Huu ndio ubaya wa kukariri maneno na kwa Watanzania walio wengi, hili ni tatizo kubwa miongoni mwao.
FUSO, unaweza kutaja tofauti kati ya mwanasiasa na mwanaharakati ni zipi hasa?
Je una maana mwanasiasa hatakiwi kuwa mwanaharakati au mwanaharakati hatakiwi kuwa mwanasiasa? Je uanaharakati huanzia wapi na uanasiasa huanzia wapi na kuishia wapi
Nashauri tujizuie kutumia hovyo maneno haya mawili. Uanaharakati ni dude kubwa sana linalohusisha makundi mengi uanasiasa ukiwa ni sehemu ndogo tu mojawapo katika hayo makundi.
Katika siasa tunamhitaji mwanaharakati mbobezi atakayeonesha na kusimamia kwa tabia, maneno na matendo anayoyapigania katika kuboresha maisha ya wananchi anaowaongoza.
Hi ndiyo sababu tunapomchagua kiongozi wa juu katika jamii tunataka kujua historia yake, weledi wake, hoja zake na ujasiri wake katika kutetea na kulinda utawala wa haki na sheria..
Kwa Watanzania tulipofikia kwa unafiki wetu kunatia huruma na tunamtaka mtu jasiri aliye tayari kuita dhulma, rushwa na uongo unaoendelea katika jamii kwa jina lake, UOVU!