Ni hatari sana wananchi kuanza kusifia rushwa, yaani MLA rushwa anaheshimiwa zaidi ya asiyekuwa rushwa!
Hii inapelekea kuua taifa, na wananchi wanakuwa wapumbavu, inakuwa bora wangezaliwa mbuzi au nguruwe tu, kuliko kuwa binadamu usiyejitambua!
Inawezekanaje, askari aliyepata div.4 ya 28, akawekwa barabarani kusimamia Sheria, akavimbisha tumbo kwa rushwa, eti anaheshimiwa na jamii, kuliko Mwalimu aliyefaulu Kwa div.2, na akaenda mpaka chuo kikuu, maxima digrii yake ya elimu, na kufaulu kwa upper second award, halafu jamii hiyo hiyo anayoitumikia inamdharau! Eti sababu kazi yake Haina mianya ya rushwa [emoji848][emoji848][emoji848] (hivi hawa nao wanaodharau taaluma ya walimu ni binadamu kamili?)
Halafu wakati huo huo wanawahimiza watoto wao kufundishwa na walimu hao hao, Sasa kwanini Kila mtu mwenye kudharau walimu asifundishe watoto wake nyumbani kwake?
Taifa linaendekeza rushwa kiasi kwamba wasiokuwa na nafasi za kuikoboa rushwa wanaonekana dhaifu, na wanaoikoboa rushwa ndo wanaonekana mashujaa, nchi yangu, nchi yangu, nchi yangu!