Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Je, umewahi kumwamini ndugu au rafiki wa karibu na akakutapeli mkwanja mrefu?

Mimi mwaka 2014/15
Nililima mpunga Morogoro nikamkabizi mtu 50M..watoto wa mjomba ...wakajengea nyumba....wakaolea...then wakaaza kuniloga ili nice
Mpaka Leo nimeyumba kiuchumi
Najuta sana ndugu sio watu kbsa
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Kuna jamaa aliniambia anataka tufungue sehemu ya kuwafundisha watu basic ya computer
Alipata sehemu akalipia kila kitu na mimi nilichangia computers 30 kwa kuanzia na sehemu ilipata wateja wengi tu ingawa alikuwa anakula upande wa serikali zaidi kwa utapeli (sio Tz)
Mimi sikuwa nafanya nae bali alikuwa ana run show mwenyewe baada ya kukamatwa kwa wizi wa mali ya umma akagawa computer zote

Nilijaribu kudai sana anirudishie changu bila mafanikio.

Ilipita miaka bila kumsemesha na yeye akaoa na kupata watoto watatu
Kumbe shida zikaanza hapo
Nikaamua kwenda kumtembelea ili anipe changu
Mungu mkubwa nilichokikuta namhurumia mpaka leo kwani hali ya nyumbani kwake ilikuwa duni sana

Kwa huruma nikamchukua na kwenda nae supermarket na kujaza chakula mpaka diapers za watoto yaani kila kitu
Nikamuachia na hela kidogo

Jamaa alilia sana
Nikamwambia ndio dunia na ipo siku tutaiacha
Ubarikiwe sana Ndugu yangu kwa ulichokifanya umenifundisha kitu sana
Naomba nikuombe tena rudi kamwangalie tena msaidie haweze kupata amani ya maisha sana
Ndio utajiri wa Roho huu
 
Yaani hapa sijui hata nifanyeje. Ni shemeji yangu kabisa. Wakati naanza ujenzi alikuwa ni mshauri Wangu lakini najuta. Kwanza aliniambia kuweka dirisha za grill ni gharama sana ila kwa kuwa yeye ni Fundi seremala atanitengenezea madirisha ya mbao kwa 150,000 kila moja. Alalamba hela ya dirisha zote, hela ya from za milango na hela ya top wakati naanza msingi. Hadi napaua hajanikabidhi Kazi hata moja. Nikamsamehe hela ya madirisha laki 9 Ili anitengezee vitu vilivyobaki. Hamuwezi kuamini ndugu zangu Leo Fundi wanamalizia Skimming bila kuweka fremu za milango wala top zake. Hapa nimekaa nawaza nimfanyeje. Naombeni ushauri wenu wakuu. Nimfanyeje kama amechukua zaidi ya Million 2 na sijapata Kazi hata moja
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Daaah mim mtoto mamdogo nilimpa kiwanja akopee siamin mpk kesho alichonifanyia kwakwel nawaza ata kujiua huruma yang ili niponza mana alikuja analia leo hii daaah
Mkuu pole sana vipi alifanya nin huyo ndugu?
 
Mimi kuna binti nikimdaka napiga ndogo kupunguza machungu.
 
Ubarikiwe sana Ndugu yangu kwa ulichokifanya umenifundisha kitu sana
Naomba nikuombe tena rudi kamwangalie tena msaidie haweze kupata amani ya maisha sana
Ndio utajiri wa Roho huu
Anaona aibu sana ingawa najaribu kumtafuta
Leo hii nimepita karibu na nyumba yake ya zamani ingawa nasikia haishi tena na mke wake, na watoto watakuwa wamekuwa sasa maana ni kitambo

Mali sio kila kitu ila uungwana ni muhimu sana you never know nani atakusaidia siku moja katika maisha yako kwani hatujui ya kesho.

Nashukuru kwa kuliona hilo
 
Duuh!! Hivi shuhuda zote hizi kuna siku nitaja tapeliwa kizembe tena na watu uchwara wanaojiita ndugu zangu? Haitokaa itokee asee!
Labda mama yangu ndo anitapeli maana mpaka umri huu sina ndugu wa dhati kama yeye! Yeye hata aje ale 50M zangu haitaniuma!
Ndugu wengine siwakopi hela bali nitawapa as a grant na haitozidi 10k maana hata asiporudisha haitoniuma kivile!
 
