Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Hakuna mwanamke ambaye ana haki ya kusema yeye hana bahati ya mahusiano kiukweli ni uongo. Wanawake wengi ule umri wa kuwa mabinti na kuwa na mvuto wao huwa wanautumia kuleta maringo na kuruka na wanaume tofauti wakiamini hakuna kuzeeka.

Mwanamke ana miaka 10 tu ya kucheza karata zake na kuwa na uhakika wa kushinda nje ya hapo ni kubet na maisha yake.

Binti ana advantage ya kufanikiwa kimahusiano akiwa kati ya umri wa miaka 16 hadi 25. Kuanzia 26 hadi 30 huo ni umri wa nenda kwa tahadhari au lala salama.

Akivuka tu hizi stage mbili ndio basi. Huko mbele ni kubahatisha kwenda mbele.
Wakifika huo umri ndo wanajifanya wanajua kupenda, watakuganda kwelikweli.
 
Hakunaga maisha ambayo yatakutaa kabisa ukose mfumo wa kuishi na kujenga familia. Tatizo katika mahusiano ya miaka hii na hawa wanawake wa kizazi cha kuanzia 1985 kuja huku mbele ujuaji ni mwingi.

Mwanamke hataki kuanzia chini anataka kuanzia level ambayo inawataka muwe na kipato cha kuanzia milioni 3 kwa mwezi huku yeye haweki hata buku mezani na anaishia kukwambia wewe si ni mwanaume.

Kuna brother m'moja nimejifunza kwake. Alianza na mkewe walifunga ndoa huyo bro akiwa anakaa kwao yaani vyumba vya uwani. Wakakaa miezi michache wakaenda kupanga sehemu hapo vyumba vya 30,000 viwili yaani chumba na sebule. Na hiyo sehemu ni bondeni mvua ikinyesha unacheza twist na tope na madimbwi ya maji hadi ukome mixer vyura wanakutumbuiza hadi alfajiri, ila ndipo walipoanzia.

Leo wana nyumba nne moja ndio wanaishi tatu wamepangisha, wana magari mawili mke analake mume ana lake. Wana watoto 4.

Kimsingi maisha yanataka utulivu na projection nzuri ya mnaelekea wapi pamoja. Hizo fujo za nataka mwanaume mrefu, awe ana akaunti yenye seven figures, awe na gari na nyumba nzuri ya kupanga kuanzia vyumba vitatu iwe ndani ya fensi. Haya maisha ya ndoto za mchana huwa yanawagharimu sana mabinti wa kisasa na tamaa zao.

Mwanaume ukute amejiimarisha hivyo halafu awe anakungoja wewe tu utokee akushobokee? So wewe ni nani aisee.
Unatema nondo saana mkuu.
 
Wakati unasoma methali kuna ile methali pendwa inayoakisi uhalisia...

1.Mficha uchi ........

Sasa umefkia wasaa methali imekuwa kweli, somo achia mapaja muda sio rafiki. Maisha ndio haya haya. Game ngumu sikuhizi sio kila mwanamke ataolewa imekuwa ni kama bahati.
Hawa ni wadada kipindi cha usichana wanauliza umetoa wapi namba yangu, walipata wa kuwaoa wakawa hawajibu sms Extrovert
 
Nakuelewa sana.

Maisha hatufanani mazingira.

Wazazi wametuachia vijana jukumu kubwa hili la kutafutana mke na mume kwenye dunia iliyochafuka. Washenzi wengi kuliko wastaarabu. Chuo ni sehemu nzuri sana ya kupata mwenza. Shida ajira siku hizi tunachelewa kuzipata na bila ajira kuoa ngumu maana tunatokea familia maskini. Hivyo spouse wa chuo hamtoboi..

Kuna watu wanakulia mazingira ambayo wanapata spouse kwa jirani zao tu nyumba ya pili

Kuna watu wanapata ajira zinazowafanya wawe wanakutana na watu wengi wapya wanaotafuta wenza kila siku yao ya kazi.

