Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?


Huu ni utopolo.
 
Kaka mali ya duniani yote ni ya shetani, huu ni ukweli mchungu.
Hao mabilionea lazima uingie makubaliano na shetani au Mungu ili uwe bilionea.
Kwamba ile top ten ya dunia yotee ina makubaliano?

#YNWA
 


Umesema "umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani" kwanini asikupe tu hadi umuombe?

Huyo Mungu wenu anazidiwa nguvu na shetani? Sasa mnamuabudu wa nini?

Huu ulioandika ni utopolo na kwa akili hizi inabidi muanze kulipia tozo uzwazwa wenu.
 
Soma Mathayo 4 : 8-10
Shetani alimwambia Yesu ukinisujudu nitakupa Mali zote hizi, Hapa shetani anajigamba mbele za Yesu Mali zote za hapa duniani ni zake.
Uliona Yesu akimbishia, zaidi ya kukataa kumsujudia?
Ongeza maarifa kijana
 
Kweli aisee.
Nakumbuka nilipofungua Duka siku za nyuma kuna Dawa nilipewa na Shangazi yangu toka Tabora. Alisema nikiichimbia nje kwenye kona zote za Duka langu, hakuna mwizi atakaeiba kitu na hata akiiba nitamkuta hapohapo mlangoni akiwa amebeba hichokitu alichoiba, Ila akikiacha kitu cha wizi ndio anaweza kutoka.

Sasa nilikuja kuiamini ile dawa, kuna siku wezi walivunja milango na kuiba vitu kwenye eneo lile ila kwenye Duka langu nilikuta milango imevunjwa ila hakuna kitu kilichoibwa. Majirani zangu wote waliibiwa vitu.
 
Kuna viashiria vilivyo wazi ambavyo huwezi jiuliza mara mbili kuwa flani utajiri wake ni wa nguvu za giza. Ila usisahau pia kuna walio na ratiba zao juu siku flani kutofanya kazi; kwa mfano usishangae msabato kutofungua biashara zake Jumamosi au mkristo flani kutofungua J'pili au kwa muislamu siku ya ijumaa.
Kwa mwenye utajiri wa kichawi lazima kutakuwa na la ziada tu
 
Mburura hawaishagi ndg yng, Mara Mungu Mara shetani... Wapi na wapi?
Kwa nini Mungu asitoe utajiri tu mpk masharti kibao?
 
Unachopaswa kujua tu ni kwamba inapoishia sayansi ndio uchawi unaanzia hapo kwenda mbele.
Hata huo uchawi ni sayansi sema code of universe pia tunaziita pia uchawi, mfano hata kutumia maji ya baraka au mtu achukue chumvi au mawe ya mvua aogee ataambiwa uchawi, mchawi ni mtu anayedhuru wengine iwe kwa kupata Mali au kujifurahisha huyo mtu hatakiwi kuishi anatakiwa kuuwa ila sayansi ya code of universe siyo uchawi.
 
Niliwahi soma mahali kwenye kitabu kitakatifu, panasema '" vyote viijazavyo nchi ni mali ya Bwana"', sasa huyu shetani anaingiaje tena?
 
Kama nakusoma iviii
 
Kwenye biashara sijui Ila kwenye ndoa nakuhakikishia LIMBWATA lipo.
Ukila nyama iliyowekwa maskani kwa masaa kadhaa lazima uwehuke tu....
 
Niliwahi soma mahali kwenye kitabu kitakatifu, panasema '" vyote viijazavyo nchi ni mali ya Bwana"', sasa huyu shetani anaingiaje tena?
The universe has its own code,issue za shetani na Mungu ni man made kwa ajiri ya civilization code.na Siku civilization code imefunguka ndio utakuwa mwishi hii dunia maana haitatawalika tena.
 
k

kabla hujaomba Mungu alikua hajui

kuamini imani za kijinga za kishirikina ndio kujua vitu vingi,sumbawanga kuna matajiri wangapi
Huko sikunasifika kwa uchawi, na wachawi hawatakiwi kuishi maana wanachawia wenzao wasifanikiwe kwa chochote.
 
Kupambana na shetani ili umnyang'anye utajiri wake ni sawa na kulazimisha ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Jibu lipo pale shetani alipompandisha Yesu mlimani na kumuonyesha utajiri wa dunia, enyi binadamu, mnahangaika nini?? Basi mtumikie shetani upate utajiri , "Amen".
 
""Africa tuko kwenye rank za juu kabisa katika mabara yenye imani za kishirikina, lakini hatujaweza kutoa hata mchawi mmoja kwenye top 10 ya mabilionea""

Mchawi ni nani? hao wachawi hua unawatambua? Kwamba maisha yao kiuchumi yapoje..?
Mchawi ni mchawia wenzake hatakiwi kuishi hata kama ni mama au baba yako atakuchawia usiendelee kwa uchawi wake.
 
Code of universe inatofauti gn na Uchawi?
Naomba elezea mechanism of action Yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…