Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Kwahio unataka waganga wote wawe mabilionea, unawalazimisha waishi maisha unayotaka wewe wayaishi, sio kila mtu ata prove ujinga unaofikiria maishani. Kwa sababu mimi nina mabasi 100 unataka nitembelee v8 au range rover ili uamini kwamba mimi ni tajiri, nikitembelea eskudo au rav 4 au hata passo, kwani sitafika nakotaka kufika ?! Baadhi ya watanzania tuache kua na akili za kipumbavu namna hii!
Duh! Akili zako Bana. Kwa hiyo Kuna matajiri wanaamua kuishi kimasikini? Acheni Utapeli, uganga ni upuuzi
 
Kwahio unataka waganga wote wawe mabilionea, unawalazimisha waishi maisha unayotaka wewe wayaishi, sio kila mtu ata prove ujinga unaofikiria maishani. Kwa sababu mimi nina mabasi 100 unataka nitembelee v8 au range rover ili uamini kwamba mimi ni tajiri, nikitembelea eskudo au rav 4 au hata passo, kwani sitafika nakotaka kufika ?! Baadhi ya watanzania tuache kua na akili za kipumbavu namna hii!
Duh! Akili zako Bana. Kwa hiyo Kuna matajiri wanaamua kuishi kimasikini? Acheni Utapeli, uganga ni upuuzi
 
Kwaio kwa tajiri kutembelea passo ni kuishi kimaskini? Sasa sikiliza nikuambie dogo, kama ambavyo mnaona uganga ni upuuzi, hivyo hivyo na mnavyoviona sawa ni upuuzi vile vile, mbona hatusemi makanisani huko wengine hua ibada zenu mnaendesha kwa kutemeana mate? Mbona hao akina mwamposa wenu na akina gwajima tunaaambiwa wanawapa waumin utajiri, mbona wao hawapo forbes,
Narudia kusema kama mganga au muumin wa dini ya nguvu za giza, au tajiri, nina miongozo ninayoisimamia, sihitaji ku proove kwamba nina hela ama sina hela kwenu wenye akili zilizojaa maji( water) , ni upumbavu ( foolishness) kutaka wengine waishi maisha nayotaka waishi sababu wana hela au wamepatia utajiri kwenye imani wanayoiamini..
Kwanza mie sipo kwa hizo Imani za kigeni unazozitaja, pia si muumini wa ulimwengu wako wa giza. Halafu cjasema waganga wanatembelea passo. Wapo wanaotembelea hata V8 but mostly pesa zao ni za kuwatapeli kwa uongo wagonjwa just kama wanavyofanya kina Gwajima, Mwingira na makorokoro kama hayo!

So kama upo kwenye ulimwengu wa giza prove here Uchawi unasaidiaje biashara kukua...
 
Hakuna Agent anayekubali kuneemesha wenzie huku hali yake ikiwa pangu pa kavu.
We bisha wakati wenzako wanachukua ndago kwa hao hao maagent na kutajirika kwa nguvu za giza. Sikuhamasishi nawe ujaribu bali najaribu kukuaminisha kuwa kuna utajiri wa upande wa nguvu za Mungu na utajiri wa upande wa shetani. Ishi miaka mingi, jichanganye ujue kijana
 
We bisha wakati wenzako wanachukua ndago kwa hao hao maagent na kutajirika kwa nguvu za giza. Sikuhamasishi nawe ujaribu bali najaribu kukuaminisha kuwa kuna utajiri wa upande wa nguvu za Mungu na utajiri wa upande wa shetani. Ishi miaka mingi, jichanganye ujue kijana
Wengi wanaopinga ndio wako upande huo, kwa utajiri au kwa vyeo. Na wanapinga ili wasijulikane
 
Kwa mdomo huu mchafu hata mimi mtu kama wewe ukikaa vibaya nakutoa kafara tu! Watu wa mdomo kama wako hamfai kuishi duniani.
Kaanze kumtoa kafara mama yako anayekushauri upumbafu. Jitu zima ukipata matatizo unakimbilia kwa mama, mama mwenyewe mchawi. Pipa limepata funiko.wajinga kama wewe mnatakiwa mfe vifo vya ajabu pathetic.
 
Wengi wanaopinga ndio wako upande huo, kwa utajiri au kwa vyeo. Na wanapinga ili wasijulikane
Wengi wao hujulikana kwa masharti wanayopewa yakiwa dhahiri mbele ya jamii. Kwa mfano unakuta jamaa ni tajiri vibaya mno akimiliki vitega uchumi kibao na magari yakutosha, lakini anatembea kwa mguu na ndala miguuni.! Au unakuta mzee flani ni don haswa ila ana kidonda kikubwa eneo fulani mwilini mwake alafu hakiponi. Won't you use your common sense to relate his richnness na hali yake?
 
