Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Sizungumzii kwa wengine, ila kwangu binafsi.

Nafanya biashara ya kifedha (za mtandao na benki). Mwaka 2018 nilipigwa tukio na wakulungwa wakaondoka na 28+ Million cash, simu na mashine za benki.

Nilimpigia simu mama yangu kumueleze maswaibu yaliyonipata. Alishangaa sana nimesurvive vipi zaidi ya miaka 5 bila kuzindika eneo langu la biashara.

Akanitaka niende nyumbani kwa mwitikio wa haraka. Baada ya kuandika maelezo polisi, jioni nikazama nyumbani.

Akanipeleka kwa mzee mmoja. Wala siyo mchawi, ila ni mtaalamu wa kuzindika.

Kuzindika siyo uchawi. Nikampeleka mjini. Akafanya yake akarudi.

Nimeshakosa majaribio matatu ya kuvamiwa.

Na ripoti zote nazipata kutoka polisi. Wakivamia na kukamatwa, wakihojiwa wanasema walipanga kuja kuniibia. Ila mikakati yao inafeli.

Zindiko ni muhimu sana.
Mkuu ingekua mambo yanaenda smoothly kama hivyo basi tungetegemea kuona biashara za makufuli na security tools kama CCTV camera zinakufa

Nani mwenye mali ambaye haitaji kuzilinda zisiibiwe mpaka atumie gharama kubwa kulipa walinzi wakati ukiwa na zindiko hayo yote huyaitaji?

Kuna sababu nyingi za wewe kutoibiwa mara ya pili bila kuhusisha uchawi

Majambazi waliovunja na kuiba ndio wanajua siri ya duka lako, halafu wezi kuja kuiba kwako mara moja haimaanishi wameweka territory kua next project lazima waje tena hapo kuiba na ikisipotokea wameiba useme ni dawa uliyopewa na mganga ndio imewazuia
 
Sijazungumzia hilo.

Baada ya wiki mbili sehemu ya walioniibia walikamatwa.

Waliwashirikisha boda boda wa eneo la karibu. Alipewa gawio la hela kidogo na maagizo ya kwenda kuitupa simu za miamala.

Bahati nzuri ama mbaya tamaa ikamuingia akaingia mtaani kuziuza. Tracking ikawakamata waliouziwa na kumtaja huyo ndugu.

Waajiri wake, walipigwa risasi baada ya kwenda kuvamia sehemu nyingine.

Sikupata hata mia, lakini simu na mashine zilirudi.
Elezea vizuri walikamatwaje
 
Mkuu ingekua mambo yanaenda smoothly kama hivyo basi tungetegemea kuona biashara za makufuli na security tools kama CCTV camera zinakufa

Nani mwenye mali ambaye haitaji kuzilinda zisiibiwe mpaka atumie gharama kubwa kulipa walinzi wakati ukiwa na zindiko hayo yote huyaitaji?

Kuna sababu nyingi za wewe kutoibiwa mara ya pili bila kuhusisha uchawi

Majambazi waliovunja na kuiba ndio wanajua siri ya duka lako, halafu wezi kuja kuiba kwako mara moja haimaanishi wameweka territory kua next project lazima waje tena hapo kuiba na ikisipotokea wameiba useme ni dawa uliyopewa na mganga ndio imewazuia
Tajiri mwenyewe mwenye mauchawi tulienda kumfungia CCTV wakati Ana Kinga ya waganga[emoji1787][emoji1787]
 
Binafsi nilipomaliza chuo nilikuwa na wasiwasi sana juu ya kazi.Hali hii ilinipelekea kupata mawazo na kukosa amani.Siku moja niliamua nijikite katika maombi. Nilianza kusali asubuhi kabla ya kuamka ,mchana nikipata nafasi baada ya kazi za kawaida na jioni kabla ya kulala.Niliendelea kusali muda kama mwezi mmoja.Lakini pia hapo ikumbukwe natuma cv za kuomba kazi.Siku moja mama aliniambia ameota nipo ofisini na bosi wangu ni mhaya. Haikuchukua muda sana kuna sehemu niliapply wakanipigia simu niripoti kwa ajili ya usaili wa kazi.Nilifunga safari kwenda kuanza usaili bahati nzuri nilipita kwenye usaili na kupewa mkataba.Kwa mshangao pia nilikuta bosi ni mhaya kama mama alivyoniambia.Inawezekana kufanikiwa kupitia sala Mungu yuko juu ya watu na viumbe vyote
 
Code of universe inatofauti gn na Uchawi?
Naomba elezea mechanism of action Yake
Ni tofauti na uchawi, wenzetu wanaziita black magic zipo kwaajili ya kumsaidia mtu personal na kuzifanya unatakiwa ufanye kwa haki isiwe kwaajili ya kumdhuru mtu ila kujilinda na huo uchawi wa wachawi na kujifungulia milango iliyofungwa na hao wachawi na ndo maana wachawi hawatakiwi kuishi Ili wasiendelee kudhuru wengine, Sasa waafrika kwa vile ni weusi wakisoma neno black wakadhani ni weusi wao kumbe ni nguvu za kublock nguvu hasi na ndo mataifa ya weupe wote wanatumia hizo black magic kufanikisha mambo yao na weusi wanatumia uchawi wa kuloga na kudhuru kitu kinachoondoa mafanikio, mfano charcoal black magic zinafanya mengi and so on, Chumvi hivyo hivyo.
 
