Wanajamvi,salamu kwanza.
Kutokana na mfululizo wa matukio ya mauaji na ugaidi hapa nchini,na kupelekea kuwepo na shirika la upelelezi la marekani(FBI) wakishirikiana na na jeshi la polisi nchini,hii ni dhahiri kuwa huu ni uzushi na danganya toto kwa watanzania.
Nikianzia na tukio la Dr.ulimboka.Mtu aliyekamatwa si mtanzania,kwa nini Dr ulimboka asihojiwe wakati yeye ndio victim yu hai na anawatambua waliomteka,ulimboka alikamatwa akiwa hai na alikuwa anatambua kila kitu kilichokuwa kinaendelea.Huu ni uzushi na uongo kwa watanzania,aliyekamatwa kwenye tukio hilo kesi yake haieleweki imefikia wapi,huku tukio la kutekwa na kuteswa kwa ulimboka likifuatiwa na kauli ya kwamba NI SIRI YA TAIFA.Ninachokifahamu serikali wanaogopa kumpeleka mahakamani na wanatumia mahakama kama sehemu ya kufichia maovu kwa kisingizio cha upelelezi haujakamilika na kuwa na hofu ya Dr ulimboka kuwa shahidi namba moja.Wamemkamata kijana wa watu kama funika kombe tu.Huu ni uzushi na udanganyifu kwa watanzania.
Pili,tukio la mabomu Arusha ktk kanisa la Olasiti na katika mkutano wa chadema,wote wanaokamatwa ni raia wa kigeni kulikoni? Huu ni uzushi. Hakuna ukweli wowote,bali ni uzushi wa kuwadanganya watanzania ilihali serikali inajua mrushaji wa mabomu ni nani.Hii inafanyika ili kuwapoza watz kwani jambo likiwa mahakamani si rahisi kulizungumzia.kwa nini mwigulu asihojiwe kwa kauli yake ya kwamba "watu wa Arusha msipoichagua ccm mtakufa" serikali inajua aliyerusha bomu lakini wanakamata watu wasio na hatia ili kuzuia mjadala,hii ni mbinu chafu na tumeishajua kuwa ndio sehemu ya serikali kujinusuru na hizi tuhuma.
Kwa mtazamo wangu,hakuna ukweli wowote na serikali ni mtuhumiwa no moja,lakini ipo siku ukweli utajulikana tu.Serikali ya ccm inafanya maovu na kujifichia mahakamani kwa kudai upelelezi unaendelea...huu ni uongo wa hali ya juu,na udanganyifu mkubwa kwa watz..wakati ukweli upo.