Ukiona mtu amepita na chuma kipya utafikiri kimetoka kiwandani leo, Jiulize
Ukiona kwa siku mtu anauza milioni 100, 200 n.k jiulize
Ukiona mtu tajiri anavaa rafu rafu, jiulize
Ukiona mtu tajiri, biashara zake zinakuwa na misimamo, mara siku x au muda x sifungui,jiulize
Ukiona tajiri anafanya sherehe sherehe za kuchinja wanyama nyakati fulani, jiulize
Ukiona tajiri ana watoto wachache, jiulize n.k
Ukiona tajiri anatumia pua kupumua jiulize
 
Wiki iliyopita nilitoka Moshi nikaenda kumtembelea classmate wangu pale Arusha. Jamaa ni engineer wa computer. Jumapili baada ya kula Ibada Safi na kwaya kali pale St. Theresa tuli-mount XR 250 na tukaenda kufunga Camera za usalama kwa nyumba mpya ya Tajiri mmoja wa Kanda ya Ziwa. Huyu mjuba kajenga mjumba wa kuishi wa ghorofa mbili. Pale kwake pazuri asee, kama Ikulu ati.

Basi tukiwa tunakomaa na kazi (mie sio mtaalam but nilikua Nampa kampani msela) jamaa alikuja na Range lake kutuletea Vifaa kadhaa. Baada ya kukabidhi alisepa. Basi jamaa yangu akawa ananiongelesha kwa kispanish chetu cha kuunga unga na solotepu. Akanambia huyu mjuba ni mchawi balaa. Pale kwake tulikuta watoto wawili wa kiume mandondocha wanatematema udenda tu. Jamaa akanambia ni watoto wake wa kuzaa kabisa na ndo wanalinda business zake. Yes, jamaa Ana biashara kubwa ya Hardware na electronics. Nasikia pia Ana Real estate bila kuhesabu biashara nyingine huko kwao! Pale tu nilihesabu magari 4 makali bila kuhesabu maroli ya biashara. Alikua na chale Kadhaa usoni na mikononi. Inasemekana biashara zake kazizindika kwa makafara balaa!

Sasa tujiulize, je, Uchawi una nafasi gani katika kukuza Biashara? Kuna ukweli wowote katika kuinua biashara?

Je, kwa nini tusiusome ktk masomo ya vyuoni kwa maendeleo ya umma?
Nachojua kuna mahusiano makubwa sana kati ya mafanikio ya kibiashara na ushirikina.
Lakini najua pia kuwa kuna mahusiano makubwa mno mno kati ya mafanikio ya kibiashara na ucha Mungu wako.

It is just a matter of trading of vile unavyofikiria wewe inafaa kwa wakati husika. Wengi huweza kuanza vizuri Biashara kwa kuunga unga kidogo kidogo ila once wanapofikiria kukuza na kufika viwango vya juu washauri hugonga hodi na kuwapa option nyingi zikiwepo za kishirikina.

Wakati mwingine changamoto za kibiashara zinaweza kukupelekea kuamua kuingia madude ya ajabu, mf. unaweza kufungua duka na usiuze kitu hata kimoja wiki zima, na kwa hali hiyo ukiambiwa Jiongeze utajikuta umeingia mtego wa kutafuta msaada wa kiganga.

Vema watu wajue kuwa hayo mambo yapo na ni wengi tu wanatumia, sema kuthibitisha inaweza ikawa tabu ila yapo, na bahati mbaya zaidi watumiaji wazuri wa huduma za kiganga, huwa wako vizuri sana na jamii, makanisani ni watoaji wazuri, kwenye jamii wanatoa misaada mikubwa, just to fool people.
 
Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utajiri
Kwanza kuanzia Leo utambue hili, Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwapa utajiri wote wa duniani na fahari zake wazimiliki, lakini walipohasi kwa Mungu kwa kumsikiliza shetani, utajiri wote wa duniani ukawa ni Mali ya shetani, wanadamu hatumiliki tena utajiri wa hapa duniani.
Sasa ili kuwa tajiri una options mbili tu
(1) umuombe shetani akupe sehemu ya utajiri anaomiliki, hii inawezekana kama ukikubaliana na masharti yake, na siku ukienda kinyume anakunyang'anya.
(2) umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani, na hii inawezekana kama utakuwa muombaji sana na mtakatifu haswa, kumyang'anya shetani sehemu ya utajiri wake si rahisi kihivyo.

Usijidanganye kama unaweza kuwa tajiri kwa kufuata seminar za motivation speaker peke yake, utajiri wote anao shetani, ni either uungane naye au upambane kumyang'anya.
Kwahiyo Bakheresa, Dewji ni makafara.

