Je, Ualimu ni daraja la mwisho kwa utumishi?

Je, Ualimu ni daraja la mwisho kwa utumishi?

Kwann nguvu kubwa inatumuka kuwadharau walimu !?? Tatizo ni Nini hasa!? Kwan wenyewe wameridhika na Hali zao !!! Kipi kina wakera watu mpaka kujadili maslahi ya walimu!? Pili pili uso ila yakuwashia nn!? Hee!! Walimuuu walimu Kwan kama mtu huna Cha kupost mbona hukai kimya kama wengine!??kweli "simple mind people discuss people"
Pole sana mwalimu kwa kuguswa. Mtoa mada hana nia mbaya bali anataka tu kufahamu, from the general public, kwanini hata serikali inawadharau walimu kwa kiasi kikubwa. Shida ni nini? Hiki ndicho anatchotaka kufahamu mkuu.
 
We unaongea tu, umeshajaribu kazi za ualimu? Jifunze hata kwa wenzio, huo muda anautoa wapi. Kuna shule kwa siku anatakiwa afundishe vipindi 9, jioni kuna kusahihisha kazi za wanafunzi, kuna kuandaa andalio la masomo ya siku inayofuata bado kazi za nyumbani kwake. Acheni tu hakuna watu wanafanya kazi kama walimu.
Soma hiyo aya ya mwisho .. nimeandika huenda kuna kitu tusichojua na wao huwa wanapitia.

Ila hizo kazi ulizosema hapo sio zote hufanywa na kila mwalimu.
 
Habari ndugu. Umesema vema kuwa watumishi wengi hawapendi kufanya biashara kwa kuwa ni waoga ku-take risk. Changamoto hapa inaweza kuwa muda ku-manage hiyo biashara wewe mwenyewe kwa asilimia kubwa. Kwa suala la walimu (mimi ni ticha) uzoefu ni kuwa walimu wengi hawajatoka ktk familia zenye nguvu kubwa kiuchumi, hivyo wengi hujikuta mara tu waingiapo kazini huanza kusaidia familia watokazo(kusomesha waliobaki) hali ambayo huanza kuwasumbua mapema sana ktk ajira yao.
Umri wa walimu wengi kuingia kwenye ajira ni mdogo (social age) mwalimu anatoka form 4 or 6, chuo then kazini anakuwa hajafunguka sana namna gani dunia (ya kibiashara) inaenda. Hali hii hutufanya tukiingia kazini tu, tunajua kifuatacho ni nyumba au gari (kumbuka background ya familia yake) na hapa wengi huingia kukopa ili kujenga (nyumba hula pesa na si kuzaa pesa) hali hugeuka kuwa ngumu kiuchumi.
Suala lingine ni kazi ya ualimu haimpi mtu new exposure outside there. Anakutana na mtoto maisha yake yote ya kazi hali inayofanya wengi (sio wote) kutokuwa wabunifu nje ya ualimu. Pia mazingira ya kazi yake humfanya mwalimu muda mwingi wa utumishi wake kuwa wa manung'uniko zaidi (roho ya chuki hujijenga taratibu na kumfanya mtu wa kuigopa tu), mwalimu anamlumu kila afisa wake; halipwi nauli kwa wakati, halipwi uhamisho kwa wakati, akihamishwa ni figisu, hana posho yoyote, hata akifanya overtime anaambiwa awe mzalendo nk nk nk.
Wengi husema walimu wana muda mzuri wa kufanya mambo mengine nje ya ualimu (hili jambo mkijua kuwa nchi hii imebahatika kupata viongozi wakuu kutoka ualimu lakini hawakuweza katu kuyageuza maisha ya waalimu wenzao, mtaelewa kuwa adui mkubwa wa ticha ni ticha) lakini ukweli ni kuwa ili utumishi wako waualimu uwe ktk changamoto basi uwe bize na mambo yako, utaonekana mkorofi, kupewa vikazi vya kusimamia mitihani, kwenda sijui marking utakusikia tu (na shughuli hizi walimu huona ndio bonus zao).
Mwisho, maisha ni malengo na kusimamia malengo. Wapo walimu wana uchumi mzuri kutokana na utumishi wao kwani suala la kuthubutu ni la mtu binafsi japo walimu wengi baada ya 40yrs ndio akili ni kama zinaanza kukaa sawa. TUSAIDIENI MSITUBEZE.
Aisee jamaa umeongea from expirience kabisa.
Chuo then ajira ni janga, kukutana na watu walewale kazini wenye mlengo uleule si ajabu nyote mnakaa eneo hilohilo, wateja wenu ni wanafunzi wanaopokea materials kutoka kwenu huku ninyi msipate chakula ya akili toka kwao.
 
Pole sana mwalimu kwa kuguswa. Mtoa mada hana nia mbaya bali anataka tu kufahamu, from the general public, kwanini hata serikali inawadharau walimu kwa kiasi kikubwa. Shida ni nini? Hiki ndicho anatchotaka kufahamu mkuu.
Huyo ni teacher asikuumize kichwa
 