Kodisha gari(fuso)nenda nalo ofisini kwake;ukifika beba kila utakachokikuta hapo from vifaa vya ufundi mpk bidhaa za wateja wengjne kama madirisha,milango,masofa then peleka kwako,wateja wakianza kumsumbua khs bidhaa zao jamaa lazima akuibukie kwako.

Then hakuna kumpa bidhaa yoyote ya mteja mpk akamilishe hivyo vitu vyako tena anatengenezea hapo hapo kwako,kuwa mbabe kwny hili ni muhimu boss.

Tenga wiki 1 ya kusimamia zoezi hili then leta feedback hapa mkuu,it works.
Hahahahaha wazo zuri hili
 
Kuna ndugu yangu nilimuagiza akaninunulie kiwanja nje ya mji huko, 2004. Akaniambia 1.5m. Nikamtumia akanunua kwa niaba yangu. Baadae sana nikagundua alinunua kwa 700,000 tu...ila wakati nagundua hivyo hilo eneo thamani ya viwanja ilikuwa 15m wala sikum-mind ila nilimshukuru.

Kwahio ukimpiga ndugu au rafiki yako ongeza cha juu ila kitu kiwepo. Ukila na kipofu usimguse mkono.
Hapo hakukupiga bali alikula ya udalali
 
Mwaka jana nimemkopesha rafiki yangu 70, 000 kama nauli afate Transcript ili atume maombi BAKITA(walipohitaji walimu wa Kiswahili watume vyeti vyao). Cha ajabu ananunua pikipiki wakati anajua namdai na pia anafundisha English Medium lakini pesa halipi. Hapa ndo inafika nakumbuka bango lisemalo KUNENEPA WAKATI NAKUDAI NI DHARAU.
 
Duuh. Kwa nusu bei tena Mkuu. So ndio mwanzo wa kuniletea milango ya mbao ambazo kesho tu mchwa wamefanya makazi. Tatizo sio being Bali quality
Wala usikubali. Wengine ni matapeli tu mjini hapa, wanajifanya mafundi kumbe sio.

Mwambie dadako akomae na mumewe akulipe vifaa vyako, bila hivyo unavunja udugu!!
 
Kuna jamaa aliniambia anataka tufungue sehemu ya kuwafundisha watu basic ya computer
Alipata sehemu akalipia kila kitu na mimi nilichangia computers 30 kwa kuanzia na sehemu ilipata wateja wengi tu ingawa alikuwa anakula upande wa serikali zaidi kwa utapeli (sio Tz)
Mimi sikuwa nafanya nae bali alikuwa ana run show mwenyewe baada ya kukamatwa kwa wizi wa mali ya umma akagawa computer zote

Nilijaribu kudai sana anirudishie changu bila mafanikio.

Ilipita miaka bila kumsemesha na yeye akaoa na kupata watoto watatu
Kumbe shida zikaanza hapo
Nikaamua kwenda kumtembelea ili anipe changu
Mungu mkubwa nilichokikuta namhurumia mpaka leo kwani hali ya nyumbani kwake ilikuwa duni sana

Kwa huruma nikamchukua na kwenda nae supermarket na kujaza chakula mpaka diapers za watoto yaani kila kitu
Nikamuachia na hela kidogo

Jamaa alilia sana
Nikamwambia ndio dunia na ipo siku tutaiacha
Hongera sana.

Dhuluma wanasema inalipwa hapahapa duniani.
 
Mwaka jana nimemkopesha rafiki yangu 70, 000 kama nauli afate Transcript ili atume maombi BAKITA(walipohitaji walimu wa Kiswahili watume vyeti vyao). Cha ajabu ananunua pikipiki wakati anajua namdai na pia anafundisha English Medium lakini pesa halipi. Hapa ndo inafika nakumbuka bango lisemalo KUNENEPA WAKATI NAKUDAI NI DHARAU.
Hajawahi kukupa hata rift?
 
Back
Top Bottom