Yaan usimwamini mtu,
Hata kama ni ndugu,
Nakumbuka mwaka 2001 nikiwa ufaransa namalizia masomo yangu,nikapata mchongo mkubwa wa hela, ni siri yangu sitasema,
Nikaamua niweke mazingira ya kufungua kimradi maeneo ya muleba kagera, mradi
wenyewe sitautaja ila ulikuwa planned kugharimu 12,000 USD then, nikamtumia mdogo wangu kabisa wa tumbo moja aufungue,
Akaenda sehem akanipigia picha majengo kwamba kayakodi hayo,
Nikakubali nikafurahi kwakuwa ilikuwa sehem powa, akasema anaenda dar kufuatilia usajiri na kupitia wizara na taasisi zote husika, nikamuongezea 500 USD, kumbe ndo ilikuwa njia kurudi bongo nakuta jamaa alienda Malaysia, hakuna kitu alikuwa ananidanganya,
Nikataka nimfungulie kesi, wazazi wakaingilia eti undugu ni muhimu kuliko mali,
Iliniuma mno
Je una la ku share nasi?