Ndio maana niliuliza swali rahisi, kwamba je wanawake wote wenye tabia njema wanaolewa na wote wanaoachwa wana tabia mbovu, na je una uhakika walioolewa wote wana tabia njema tuanzie hapo
Tatizo kubwa wadada wengi wanadefinition tofauti kati ya kuolewa/kufunga ndoa na kuanzisha familia au kuishi mwanamme.
Hivi unajua ya kwamba asilimia kubwa ya wadada wanapenda kufunga ndoa au kuolewa yaani ile tukio(event) la kupeleka mahari, kuvaa shera, kwenda kanisani, kufanya sherehe basi kiu yao inakuwa imeishia hapo.
Wadada wengi hawana kiu ya kuishi na mwanamme ndiyo maana hizo events zikiisha asilimia kubwa wanakimbia ndoa zao.
Mwanamke ambaye anatabia mbovu na amefanyiwa events za kuolewa, huyo hawezi kaa na mwanamme, lazima ndoa yake ataivunja muda wowote kwani tabia zake ni mbovu hata kama kaolewa/ kafanyiwa events hawezi ishi na mwanamme.
Ila mwanamke ambaye anatabia njema, afanyiwe au asifanyiwe events za kuolewa huyo lazima ataendelea kuheshimu mahusiano yake na atadumu kuishi na mwanamme.
Siyo kila mwanamme anaweza kuscreen mwanamke mwenye tabia njema, wengi huwa wanaingia mkenge wanaoa mwenye tabia mbovu ambapo huwa wanashindwana kwenye kuishi pamoja na wanaachana.
Wadada wakiacha kuwa trapped kwenye event ya kuolewa/kufunga ndoa, maana hayo maevents yanafanyika sana na hayana maana yoyote katika maisha halisi ya familia. Ila siku wakifocus katika kuanzisha familia na mwanamme, hakuna mdada yeyote aliye serious atakosa mwanamme wa kuishi naye.
N.B mahusiano au ndoa ni ya mwanamke. Mwanammke ndiye anauwezo wa kuanzisha mahusiano au kuyavunja. Fact ni kwamba Zaidi ya 80% ya talaka mahakamani zinaombwa na wanawake.