Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Fact madam Katrina 😍
 
Sana yani ukiona mdada mpaka kafika huku na kawa member kwa mda mrefu jua kabisa huyo anakitu cha ziada kichwani.

Jamii Forums ni maisha halisi na ni msaada mkubwa kwa jamii na nchi kwa u jumla.
Kongole nyingi kwa Maxence Melo
Sasa kama nyie wanaume mnatambua hili, kwanini kila siku mada za kutuponda na kutusagia wanawake haziishi humu Jf?
 
Najua kuna ambao wanakutana kwa matukio maalum.
Ila si ile ya ghafla kwenye daladala au sehemu ya mkusanyiko.
Watu wengi sana simu zao naona zina App ya Jf, na wanafungua kisirisiri😂😂 wakiwa kwenye halaiki za watu🤣
Ya ghalfa nilishakutana na mdada mmoja tu ila yeye ndio alijua id yangu mimi aligoma nijue yake , akiona hii lazima ata like hapa🤣🤣🤣
 
Kuna mwamba ni mwana ila si kivile ni deal tu huwa zinatukutanisha aliniona natumia JF na yeye akasema ni member ila hakujua natumia ID gani kwa sababu nilikuwa nasoma nyuzi mbalimbali tu

Tukakubaliana kuwa hakuna haja ya kujuana tuendelee kuwa anonymous

Tukakubaliana kuwa ukiwa mtumiaji wa JF ni vizuri usifahamike na yoyote
 
Ikawaje sasa Makiseo ukabadili ID 🎫 , Au ndo ulihofia mkaka (Si haha) atakusumbua 😁
 
Kwa nini mkuu iwe vizuri usifamike?
 
Ya ghalfa nilishakutana na mdada mmoja tu ila yeye ndio alijua id yangu mimi aligoma nijue yake , akiona hii lazima ata like hapa🤣🤣🤣
🤣🤣🤣
Kwa mimi binafsi naona Id za kiume hazina mambo mengi
Ngoma ngumu ipo huku kwetu kwenye id za kike.
Yaani tunasoma jf kwa shida sana tukiwa kwenye mikusanyiko
 
Waliowahi kukutana na Mimi hasa Kilingeni Msata hii sura sio ngeni kwao
 
miezi kama miwili nyuma nilikua kwenye kosta natokea mwanga kwenda moshi nilikaa siti ya mwisho kabisa kwenye kutupa tupa macho kuna jamaa mmoja akafungua simu na kuingia jf ya app nikawa namsorora kila muda anajistukia anaangalia nyuma alipitia mada kadhaa akafunga simu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…