tu.

Kuna mtu kabisha hapo kuwa bei za gari ni ndogo ndo maana kodi ni tofauti. Sasa si akaombe zawadi ya gari huko nje asilipe kodi.
Hahahaaa inafurahisha mkuu ila ndo JF kila mtu mjuaji. Sema ndo tunaelimishana
 
Mbona ni simple math tu, tax ni variable inategemea na CIF value. Sasa ya kwanza imeweka CIF dolla 26k, ya pili ukaweka CIF dollar 13k ambayo ni almost 50% less, ndio maana na kodi imeshuka kutoka 31k to 15k. Haina uhusiano na mabadiliko yoyote ya kodi. Ni math tu hapo. Check between lines.
 
Mkuu hebu tuwekee na data za gari ya uchumi wa kati IST
Sasa IST hata sijawahi kuiagiza so sijui bei yake(kodi) hapo kabla mkuu na siwez kujua kama kuna mabadiliko
 
Kwa nini?

Ni kwamba kati ya Watanzania takriban milioni 60, ni yeye tu mwenye kuiweza hiyo kazi mpaka alazimishwe kuifanya hata kama hataki?

Fikra dhaifu sana hizo katika karne hii ya 21!
Mbona ulikuwa unataka Magufuli alazimishwe atake asitake?🤔🤔🤔
 
Labda gape ya tofauti itakayosababisha ulipe dumping fee kubwa. 2017 na 2018 ni same group.
Nisaidie kumuelewesha huyu. 2017 na 2018 ni kodi moja. Labda kama wakitumia bei uliyonunulia kule ya 2018 itakua kubwa kidogo. Ila kama ulipata kwa gharama nafuu unarudi hapo kwenye makadirio yao ambayo inakua sawa tu
 
Hiyo comparison ina shida. Ya kwanza ina CIF dollar 26k na ya pili ina CIF dollar 13k. Hapa kuna tofauti ya 50% less. Ndio sababu na kodi imeshuka kutoka 31k to 15k. Ni math tu kuwa kodi ni dependent variable ya CIF value. Hakuna mabadiliko ya kodi.
 
Nisaidie kumuelewesha huyu. 2017 na 2018 ni kodi moja. Labda kama wakitumia bei uliyonunulia kule ya 2018 itakua kubwa kidogo. Ila kama ulipata kwa gharama nafuu unarudi hapo kwenye makadirio yao ambayo inakua sawa tu
Njia nzuri ya yeye kuelewa ni kufanya kwa vitendo. Aagize gari.
 
Sio kweli hapo bei ya hizo gari ni tofauti (CIF).
Therefore lazima kodi itakuwa tofauti.
Usiangalie jina la gari angalia CIF
Sasa unajua CIF wanavyokadiria TRA mkuu? Tuanzie hapo kwanza

Yaaani TRA wanakuwa na makadirio yao labda tuseme 13,000 dola halafu wewe ukinunua 10,000 manaake unalipa kodi ya 13,000 ila ukinunua 15,000 basi unalipa kodi kwa hiyo 15,000

Sasa kilichotokea ile makadirio ya TRA yameshuka toka 26,000 mpaka 13,000 huo ndio msingi wa hoja yangu

Tu nacho lala nikawa siku zote ni MAKADIRIO kuwa juu kuliko uhalisia

Nadhani umenielewa. Hiyo CIF hapo sio mimi niliyeweka(kutokana na bei ntakayonunua) hiyo ni makadirio ya TRA
 
Maza Atake asitake lazima aongezewe, akikataa alazimishwe yule. Suluhu mikumi tena.
Niongezee sauti mkuu tafadhali hii haisikiki!
Mikumi na tano kwake mama Raisi?? 😅
Mpango atakuwa pembeni huko anajiona fala sana, maana yeye ndiye engineer mkuu wa hizo vyanzo kandamizi za makusanyo.

Everyday is Saturday................................😎
 
nadhani inategemea magari hayo mawili yalikuwa na hali gani na yalishatembea maili ngapi kwani CIF zake zinatofautiana kwa karibu 100%, moja lina CIF value ya US$26.6k na jininge lina CIF value ya US$13.3k! Kwa hiyo kodi zake bado ni zile zile, yule wa US$26.6k analipa Ths 23.32m na huyu wa US$13.3k! analipa Ths 15.97m ambayo ni ratio ile ile.
Hiyo CIF ni makadirio ya TRA sio bei ya kweli ninayonunulia South Africa. Kwahiyo wamepunguza makadirio yao kwa 100%
 
Back
Top Bottom