Tajiri mwenyewe mwenye mauchawi tulienda kumfungia CCTV wakati Ana Kinga ya waganga[emoji1787][emoji1787]
CCTV za kazi gani wakati mizizi inafanya kazi?

Hao ndo wale waganga ambao wanaweka bango kujitangaza afu ukifika ofisini anakuambia anauza dawa ya kuvutia wateja

Yani yeye kashindwa kukuvuta kwa dawa hiyo mpaka akatumia tangazo ambalo kaligharamia kulichapa stationery pamoja na kuweka address na namba ya simu
 
Uchawi ni uongo uongo wa kishamba sana
 
Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utajiri
Kwanza kuanzia Leo utambue hili, Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwapa utajiri wote wa duniani na fahari zake wazimiliki, lakini walipohasi kwa Mungu kwa kumsikiliza shetani, utajiri wote wa duniani ukawa ni Mali ya shetani, wanadamu hatumiliki tena utajiri wa hapa duniani.
Sasa ili kuwa tajiri una options mbili tu
(1) umuombe shetani akupe sehemu ya utajiri anaomiliki, hii inawezekana kama ukikubaliana na masharti yake, na siku ukienda kinyume anakunyang'anya.
(2) umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani, na hii inawezekana kama utakuwa muombaji sana na mtakatifu haswa, kumyang'anya shetani sehemu ya utajiri wake si rahisi kihivyo.

Usijidanganye kama unaweza kuwa tajiri kwa kufuata seminar za motivation speaker peke yake, utajiri wote anao shetani, ni either uungane naye au upambane kumyang'anya.
Umejitahidi kueleza.
 
Nimeishi kigoma, pangani, tanga mjini, sumbawanga, namanyere, lyambamfipa, shinyanga, bariadi huko wanasema kuna mlango wa kuzimu, pemba na mafia kote huko nk nk lakini sijawahi kukwamishwa jambo langu kwa namna yoyote ile ya kichawi labdq figisu tu za kuchongeana kwenye majukumu. Mm siamini katika utajiri ni nguvu za shetani bali naamini utajiri ni katika juhudi na mawazo yetu katika kufanya kazi.
chaguo NI laki kuwa tajiri wa WAGANGA au kuwa tajiri wa juhudi na bidii zako.vyote hivyo utapata utajiri.
Ila utajiri tunaozungumzia hapa sio wa nyumba na IST .ambao unao.
Bali wa magari 300+ ya abiria,semi truck 500+. Nk
 
Hakuna kitu unachomiliki katika hii dunia, wewe ni mpitaji tu, unaakodisha Mali za shetani ukifa unamuachia au umnyang' anye kwa msaada wa Mungu ila ukifa unamuachia Mungu vitu vyake.
Hapa duniani unakuja mtupu unaondoka mtupu.
Hivi unajua hata huu mwili tunaazima tu, ila tukifa tunauacha hapa duniani.
Tukiwa tunapita tunaelekea wapi mkuu
 
Kama MTU anolaga apate Mme kwanini asiroge apate Mali.
Limbwata sio uchawi wa kumtanya mwanamke apate mume, lah hasha. Limbwata anafanyiwa mume awe bwege, asitamani mwanamke mwingine,mshahara wote apewe yeye mwanamme.
Liko aina tofautitofauti kutokana na sehemu tofauti.
Ni kulishwa uchafu tu usiozingumzika hapa.
Kuna mtu aligundua alichokishwa kidogo atapike Hadi maini
Jua tu wanawake sio watu.
 
chaguo NI laki kuwa tajiri wa WAGANGA au kuwa tajiri wa juhudi na bidii zako.vyote hivyo utapata utajiri.
Ila utajiri tunaozungumzia hapa sio wa nyumba na IST .ambao unao.
Bali wa magari 300+ ya abiria,semi truck 500+. Nk
whatever mkuu ni suala la imani tu, kama ya kwako inakutuma kuwa utajir wa magar 300+ ni mpaka utumuie ndumba ni sawa tu mm sina shida na imani za watu.
 
Kwenye maandiko kuna sehemu wanasema wakati mwana wa adamu amezaliwa, kuna nyota ilikuwa inang'aa juu upande wa mashariki; na watu mbalimbali walikuwa wakiifuatilia ile nyota ili waweze kumfikia mtoto aliyezaliwa. Wanachofanya wakulungwa ni kukutengeneza wewe kuwa kama ile nyota, na matokeo yake hela zinakuwa zinakutafuta wewe popote ulipo na si wewe kuzitafuta hizo hela. Kumbuka zile hela zinazokuja kwako kuna sehemu zinakuwa zimepungua, yaani mwingine anapoteza mwingine anapata. Swali la kujiuliza, zinatokajetokaje huko ziliko na kuja kwako?
 
whatever mkuu ni suala la imani tu, kama ya kwako inakutuma kuwa utajir wa magar 300+ ni mpaka utumuie ndumba ni sawa tu mm sina shida na imani za watu.
Hayo magari ya mizigo unayoyaona na mabasi ya abiria unayoyaona kuna 90% wamiliki wake NI matajiri wa WAGANGA.
 
Back
Top Bottom