Je, Tundu Lissu anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania?

Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?

Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Hatutaki Rais mwenye sifa bali moyo wa kupenda watu na nchi yake.Nyerere aliwapenda watu na nchi yake na laiti angekuwa Rais ktk nchi ya kidemokrasia kama Sasa,wananchi tungefaidi uchumi wetu
 
Hatutaki Rais mwenye sifa bali moyo wa kupenda watu na nchi yake.Nyerere aliwapenda watu na nchi yake na laiti angekuwa Rais ktk nchi ya kidemokrasia kama Sasa,wananchi tungefaidi uchumi wetu
Umeongea pointi maana hawa wengine wazalendo uchwara wamejaza maPhd tu kichwani. Ila wanachotufanyia .......hatuna hamu.
 
Una maanisha kuwa Rais lazima apime consequences ya kila neno na tendo lake?
 
spinning!
 
"By Lucas Mwanshambwa".
 
Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anazo sifa kumzidi Mwinyi, Kikwete na ningesema hata Magufuli, isingekuwa uigizaji wa uzalendo aliojaribu kuuonyesha.
Labda sifa ya kuwa mgombea wa kwanza kuwa mkimbizi, siyo urais.
 
Chadema ni chama kikubwa na makini hata Nyerere aliyasema hayo. Lakini chadema inaendelea kupoteza umaarufu wake sasa kutokana na:
1. Tangu enzi hizo Mwenyekiti wa chama lazima awe wa kabila hilohilo kutoka hukohuko.
2. Wagombea wake wa Urais kutoka CCM na kisha kurudi CCM tena (imani inapotea)
3. Wabunge wa chadema kuhamia CCM na vyama vingine bila chama kuwaomba msamaha hadharani wapiga kura wao walipiga kura, kuhesabu kura na kulinda kura za wagombea wa CDM. Watu wanapoteza imani na wagombea wa chadema, hawana imani nao tena.
4. Kuyakubali matokeo ya uchaguzi waliyoyasusia kimyakimya bila kuwafahamisha wapiga kura wao. Mfano, wanataka akina Halima wafukuzwe ubunge ili wapeleke watu wao wengine kwenye bunge ambalo walisusia matokeo yake ya uchaguzi.
5. Kulalamika majukwaani kuliko kutoa sera zao. Trump kila akipa nafasi huwa anawaambia Wamarekani wenzake kama akirudi tena madaraki 2024 atafanya nini tofauti na Biden kwenye kila jambo.
 
Una maanisha kuwa Rais lazima apime consequences ya kila neno na tendo lake?
Yeah mfano Kulikua hakuna haja ya kuongelea au kukosoa kauli za "hakuna kama Mama". Au hakuna haja ya kwenda Chato na ukaanza mkosoa JPM hata JPM alivyoenda Ikungi na Manyoni alimpamba sana Lissu na kumuita "handsome boy... Akasema ana akili sana na atampa kazi serikalini kwake" that's PR

Sasa Lissu yeye Hana unafiki (Ni kitu kizuri) ila Kwa siasa zetu ni ngumu sana kuungwa mkono na makundi yote. Najua kura zikiwa huru na haki Lissu anamshinda Samia obviously ila tunaongelea Ili awe Rais BORA ni vizuri akapata PR nzuri kuelekea 2025.
 
Wagombea wake wa Urais kutoka CCM na kisha kurudi CCM tena (imani inapotea)
Labda Lowassa tu ila Mbowe, Dr Slaa na Tundu Lissu waligombea Urais wakiwa wanachama hai wa Chadema sio chini ya miaka 15.
Wabunge wa chadema kuhamia CCM na vyama vingine bila chama kuwaomba msamaha hadharani wapiga kura wao walipiga kura, kuhesabu kura na kulinda kura za wagombea wa CDM. Watu wanapoteza imani na wagombea wa chadema, hawana imani nao tena
Hiyo sio kazi ya CHADEMA, mbunge kama akisaliti unalaumuje chama?

Kuyakubali matokeo ya uchaguzi waliyoyasusia kimyakimya bila kuwafahamisha wapiga kura wao. Mfano, wanataka akina Halima wafukuzwe ubunge ili wapeleke watu wao wengine kwenye bunge ambalo walisusia matokeo yake ya uchaguzi.
CHADEMA Haina mpango wa kupeleka wabunge maana halitambui wabunge waliopo maana wote waliingia kwa wizi. Wao wamewafukuza Kina Mdee uanachama Wala hakuna mahali walijadili wang''olewe bungeni.

Kulalamika majukwaani kuliko kutoa sera zao. Trump kila akipa nafasi huwa anawaambia Wamarekani wenzake kama akirudi tena madaraki 2024 atafanya nini tofauti na Biden kwenye kila jambo.
Sio kweli CHADEMA imeshaeleza sana kuwa ikiingia itatekeleza sera ya majimbo/ugatuzi, kuleta katiba mpya Ili kuepusha tozo za ajabu kutungwa na Rais, kufanya PPP kwenye miundombinu n.k Wala hakuna ambacho huwa hawasemi.
 
Wanataka awe anaongea kama Philip Mpango.
 
Benjamini Mkapa alikataa kuitwa MTUKUFU RAIS na akapendekeza aitwe MHESHIMIWA RAIS au NDUGU MKAPA.
 
Mkuu kuongoza nchi kunahitaji vitu vingi zaidi ya uzalendo,
Nyerere alikuwa mzalendo ila aliharibu hii nchi,
Inahitaji kumchek mtu mwenye kuliunganisha taifa, kuunganisha taifa, kuwa na busara, na kuwa na sera nzuri hususanu wakati huu ambapo tunahitaji zidi kujikomboa kiuchumi tunahitaji kiongozi mwenye sera nzuri za uchumi,
Bahati mbaya kwa Lissu sijawahi sikia akiongelea uchumi, yeye yupo more political based
 
Kumbuka kuwa Tanzania tulitawaliwa na Waarabu na walituletea shanga na mavazi,kwa hiyo kufafananisha maendeleo ya Tanzania na Waarabu ni ukosefu wa fikra na uzalendo kwa Watanzania wengi.
 
hana sifa, aache kwanza agenda zake za siri, vile vile hatuwezi kua na Rais ambaye ni mgonjwa...sisi wenyewe wagonjwa tutaongozwaje na mgonjwa mwenzetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…