Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Habari ya weekend great thinkers?

Maisha yananipa experience tofauti, Sikuwahi kufikiria kama ningefika third floor bila kuwa na familia wala watoto, kuna muda nahisi kupanic nahofia watoto wasije kuniita bibi badala ya mama, au kukosa kabisa sababu ya umri mkubwa🤔

Enzi hizo nilikua nashangaa mtu hasa mdada unafikaje hadi 30s huna familia, aisee kumbe ni kweli now ni mimi mwenyewe.

Mlioanza familia mkiwa 30s je ni kweli au mnaona dalili za watoto wenu kuwaita bibi au babu? Vipi changamoto za uzazi sababu ya umri mkubwa?😔

Nipo tayari kwa comments zote.

Happy valentine's day in advance 👏🥰
Naona unafaa kuwa bi mdogo wangu joo tupange kabla hujachelewa
 
Sijawahi kuumba hata nzi siwezi kuchagua sana sababu huko ni kumkufuru Mungu, basi tu mimi mwenyewe sielewi ila huenda ni tight schedule kipindi nasoma kidogo nilikua busy so sikua na social life sana😢
Pole sanaa, natumia wasaa huu kukupa ushauri kwako na kwa wengine, kama ulikuwa unajitenga tenga basi jitahidi kujichanganya na jamii unayoishi. Jitahidi kuwa simple most of the time, usijiweke high classic kama huwa unapendelea kuonekana hivyo. Si wanaume wote watakuwa na ujasiri wa kukutongoza wakishaanza kuona viashiria vya wewe kuwa ni mtu wa high class, onyesha tabia nzuri za kipekee mfano. Ukarimu hili unaweza kuliiga kwa wanawake wa kisukuma waliowengi wana ukarimu wa wazi(simaanishi kujirahisi), kuwa na kauli nzuri hata kama unaona umezinguliwa na lijamaa. Nje ya mwonekano wa sura na umbo, Wanaume tunaangalia haiba, nwanamke mnyenyekevu na mtiifu pia, siyo mwanamke anakuwa mjuaji mpaka unamuogopa. Kubwa katika yote amini yupo aliyeumbwa wa kufanana na wewe, ukikutana naye mtaelewana sanaa na mtaweza kwenda pamoja. Muombe Mungu kwani yeye ndiye muasisi wa taasisi ya ndoa.
 
Pole sana, ni hakika huenda ikawa ndiyo sababu mojawapo pia. Nakusihii utoke sasa ili uonekane katika kuchangamana na watu ndipo utaonekana. Kanisani siku ya jumapili ni ngumu mtu kukusoma ulivyo na kua serious sana na wewe. Lakini mkikutana huko kwenye shughuli za kijamii, mtu anakufahamu na kukuona wewe halisi. Usijali sanaa juu ya hilo, usibague shughuli, hata kanisani unaweza shiriki matukio ambayo ni ya katikati ya wiki ili uonekane.(Nime-assume wewe ni mkristo moja kwa moja)
Nimekujibu baada ya hii post, ila huenda ndiyo sababu coz sishiriki kikamilifu kiukweli
 
Tushachukulia tu poa.
Hamna namna mana changamoto za uchumi zimetuandama mpaka familia unaona nayo ni changamoto... kikubwa tunaishi maramoja! Hatuwezi kuishi tuminamisha vichwa kwa sonona kisa hatuna familia.. sisi sio wa kwanza na hatutakua wa mwisho.
Hongera mkuu, inaonesha unajitambua sana.
 
Noo nakataa ,sitongozwi sababu nadhani ya mvuto(sifuri)🤔
Usikate tamaa, huo mvuto ambao unajisemea hauna sijajua unazungumzia wa muonekano wa nje(sura+umbo) au mvuto kwa maana ya haiba yako pia? Kuna wanawake wanaolewa wana muonekano wa nje wa kawaida sanaa na mara nyingi waoaji hulenga hao(kuna siri hapa)
 
Back
Top Bottom