Mwanamke mstaarabu na mwanaume mstaarabu kukutana ni ngumu sana zama hizi kama sio majirani, ama hamjasoma shule ama chuo pamoja.

Nje ya hapo hata mkikutana mnakuwa hamna imani maana hamjuani. Kitu kidogo tu mnaachana
Umeongea point [emoji4][emoji106]
 
Shida ni moja, psychology ya mwanaume haijaumbwa kudeal na mwanamke ambaye ana compete nae.

So ukisema hata Alpha males kuwa wapo interested na wanawake ambao wanalevel ya juu ya elimu, wapo high thinkers etc hivyo vitu huwa havivutii mwanaume yoyote ambaye ni mwenye uwezo wa kuongoza.

Labda hawa Beta males yaani wanaume wa kuburutwa.

Kuwa kiongozi wa mtu ni kupewa heshima yako unayostahili pasipo mwanamke kujihisi yupo juu yako ndani ya ndoa ila kama unahisi mwanamke ni lazma ajidogoshe ili wewe ujione umemzidi kila kitu ili umuongoze unavyotaka. Bro hiyo ni insecurity binafsi na ni reflection ya kitu ambacho umekosa ndani yako kuliko yule unaetaka kumuongoza..

Ni kwa mentality hii hii inayowafanya watu wengi waepuke kuoa makabila ambayo wanawake wanakuzwa kuwa independent kama wachagga ama wahaya.

Mkuu si lazma mwanamke awe dependent kwako ili umuongoze kwa sababu mwanamke hata afikie height ipi ya mafanikio. Bado atabaki kuwa emotional being ambaye anategemea emotional support yako kama mwanaume lakini kupata ushauri na maamuzi logical.

hapa ni Ukitoa wale nimewazungumzia ambao hujawa kiburi baada ya mafanikio kidogo. Ila wapo wanawake wengi sana ambao wanajitegemea na wanaishi na waume zao fresh
 
Tatizo jingine mabinti wa siku hizi wengi wenu, mnamatarajio makubwa ya kiuchumi kupitia ndoa na ndio maana hata standards zenu mnazo set kipindi mkiwa hot zinakuwa sio halisi. Ila jua likizama ndipo unakuja kujua vyote mlivyokuwa mkivitaka ni batili. Mnamahitaji mengi sana ambayo si ya msingi Mf vikoba viwili viwili,mchezo majina matatu,unataka simu kali tena latest,nguo zinazo trend,nyumba kali,usafiri nk wakati shughuli ya kumuingizia kipata hana.

Sababu hizo ndio zina wafanya baadhi ya mabinti kudate na waume za watu na hata kuwazalia watoto sababu tu wana hela. Huku wakiwapiga vibuti vijana wenzao ambao walikuwa na nia thabiti ya kuwaoa.Ila siku wakiachwa baada ya umri kwenda na kuaanza kuchuja ndipo huja kugundua vyote ni batili. Mara nyingi mademu ambao huangukia kwenye kundi hili ni wale wanao jiona ni pisi kali.

Mara nyingi wanaume ambao huonyesha nia ya kweli ya kutaka kumuoa binti wakati akiwa ktk ubora wake, huwaga ktk kipindi fulani cha kujitafuta japo ana uwezo ya kutimiza mahitaji ya msingi na si hizi luxury ambazo baadhi ya mabinti mnaziendekeza ambazo hazina msingi. Anza nae hivyo hivyo kijana wa watu,kuna baadhi ya wazee ambao ndoa zao zimedumu, wamenza na vistuli na mkeka leo hii wametoboa.
Endelea kutema nondo mkuu, mimi nina ushuhuda wa hawa mabinti wanaojiona pisi kali wakipitia haya maisha unayosema hapa.
 
Back
Top Bottom