Mimi ni ticha. Ktk jamii inayoamua mambo bila ya tafiti za kuaminika (hasa afrika) ni vigumu sana kuona athari (hasi au chanya) juu ya mwalimu. Hapa Tanzania kila mwaka huwa inatangazwa ufaulu umeongezeka(wa mitihani tu) lakini upande mwingine ambao mwalimu hapimwi kwa matokeo ya mtihani wa mtoto (ambao ni hatari sana ukipuuzwa) hakuna anayejali.NI kwa nchi zetu hizi za kimaskini zilizojaa rushwa na watu wenye akili km mleta mada. Nenda kwa wenzetu walioendelea hasa wazungu halafu urudi hapa jukwaani uandike tena kuhusu kada hii barikiwa ya ualimu. Walimu wanatimiza makusudi ya Mungu kuwapatia elimu wanadamu. Maandiko yasema "mtafute sana elimu angalia usimwache akaenda zake" Mi nawaheshimu sana walimu halafu nawapenda sana watoto wadogo ikiwa pamoja na kuwafundisha, na nyie mliolaaniwa kila mara walimu wanadharaulika, mmelaaniwa.
Kwa mfano; unaniletea mtoto ninakaa nae miaka 2+7+4+2 then kila nikimtazama naona kitaaluma haendi popote (KWA SAUTI KUBWA, HAENDI POPOTE) ila namuona ni mwana jamii mzuri sana (dereva, mfanya biashara, mama au baba bora, mchungaji au imamu mzuri nk nk nk)hivi huwa mnajiuliza kitu gani mimi kama mwalimu nawekeza aweze kuwa hivyo? Utanipima kwa lipi ktk haya? Serikali inanipimaje hapa? (Extra curriculum?)
Jamii zote zinazofanya tafiti na kuamua kwa tafiti ndizo huona mwalimu ni FUTURE hivyo huakikisha saikolojia yake ipo chanya kwa muda mwingi kwani wanatambua generation ipo mikononi mwake. Sisi huku future ipo kwa wanasiasa ( yamejengwa mavyumba sijui mangapi vile na kujisifu kidato cha kwanza wote kwa mara ya kwanza wameanza pamoja!) Ila nani anauliza HAO KIDATO CHA KWANZA WOTE WAMEANZA KUSOMA PAMOJA? Lakini mimi ticha nipo nao tu na roho inauma juu ya jamii yangu hii ( wameejirundika wanakaa chini nk) lkn kuna kitu wapata (toka kwenye roho ya mwalimu) ila mwanasiasa anayejilipa vizuri yeye anawatangazia amewaletea shule (shule au kituo cha kukusanya watoto!)
Ugumu wa maisha ya mwalimu ni wakutengenezwa pia ili asiwe huru sana(free thinker) maana hawezi kudhibitika na tabaka tawala. Kujua hili ndio maana hata wakuu wa shule wao wanapewa daraja jingine (mwajili/madaraka allowance) sababu tu kumfanya mwalimu awe muoga toka chini kabisa mwisho naye huleta jamii ya waoga tu.
WASALAAM.