Kwanza maana ya neno dini ni 'njia' kwa maana ya muongozo, Sasa Mungu anaposema mfuate dini yake inamaana kuwa mfuate muongozo wake na kwanini asitoe muongozo wakati yeye ndio katuumba?
Muongozo wenyewe ndio dini mifano ya muongozo ni kama usizini, usiibe, usile riba, usidhulumu n.k
Na ndio maana kwa mujibu wa Qur an hakuna mtu ambaye hana dini kwa maana hakuna mtu ambaye hana muongozo wa maisha ni watu tu hujifanya mimi sina dini lakini kiuhalisia hakuna ambaye hana dini kwa maana mfumo mzima wa maisha anaoishi mwanadamu asubuhi mpaka usiku ndio dini yake mfano mtu anaye muamini Allah na mtume Muhammad akaswali na akaacha makatazo ya ALLAH huyo dini yake ni muislamu, Mtu anaye muamini Yesu kristo kuwa ndio mwokozi wa maisha yake na akaamini katika utatu mtakatifu huyo dini yake ni mkristo.
Sasa unaweza kujiuliza kuna watu wao sio waislamu wala wakristo wala wayahudi je wao ni dini gani na kwa mujibu wa Qur an hakuna mtu ambaye hana diini?
Jibu ni kuwa mfumo wa maisha wa huyo mtu ndio dini yake kama ni mtu wa uzinzi na riba basi dini yake ni dini ya upotofu.
Mila ni taratibu, Mungu anaposema ana mila ni kwa sababu yeye ndio kafundisha taratibu hizo ili sisi tuzifuate kwa hiyo Allah anaposema na mfuate mila yangu maana yake na mfuate utaratibu wangu kwa maana utaratibu ambaye yeye Allah kauweka ajili ya wanadamu
Mahali ambapo Mungu kawataja wayahudi na wakristo ni mahali ambapo anaongelea dini kwasababu uyahudi ni dini na ukristo ni dini.
Sasa sio kwamba Mungu hajaongelea watu wa jamii nyingine hapana Kuna aya katika qur an ALLAH anasema ياايحنس yaani enyi watu hapa ana maanisha watu wote kwa maana ya wahindi, wachina n.k
Hawezi kuwa sahau na nishajibu kwa swali la tatu
siwezi kuwajibia maadui wa waarabu kwa sababu mimi sio msemaji wa mataifa ya kiarabu.