Usipo iba wewe mwenzako ataiba
Ndiyo watu wanaiba, lakini kinachosikitisha zaidi ni pale ambapo jamii inawadhihaki wasioiba na kuwasifia wanaoiba, hii jamii ya aina gani????
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Habari ndugu. Umesema vema kuwa watumishi wengi hawapendi kufanya biashara kwa kuwa ni waoga ku-take risk. Changamoto hapa inaweza kuwa muda ku-manage hiyo biashara wewe mwenyewe kwa asilimia kubwa. Kwa suala la walimu (mimi ni ticha) uzoefu ni kuwa walimu wengi hawajatoka ktk familia zenye nguvu kubwa kiuchumi, hivyo wengi hujikuta mara tu waingiapo kazini huanza kusaidia familia watokazo(kusomesha waliobaki) hali ambayo huanza kuwasumbua mapema sana ktk ajira yao.
Umri wa walimu wengi kuingia kwenye ajira ni mdogo (social age) mwalimu anatoka form 4 or 6, chuo then kazini anakuwa hajafunguka sana namna gani dunia (ya kibiashara) inaenda. Hali hii hutufanya tukiingia kazini tu, tunajua kifuatacho ni nyumba au gari (kumbuka background ya familia yake) na hapa wengi huingia kukopa ili kujenga (nyumba hula pesa na si kuzaa pesa) hali hugeuka kuwa ngumu kiuchumi.
Suala lingine ni kazi ya ualimu haimpi mtu new exposure outside there. Anakutana na mtoto maisha yake yote ya kazi hali inayofanya wengi (sio wote) kutokuwa wabunifu nje ya ualimu. Pia mazingira ya kazi yake humfanya mwalimu muda mwingi wa utumishi wake kuwa wa manung'uniko zaidi (roho ya chuki hujijenga taratibu na kumfanya mtu wa kuigopa tu), mwalimu anamlumu kila afisa wake; halipwi nauli kwa wakati, halipwi uhamisho kwa wakati, akihamishwa ni figisu, hana posho yoyote, hata akifanya overtime anaambiwa awe mzalendo nk nk nk.
Wengi husema walimu wana muda mzuri wa kufanya mambo mengine nje ya ualimu (hili jambo mkijua kuwa nchi hii imebahatika kupata viongozi wakuu kutoka ualimu lakini hawakuweza katu kuyageuza maisha ya waalimu wenzao, mtaelewa kuwa adui mkubwa wa ticha ni ticha) lakini ukweli ni kuwa ili utumishi wako waualimu uwe ktk changamoto basi uwe bize na mambo yako, utaonekana mkorofi, kupewa vikazi vya kusimamia mitihani, kwenda sijui marking utakusikia tu (na shughuli hizi walimu huona ndio bonus zao).
Mwisho, maisha ni malengo na kusimamia malengo. Wapo walimu wana uchumi mzuri kutokana na utumishi wao kwani suala la kuthubutu ni la mtu binafsi japo walimu wengi baada ya 40yrs ndio akili ni kama zinaanza kukaa sawa. TUSAIDIENI MSITUBEZE.
Hongera mkuu. Umefafanua vizuri kabisa. Hili la kuwaza kukopa na kununua gari ama kujenga siyo kwa walimu tu..nadhani ni asilimia 95 ya watumishi wa kada zote. Na sababu nyingi umeziainisha hapo.
 
Mi mbona kazi ya kujenga nilifundishwa na mtu ambaye hajasoma?
Na si mimi tu katufundisha wengi tu so ye ndo mwalimu wetu.
Kwahiyo kufundish a,e,I,o,u inawezekana hata usipoingia darasani!?
 
Kwa hiyo na hawa daraja la tatu A walipata Division 1 au 2.

Hata hao waliofika shahada ya kwanza wakiwa chuoni kwao ni bora liende tu, maana hata ukipata gentlemen degree wanaajiriwa.

Hii ni semi professional until ianzishiwe body yake na kumaliza astashahada, stashahada, shahada, uzamilo na uzamivu
Kwa hiyo course gani hawapati hizo gentlemen grades?
Mbona argument Yako dhaifu sana mkuu, ukisema grade A, anatofauti gani ya ufaulu na qnayekwenda kusomea cheti kwenye kada zingine?
Nasikia kwa sasa form four ili kwenda kusomea ualimu grade A anapaswa kuwa na angalau div 3, huko kwingine wanaenda wakiwa na angalau D tatu, ambayo ni kama four ya 30, Sasa fact ya kumwita mwalimu kilaza au kuwa ndiyo asiye na uwezo darasani inatoka wapi?
Je, jamii yetu inahusianisha rushwa na akili? (Kwamba anayekali ofisi ya umma na kula rushwando mwenye akili kuliko Mwalimu aliyakalia ofisi ya umma akafaulu lakini hajihusishi na rushwa basi Hana akili?)

Watanzania wamenishinda....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Wakati huko duniani ualimu ni miongoni mwa noble professions (hata kama hawalipwi pesa nyingi) lakini Afrika eti ualimu ni laana, na bado mnategemea kuna wakati hizi nchi zitapiga hatua kimaendeleo?
Najaribu kufikiria kwa mentality kama ya Mpwayungu, akipata dhamana ya kuwa waziri wa elimu, si atakuwa anatemea mate walimu huyuuu...
 
Nchi hii kazi isiyo na nafasi ya kula rushwa inadharauliwa sana,isitoshe uandaaji wa walimu inasemekana ni wale waliofeli hii dhana imekuwepo Siku nyingi,bila kusahau Kuna kada ya upolisi na wanajeshi,polis wakiwa doria usiku hatukosi laki ukiwa mjini,wanajeshi wa posho na MSHAHARA.Hao walimu wanajipewa kazi ngumungumu lkn malipo kidogo na wanarudhika.Wenyewe wameridhika,halafu wewe unawachokonoa.
 
Kazi ya ualimu ni mzuri shida ni kungoja salary tu mwisho wa mwezi akuna allowance yoyote madaraja kwa manati basi shida tupu
 
Back
Top Bottom