Tatizo jingine mabinti wa siku hizi wengi wenu, mnamatarajio makubwa ya kiuchumi kupitia ndoa na ndio maana hata standards zenu mnazo set kipindi mkiwa hot zinakuwa sio halisi. Ila jua likizama ndipo unakuja kujua vyote mlivyokuwa mkivitaka ni batili. Mnamahitaji mengi sana ambayo si ya msingi Mf vikoba viwili viwili,mchezo majina matatu,unataka simu kali tena latest,nguo zinazo trend,nyumba kali,usafiri nk wakati shughuli ya kumuingizia kipata hana.
Sababu hizo ndio zina wafanya baadhi ya mabinti kudate na waume za watu na hata kuwazalia watoto sababu tu wana hela. Huku wakiwapiga vibuti vijana wenzao ambao walikuwa na nia thabiti ya kuwaoa.Ila siku wakiachwa baada ya umri kwenda na kuaanza kuchuja ndipo huja kugundua vyote ni batili. Mara nyingi mademu ambao huangukia kwenye kundi hili ni wale wanao jiona ni pisi kali.
Mara nyingi wanaume ambao huonyesha nia ya kweli ya kutaka kumuoa binti wakati akiwa ktk ubora wake, huwaga ktk kipindi fulani cha kujitafuta japo ana uwezo ya kutimiza mahitaji ya msingi na si hizi luxury ambazo baadhi ya mabinti mnaziendekeza ambazo hazina msingi. Anza nae hivyo hivyo kijana wa watu,kuna baadhi ya wazee ambao ndoa zao zimedumu, wamenza na vistuli na mkeka leo hii wametoboa.