Je, Ualimu ni daraja la mwisho kwa utumishi?

Pole sana mwalimu kwa kuguswa. Mtoa mada hana nia mbaya bali anataka tu kufahamu, from the general public, kwanini hata serikali inawadharau walimu kwa kiasi kikubwa. Shida ni nini? Hiki ndicho anatchotaka kufahamu mkuu.
 
Soma hiyo aya ya mwisho .. nimeandika huenda kuna kitu tusichojua na wao huwa wanapitia.

Ila hizo kazi ulizosema hapo sio zote hufanywa na kila mwalimu.
 
Aisee jamaa umeongea from expirience kabisa.
Chuo then ajira ni janga, kukutana na watu walewale kazini wenye mlengo uleule si ajabu nyote mnakaa eneo hilohilo, wateja wenu ni wanafunzi wanaopokea materials kutoka kwenu huku ninyi msipate chakula ya akili toka kwao.
 
Pole sana mwalimu kwa kuguswa. Mtoa mada hana nia mbaya bali anataka tu kufahamu, from the general public, kwanini hata serikali inawadharau walimu kwa kiasi kikubwa. Shida ni nini? Hiki ndicho anatchotaka kufahamu mkuu.
Huyo ni teacher asikuumize kichwa
 
Usipo iba wewe mwenzako ataiba
Ndiyo watu wanaiba, lakini kinachosikitisha zaidi ni pale ambapo jamii inawadhihaki wasioiba na kuwasifia wanaoiba, hii jamii ya aina gani????
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Hongera mkuu. Umefafanua vizuri kabisa. Hili la kuwaza kukopa na kununua gari ama kujenga siyo kwa walimu tu..nadhani ni asilimia 95 ya watumishi wa kada zote. Na sababu nyingi umeziainisha hapo.
 
Mi mbona kazi ya kujenga nilifundishwa na mtu ambaye hajasoma?
Na si mimi tu katufundisha wengi tu so ye ndo mwalimu wetu.
Kwahiyo kufundish a,e,I,o,u inawezekana hata usipoingia darasani!?
 
Kwa hiyo course gani hawapati hizo gentlemen grades?
Mbona argument Yako dhaifu sana mkuu, ukisema grade A, anatofauti gani ya ufaulu na qnayekwenda kusomea cheti kwenye kada zingine?
Nasikia kwa sasa form four ili kwenda kusomea ualimu grade A anapaswa kuwa na angalau div 3, huko kwingine wanaenda wakiwa na angalau D tatu, ambayo ni kama four ya 30, Sasa fact ya kumwita mwalimu kilaza au kuwa ndiyo asiye na uwezo darasani inatoka wapi?
Je, jamii yetu inahusianisha rushwa na akili? (Kwamba anayekali ofisi ya umma na kula rushwando mwenye akili kuliko Mwalimu aliyakalia ofisi ya umma akafaulu lakini hajihusishi na rushwa basi Hana akili?)

Watanzania wamenishinda....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Wakati huko duniani ualimu ni miongoni mwa noble professions (hata kama hawalipwi pesa nyingi) lakini Afrika eti ualimu ni laana, na bado mnategemea kuna wakati hizi nchi zitapiga hatua kimaendeleo?
Najaribu kufikiria kwa mentality kama ya Mpwayungu, akipata dhamana ya kuwa waziri wa elimu, si atakuwa anatemea mate walimu huyuuu...
 
Nchi hii kazi isiyo na nafasi ya kula rushwa inadharauliwa sana,isitoshe uandaaji wa walimu inasemekana ni wale waliofeli hii dhana imekuwepo Siku nyingi,bila kusahau Kuna kada ya upolisi na wanajeshi,polis wakiwa doria usiku hatukosi laki ukiwa mjini,wanajeshi wa posho na MSHAHARA.Hao walimu wanajipewa kazi ngumungumu lkn malipo kidogo na wanarudhika.Wenyewe wameridhika,halafu wewe unawachokonoa.
 
Kazi ya ualimu ni mzuri shida ni kungoja salary tu mwisho wa mwezi akuna allowance yoyote madaraja kwa manati basi shida tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…