Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Yaani hapa sijui hata nifanyeje. Ni shemeji yangu kabisa. Wakati naanza ujenzi alikuwa ni mshauri Wangu lakini najuta. Kwanza aliniambia kuweka dirisha za grill ni gharama sana ila kwa kuwa yeye ni Fundi seremala atanitengenezea madirisha ya mbao kwa 150,000 kila moja. Alalamba hela ya dirisha zote, hela ya from za milango na hela ya top wakati naanza msingi. Hadi napaua hajanikabidhi Kazi hata moja. Nikamsamehe hela ya madirisha laki 9 Ili anitengezee vitu vilivyobaki. Hamuwezi kuamini ndugu zangu Leo Fundi wanamalizia Skimming bila kuweka fremu za milango wala top zake. Hapa nimekaa nawaza nimfanyeje. Naombeni ushauri wenu wakuu. Nimfanyeje kama amechukua zaidi ya Million 2 na sijapata Kazi hata moja
Kaa mbali
 
Kuna jamaa aliniambia anataka tufungue sehemu ya kuwafundisha watu basic ya computer
Alipata sehemu akalipia kila kitu na mimi nilichangia computers 30 kwa kuanzia na sehemu ilipata wateja wengi tu ingawa alikuwa anakula upande wa serikali zaidi kwa utapeli (sio Tz)
Mimi sikuwa nafanya nae bali alikuwa ana run show mwenyewe baada ya kukamatwa kwa wizi wa mali ya umma akagawa computer zote

Nilijaribu kudai sana anirudishie changu bila mafanikio.

Ilipita miaka bila kumsemesha na yeye akaoa na kupata watoto watatu
Kumbe shida zikaanza hapo
Nikaamua kwenda kumtembelea ili anipe changu
Mungu mkubwa nilichokikuta namhurumia mpaka leo kwani hali ya nyumbani kwake ilikuwa duni sana

Kwa huruma nikamchukua na kwenda nae supermarket na kujaza chakula mpaka diapers za watoto yaani kila kitu
Nikamuachia na hela kidogo

Jamaa alilia sana
Nikamwambia ndio dunia na ipo siku tutaiacha
 
Yaan usimwamini mtu,
Hata kama ni ndugu,
Nakumbuka mwaka 2001 nikiwa ufaransa namalizia masomo yangu,nikapata mchongo mkubwa wa hela, ni siri yangu sitasema,
Nikaamua niweke mazingira ya kufungua kimradi maeneo ya muleba kagera, mradi
wenyewe sitautaja ila ulikuwa planned kugharimu 12,000 USD then, nikamtumia mdogo wangu kabisa wa tumbo moja aufungue,

Akaenda sehem akanipigia picha majengo kwamba kayakodi hayo,
Nikakubali nikafurahi kwakuwa ilikuwa sehem powa, akasema anaenda dar kufuatilia usajiri na kupitia wizara na taasisi zote husika, nikamuongezea 500 USD, kumbe ndo ilikuwa njia kurudi bongo nakuta jamaa alienda Malaysia, hakuna kitu alikuwa ananidanganya,

Nikataka nimfungulie kesi, wazazi wakaingilia eti undugu ni muhimu kuliko mali,

Iliniuma mno

Je una la ku share nasi?
Je alifanikiwa safari yake ya Malaysia? Kama alifankiwa alikuja na kurudisha fedha zako? Uhusiano wenu ukoje kwa sasa? Kama unaweza ku share ni vizuri kwani hapa tunajifunza mengi
 
Kuna jamaa aliniambia anataka tufungue sehemu ya kuwafundisha watu basic ya computer
Alipata sehemu akalipia kila kitu na mimi nilichangia computers 30 kwa kuanzia na sehemu ilipata wateja wengi tu ingawa alikuwa anakula upande wa serikali zaidi kwa utapeli (sio Tz)
Mimi sikuwa nafanya nae bali alikuwa ana run show mwenyewe baada ya kukamatwa kwa wizi wa mali ya umma akagawa computer zote

Nilijaribu kudai sana anirudishie changu bila mafanikio.

Ilipita miaka bila kumsemesha na yeye akaoa na kupata watoto watatu
Kumbe shida zikaanza hapo
Nikaamua kwenda kumtembelea ili anipe changu
Mungu mkubwa nilichokikuta namhurumia mpaka leo kwani hali ya nyumbani kwake ilikuwa duni sana

Kwa huruma nikamchukua na kwenda nae supermarket na kujaza chakula mpaka diapers za watoto yaani kila kitu
Nikamuachia na hela kidogo

Jamaa alilia sana
Nikamwambia ndio dunia na ipo siku tutaiacha
Una moyo mzuri sana mkuu, yani mtu unamdai na bado unamuonea huruma aisee, itakua alijutia sana alichokufanyia.
 
Wacha nitoe yangu kwa huzuni
Nitapeliwa na kuibiwa na mzazi mwenzangu wa ndoa kabisa zaidi ya milioni 10 nilimpakilia mzigo wa biashara akadai amekopwa kumbe alikula na malaya huko mkoa miaka mitatu nikafilisika nahangaika na watoto yeye ata chembe ya huruma hana nikambuluza mahakamani mahakama ikalegeza shtaka sikupata pesa yangu mpaka Leo na yeye yupo bado anavizia vizia kuniumiza tena namkwepa mahakamani niliambulia talaka na pasipi huduma ya watoto ila nakomaa nao nikikwama nauza nilichonunua maisha yanaenda huyo jamaa hana mafanikio yotote duniani ladhi ya mke ipo kweliii
 
Kuna mbwa mmoja anaishi kinondoni hapo nimemtumia mzigo wa kutuma mkoani wenye thamani ya 920,000 alafu anazingua kauza mzigo wa watu Alafu anajibu kwa jeuri nimemtafta anazima simu nikaamua kwamba niwatafte ndugu zake, ananiambia basi hao ndugu ulowaambia kunichafua ndo wakulipe,

Nasema hivi huyu jamaa nikimkamata ndo basi
 
Mtoe marinda tu mkuu.
 
haya mambo basi tu jamaa alikuwa na mke na watoto nikamuonea huruma kwenye dili la m5 (ambalo mimi ndo injinia wake) anipe m1.5 hadi leo ajanipa ananizungusha

nacho furahi msimu mpya (tunafanya kazi kwa msimu) ananitegemea nifanye mazuri ntamliza mpaka ajute yaan kwenye m5 na nafahamu kashaipokea ila ananikwepa anashindwa nipa m1

ba mdg kampiga mzee wangu zaidi ya m100 za kustaafu. hii dunia hatari tupu
 
Komaa haya manyau mpaka yalete hela
 
Back
Top Bottom