The same hoja yako pia haionyeshi Mungu hayupo kwani ili Mungu awepo ni lazima atoe mali kwa watu wote?
Haya chukulia ndio katoa kwakuwa umeamua kupinga uwepo wake bado ungesema hizo mali watu wote wametafuta kwa juhudi zao.
Hapa ni vizuri kuelewa kuwa jitihada hazizidi kudra, Mungu ndio mmiliki wa hali zote, zote kwa maana ya zote na yeye ndio aliyesema tokeni mkatafute riziki hapa ndio watu huchanganya mambo wengi hudhani kuwa rizki ni mali tu, Kumbe rizki ni mjumuisho wa mambo mengi kama elimu,Afya,mali, n.k
Ndio maana utakuta mtu ana elimu lakini hana mali mungine ana mali lakini hana afya, Sasa usichukulie Mungu anagawa mali tu uka hitimisha kwa kuwa watu wengine hawana mali basi hayupo my friend logic ya wapi hiyo ? Mungu kuwa muweza wa yote na mwenye upendo wote sio sasa ndio watu wasife, ndio watu wawe na mali wote n.k, Yeye anabaki kuwa muweza wa yote tu hata kama wewe hauna mali, hata kama mtoto wako kafa kwenye ajali n.k
Alafu maswali yote hayo Mungu mwenyewe kashayajibu kwenye vitabu vya dini kuwa Yeye ndie Mola wa ulimwengu, Ametuumba wanadamu ili tuishi katika hii dunia na akatupa akili ili tuitumie kudhibiti matamanio yetu hivyo tumuamini yeye na kumuabudu, baada ya hayo ndio kuna maisha ya umilele na furaha kwa waliotumia akili zao vyema kumuabudu Mungu na hapo ndio hayo maswali yako yanapojibika kwa urahisi kuwa.. Baada ya kukuumba na kukuweka duniani kisha ukafa sasa unaenda kuishi tena katika umilele huko hakuna hizo ajali unazolalamikia huku duniani, Huko kuna mali unazoziangaikia huku duniani.