Sasa aliyegundua FB, Amazon anarogea wapi?

Dangote nae kile kiwanda cha Mtwara kinarogea wapi?

#YNWA
 
Mkuu biashara nyingi zimezindikwa na zimepigwa kalilio la kivutia wateja, hakuna biashara mjini zinaenda kwa uzoefu . Mjini kuzito sana , last weekend nilitembelea night club flan hivi chugga nilishangaa nilipoingia mwili ulisisimka sana hata watu niliowakuta hawakuwa wakawaida na cha kushangaza club nzima nilikutana na sura ngeni halafu zinafanana we acha tu. Kipindi nipo mwanza niliwahi kuwa na mwenyeji alinisimulia mambo mengi kuhusu biashara na nguvu za Giza zinavyotumika . Duniani ni mapito tu kila mtu ashinde mechi zake kwa juhudi au kubebwa.Mjini kuzito sana , nenda kwa mfano hapa Arusha , soko kuu, Kilombero au maduka ya stendi ndogo Kama uko vizuri na Kinga za jadi utaona mengi . Wamama wa Kilombero ni nomana hata wale wauza matunda Kilombero .
Tajiri wa Amazon, FB, yaani Ile top ten ya dunia IMEZINDIKA NINI?

Dangote nae uchawi wake ni upi?

#YNWA
 
Kama mnautaka uchawi wa kweli nendeni namanyere karibu na sumbawanga...huombwi hata mia mpaka ishu yako itiki
Acha uongo,wajinga kama nyie mnaharibu sifa ya mkoa wa Rukwa.
Ingekuwa hivyo Rukwa isingekuwa miongoni mwa mikoa maskini kwa kipato.
 
Sizungumzii kwa wengine, ila kwangu binafsi.

Nafanya biashara ya kifedha (za mtandao na benki). Mwaka 2018 nilipigwa tukio na wakulungwa wakaondoka na 28+ Million cash, simu na mashine za benki.

Nilimpigia simu mama yangu kumueleze maswaibu yaliyonipata. Alishangaa sana nimesurvive vipi zaidi ya miaka 5 bila kuzindika eneo langu la biashara.

Akanitaka niende nyumbani kwa mwitikio wa haraka. Baada ya kuandika maelezo polisi, jioni nikazama nyumbani.

Akanipeleka kwa mzee mmoja. Wala siyo mchawi, ila ni mtaalamu wa kuzindika.

Kuzindika siyo uchawi. Nikampeleka mjini. Akafanya yake akarudi.

Nimeshakosa majaribio matatu ya kuvamiwa.

Na ripoti zote nazipata kutoka polisi. Wakivamia na kukamatwa, wakihojiwa wanasema walipanga kuja kuniibia. Ila mikakati yao inafeli.

Zindiko ni muhimu sana.
Pia mkuu huwezi kununua gari usilizindike, dunia nzito sana hii linaweza likadumu muda mfupi sana barabarani. Kuna watu wanabisha mambo haya makusudi ili Wengine wafunguke tu kuhusu haya mambo
 
Tajiri wa Amazon, FB, yaani Ile top ten ya dunia IMEZINDIKA NINI?

Dangote nae uchawi wake ni upi?

#YNWA
Kaka mali ya duniani yote ni ya shetani, huu ni ukweli mchungu.
Hao mabilionea lazima uingie makubaliano na shetani au Mungu ili uwe bilionea.
 
Kaka mimi nina practice ujasiriamali, ninaweza kuwa vijana wachache wenye CPA lakini nikaamua kuwa mjasiriamali na kujikita kkoo, na sikuwahi kutaka kwenda kwa mganga, niliangaika sana karibu miaka sita napanda, nashuka, maisha hayasogei.
Nilikuja kuanza kuona mafanikio baada ya kukubali kuwa mtakatifu kweli, mimi lazima niwe na maombi asubuhi nusu saa, usiku nusu saa.
Biashara zangu hazigusiki na hili shetani analijua.
Mimi kabla ya kufungua duka, lazima niwe na siku 30 za maombi ya kufunga ndio nianze biashara mpya, bila kufanya hivyo najua hiyo biashara haitasimama.
Kila mwaka mwanzoni kabisa lazima nifunge siku 30 kuikabidhi biashara kwa Mungu. Hapo sijakuambia kwa habari ya sadaka.
Kama hizi sheria huziwezi usije kariakoo, otherwise nenda kwa waganga.
Sasa wewe njoo na maarifa yako bila nguvu ya kiroho kama hujafirisika mpaka Ukose hela ya nauli
Nahtaji niongee na wewe hats dk moja tu kaka nifanyeje

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom