Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Nilimfungulia mdogo angu wa damu duka la karibu ml12 baada ya mwaka naenda pale nakuta limefungwa na yeye kakimbia, mpaka leo mwaka 4 hatuongei tukikutana kwenye msiba km hatujuani sana sana yeye ndio ananipiga chenga, nilipo hakai wala haji, alafu hiyo ni biashara ya pili anaiua.
Aisee ungemswekaa ndaniii
 
kwakweli inauma kuuwaamini ndugu unaweza kujinyonga, inaniuma mno kwa hasara hii nakumbuka ilikuwa tarehe 12/7/2015 na baadae 25/10/2015 nikamwamini mtu wangu wa karibu Magufuli tukampa nchi kwakweli yanayoendelea mungu ndo anajua
cc tindo
Hahahaaaaaaaa.... Unamwaminije mtu aliyeshindwa kupata combi (masomo 3 tu) toka form 4 kwenda form 5 eti aongoze nchi?
 
Aisee ungemswekaa ndaniii
Hapo ya kwanza niliachana nae bila kumpa chochote bimkubwa analaumu nimemwachaje bila kumpa chochote ikabidi nimpe kiduka flani cha uswazi nilianzia nacho maisha kilikua na km m2 plus nacho akaua tena, ndio baada ya miaka m4 kaja kuomba msamaha ndio nkamfulia hilo la mwisho.
 
MAMA YAKO ATAKUTAPELI KIVIPI? AMEKULA VYAKE. NANI KAMA MAMA.
Hata mimi nashangaa. Mama kama anataka pesa, anaomba tu. Kuna watu mnakopeshana na mama zenu? Inaonekana mama zenu bado vijana sana.
 
Kamuoa dada yangu kabisa aisee. Aliniahidi atanikabidhi Leo lakini simu hazipokelewi

...Mkuu, Unatakiwa ukazushe bonge la Valangati mbele ya dada yako ili ajue kaolewa na mtu gani! Si ajabu anajisifia kwa dada yako kwamba amekumalizia kazi yako iliyopita ila hutaki kumlipa! Chukua hatua....[emoji35][emoji35]
 
Majaribu haya nimeyapitia sana - marafiki na ndugu. Nina karibu mil 10 kwenye mikono ya watu huko nje tangu 2005. Sitaki kueleza jinsi ilivyotokea ili nisije kujulikana identity yangu (Omusolopogasi) kwa hao watu. Lakini nimejaribu kusahau na tumeendelea na mahusiano kana kwamba hakuna kitu. Ila kuanzia hapo, sijakopesha ndugu/rafiki na wala sitakopesha tena. Kama hali inaruhusu, ninatoa tu - pesa ndogo ndogo - wala si kukopesha. Kama kuna mgonjwa, namnunulia dawa nampa nk nk.
 
Kuna jamaa aliniambia anataka tufungue sehemu ya kuwafundisha watu basic ya computer
Alipata sehemu akalipia kila kitu na mimi nilichangia computers 30 kwa kuanzia na sehemu ilipata wateja wengi tu ingawa alikuwa anakula upande wa serikali zaidi kwa utapeli (sio Tz)
Mimi sikuwa nafanya nae bali alikuwa ana run show mwenyewe baada ya kukamatwa kwa wizi wa mali ya umma akagawa computer zote

Nilijaribu kudai sana anirudishie changu bila mafanikio.

Ilipita miaka bila kumsemesha na yeye akaoa na kupata watoto watatu
Kumbe shida zikaanza hapo
Nikaamua kwenda kumtembelea ili anipe changu
Mungu mkubwa nilichokikuta namhurumia mpaka leo kwani hali ya nyumbani kwake ilikuwa duni sana

Kwa huruma nikamchukua na kwenda nae supermarket na kujaza chakula mpaka diapers za watoto yaani kila kitu
Nikamuachia na hela kidogo

Jamaa alilia sana
Nikamwambia ndio dunia na ipo siku tutaiacha
...Ulifanya jambo jema sana Mkuu. Ubarikiwe [emoji120][emoji120]
 
