Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Nadhani hii inatokana na ufeki wa baadhi yetu hapa jukwaani.
Let's say labda mie Katrina najisifu hivi na vile halafu unanikuta katika uhalisia sipo kama ninavyojisifu unategemea moto wake hapa jukwaani utakuwaje?
Halafu sikuhizi kuna.....ambatanisha picha....
Yaani mtu akinijua kuwa mimi ndo fulani atanipiga na picha kisha itakuwa mada jadiliwa hapa jukwaani
Sasa katika kuepuka aibu ndogo ndogo kama hizo ndo tunaona heri tusifahamike tu😁😁
Fact madam Katrina 😍
 
Sana yani ukiona mdada mpaka kafika huku na kawa member kwa mda mrefu jua kabisa huyo anakitu cha ziada kichwani.

Jamii Forums ni maisha halisi na ni msaada mkubwa kwa jamii na nchi kwa u jumla.
Kongole nyingi kwa Maxence Melo
Sasa kama nyie wanaume mnatambua hili, kwanini kila siku mada za kutuponda na kutusagia wanawake haziishi humu Jf?
 
Najua kuna ambao wanakutana kwa matukio maalum.
Ila si ile ya ghafla kwenye daladala au sehemu ya mkusanyiko.
Watu wengi sana simu zao naona zina App ya Jf, na wanafungua kisirisiri😂😂 wakiwa kwenye halaiki za watu🤣
Ya ghalfa nilishakutana na mdada mmoja tu ila yeye ndio alijua id yangu mimi aligoma nijue yake , akiona hii lazima ata like hapa🤣🤣🤣
 
Kuna mwamba ni mwana ila si kivile ni deal tu huwa zinatukutanisha aliniona natumia JF na yeye akasema ni member ila hakujua natumia ID gani kwa sababu nilikuwa nasoma nyuzi mbalimbali tu

Tukakubaliana kuwa hakuna haja ya kujuana tuendelee kuwa anonymous

Tukakubaliana kuwa ukiwa mtumiaji wa JF ni vizuri usifahamike na yoyote
 
1.2019 nipo kwenye Coaster natoka Arusha kwenda Moshi...Nilikaa ile siti karibu na mlangoni...nipo JF kuna Uzi mmoja ulikuwa hot sana na Dada mzuri Heaven Sent kuna ushauri alikuwa anautoa kwenye hiyo mada..nikawa nafuatilia kwa makini sana wakati huo sikuwa active sana hapa jukwaani...kufika Machame road kuna Abiria akashuka Mkaka( si haba)😃wakati anashuka akaniambia kumbe wewe ndiyo Makiseo( ID yangu ya mwanzo).

2. Kibaruani kwangu...Kuna mmojawapo alinibamba...Kipindi App ikiwa ipo poa...Ila hakuona ID...Akaniambia kumbe Familia😄
Ikawaje sasa Makiseo ukabadili ID 🎫 , Au ndo ulihofia mkaka (Si haha) atakusumbua 😁
 
Kuna mwamba ni mwana ila si kivile ni deal tu huwa zinatukutanisha aliniona natumia JF na yeye akasema anatumia ila hakujua natumia ID gani kwa sababu nilikuwa nasoma nyuzi mbalimbali tu

Tukakubaliana kuwa hakuna haja ya kujuana tuendelee kuwa anonymous

Tukakubalina kuwa ukiwa mtumiaji wa JF ni vizuri usifahamike na yoyote
Kwa nini mkuu iwe vizuri usifamike?
 
Ya ghalfa nilishakutana na mdada mmoja tu ila yeye ndio alijua id yangu mimi aligoma nijue yake , akiona hii lazima ata like hapa🤣🤣🤣
🤣🤣🤣
Kwa mimi binafsi naona Id za kiume hazina mambo mengi
Ngoma ngumu ipo huku kwetu kwenye id za kike.
Yaani tunasoma jf kwa shida sana tukiwa kwenye mikusanyiko
 
Habari za muda huu wanajamvi!

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa Jamii Forums katika maisha ya uhalisia (Jamii)?
🔹 Ulijisikiaje?
🔹 Ulijitambulisha kuwa na wewe ni mwanachama, au ulifanya kama hauijui kabisa?
🔹Baada ya kujitambulisha mlikuwa na mazungumzo ya aina gani?

Nimeuliza hivi kwa maana watumiaji wengi wa JF hutumia huu mtandao kwa Siri sana

Share nasi uzoefu wako! 📢👇
Naamini kila mtu ana hadithi ya kipekee ya kusimulia.

#JamiiForums #Jamii #Uhalisia #UzoefuWako
Waliowahi kukutana na Mimi hasa Kilingeni Msata hii sura sio ngeni kwao
Our forefathers went through pain because of magic.jpeg
 
miezi kama miwili nyuma nilikua kwenye kosta natokea mwanga kwenda moshi nilikaa siti ya mwisho kabisa kwenye kutupa tupa macho kuna jamaa mmoja akafungua simu na kuingia jf ya app nikawa namsorora kila muda anajistukia anaangalia nyuma alipitia mada kadhaa akafunga simu
 
Back
Top Bottom