Me mtu wa karibu mno kanitapeli.Nikimdai anasema anakumbuka atanipa but hafanyi utekelezaji
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Aiseee stori yako kama yangu vile. Kuna rafiki yangu tangu utoto nilimuomba anisaidie kusimamia ujenzi kutokana na mimi kuwa mbali. Pia kama mnavyojua mafumdi kwa kuhamisha vifaa. Basi jamaa nikampa na kazi ya kusimamia na manunuzi ya materials hapo ndio nilifutahi na roho yangu. Kila bidhaa aliongeza bei. Tripu ya mchanga laki moja yeye aliweka laki na 30 alipandilia bei hadi kwenye ufundi.
Ikaja kwenye fremu za milango na grill za madirisha hakuniacha pia. Fremu za milango nilinunua mbao za mninga ili kupunguza gharama so ikawa gharama ni fundi tu. Huyo rafiki yangu alichukua baadhi ya frem za milango na kuuza akauza na mbao za kwa fundi.
Nmekuja kurudi nikiangalia hesabu yangu na nyumba ilivyonikajua tu hapa nmepigwa parefu sana. Nikamuuliza hivi kweli gharama hii ni sawa na nyumba hii akakasirika eti sina shukurani amenisaidia sana kusimamia ujenzi na hajala hata mia yangu ndio kwanza amelipa sana hela zake.
Tangu siku hiyo akaacha kupokea smu zangu na akanipga block moja matata sana kuanzia fb hadi kila sehemu. Nikatulia tu nikamalizia ujenzi nikiangalia hapo hapo.
Hili moja bado kwenye biashara ya kuchanga mtaji niliweka kama 6mils mwenzangu hakuweka hata mia ndio kwanza akala hela zangu. Mungu sio ngwizukulu wala kindukusulikucho saizi jamaa hama hata mia mbovu juzi kat ananipgia smu anaomba hata buku mbili ya kula mke alikimbia na watoto. Nilimwambia sina hata mia labda akakope finca kama anakopesheka
Hii mambo ya mtu kukupiga cha juu unapomwomba asimamie mradi wako halafu baadae ukija kumuuliza anakugeuzia kibao yapo sana Bongo.
 
Aisee kwenye suala la pesa sitakaa nimuamini mtu yeyote... Mpaka leo bado nina majeraha ya dhuluma niliyodhulumiwa mwezi wa 5. Almanusura nilazwe, niliumwa mno...
Jikaze nakuhakikishia baada ya muda utapata kushinda hizo ulizopigwa. Miaka kama mitano iliyopita nilijiwa na jamaa yangu akaniambia kuna biashara ya masandaku na mabegi anayofanya na inalipa sana lakini hana mtaji wa kutosha kuzungusha. Akanishauri niongezee mtaji halafu biashara (duka) iwe yetu sote. Nikampa milioni 5. Kweli jamaa akachakarika baada ya mwaka na nusu akawa amenunua bajaji mbili na duka limependeza kweli. Sasa kilichonishangaza kila nikitembea kwenye biashara naona jamaa amenibadilikia na kununa sana.. Uchangamfu wote umeisha. Mimi nilikuwa naishi mkoa mwingine. Nikawa najiuliza kwanini? . Basi siku moja akaniondolea uvivu. Akanieleza makavu makavu kuwa biashara inaenda vibaya na kuna uwezekano fedha zikapotea. Akasema hataki lawama hivyo atarudisha fedha zangu. Nilisikitika sana lakini sikuwa na la kufanya nikakubaliana naye. Nikampa account namba arudishe. Baadae ndiyo nikaja kugundua kuwa baada ya biashara kuchanua alipata tamaa ya kuimiliki mwenyewe na alikuwa na mpango wa kurudisha kweli milioni 5 yangu. Lakini alivyonifukuza tu mambo yakaanza kwenda mrama mpaka sasa hana kitu tena na fedh yangu alishindwa kurudisha.
 
...Mkuu, Unatakiwa ukazushe bonge la Valangati mbele ya dada yako ili ajue kaolewa na mtu gani! Si ajabu anajisifia kwa dada yako kwamba amekumalizia kazi yako iliyopita ila hutaki kumlipa! Chukua hatua....[emoji35][emoji35]
Siku zake zinahesabika. Nimetumwa hela aisee
 
Back
Top Bottom