Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111
kamanda wa polisi wa mkoa wa iringa baada ya kifo cha mwangosi akapandishwa cheo kaletwa makao makuu sasa unadhan wanaweka mfano gani? kamanda wa polisi wa morogoro aliyeamridha ponda atandikwe risasi ya kichwa bahati mbaya ikampata began kapandishwa cheo yuko makao makuu sasa unategema mfano gani wanaojenga! kwamba makamanda wa mikoa kufanya mauaji kunaweza kua source ya promotion!!!
 
Hili jeshi linaendeshwa na utashi wa askari husika wengine waelewa,wengine washkaji,wengine wasanii,wengine wezi,na majambazi,wengine fitna ,wengine wazinzi,wengine walevi,basi mchanganyiko tu,washachanganyikiwa ,wengine wagomvi,wala rushwa duh,balaa,wengine walokole,kwa hiyo jeshi la polisi halina sura inayoeleweka.
 
Mtoa mada samahani ,hiv kuna taasisi una iman nayo nchi hii????
 
Mtoa mada samahani ,hiv kuna taasisi una iman nayo nchi hii????

Swali lako ni la msingi na ni kweli kuwa taasisi nyingi za serikali ni wakala wa viongozi wetu!!!

Serikali kwa ujumla imepoteza sifa ya kuwa mlinzi wa raia wake, lakini katika taasisi zote za serikali polisi wamekithiri kwa kukiuka hata haki za msingi na za kikatiba za raia!
 
Swali lako ni la msingi na ni kweli kuwa taasisi nyingi za serikali ni wakala wa viongozi wetu!!!

Serikali kwa ujumla imepoteza sifa ya kuwa mlinzi wa raia wake, lakini katika taasisi zote za serikali polisi wamekithiri kwa kukiuka hata haki za msingi na za kikatiba za raia!

Mkuu kinachotokea hapa ni matumizi mabaya ya ile dhamana.kwa sababu wamekabidhiwa dhamana fulani,kwa kutotumia utu anaweza kukufanaya chochote kusingizia anasiamia sheria.

Kila sekta ina madudu ila jamaa sio kwamba wamezidi ila wanang'aa kwa sababu ndio sekta inayotakiwa kuzingatia haki katika kutoa huduma.

Mfanao hembu angalia-mahakamani,hospitarini,mashuleni,takukuru,tra,tanesko,bandarini,watu wanpiga madili asikwambie mtu but silently huwezi jua.tunaona wana nafuu labda sababu tunakutana nao kwa nadra sana tena ikibidi lakini polisi sjui utawakwepaje?kwenye shida na raha wao wapo na wewe kupata chochote haijarishi un hali gani au wewe nani.

Tumefeli sehemu,sehemu kubwa sana tu itakayowarudishia ubinaadam watu hawa(uzalendo).hamna mzalendo nchi hii.

Polisi ni chombo muhimu kinachoweza kukupa taswira halisi ya muenendo wa taifa.
Ndio maana hata picha zilizozagaa mtandaoni juzi zinaweza kuwa ndio picha zilizoenea kwa kasi na kujadiliwa zaidi kuliko picha nyingine,kuonyesha kuwa watu wako senstive sana na ile uniform.

My take, polisi ni miongoni mwa wahuni wengi nchi hii.wanawakulisha.
 
Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu nzuri.. "Liars must have a good memory"

Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya kuuawa kwa kijana Yahaya Omary mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu Arusha. Polisi wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mguuni na kwenye ---- alipokua akijaribu kukimbia.

Lakini picha ya marehemu iliyoonekana baadae inaonesha kupigwa risasi ya tumbo. Sasa kwanini Polisi wamedanganya ni mguu na ----?? Wanataka kuficha nini?

Bila shaka Polisi walidhani picha ya mtuhumiwa akiwa kauawa haitaonekana.. hivyo wakaamua kudanganya ili kuhalalisha mauaji. Lakini hatimaye picha imeonekana akiwa kapigwa risasi ya tumbo, Polisi wameumbuka.

Pili, hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma si tumboni.

Lakini hii si mara ya kwanza jeshi la Polisi kuingia kwenye tuhuma za kuua watu wasio na hatia na kushindwa 'kujustify' mauaji hayo.

Mwaka 2006 aliyekua kaimu RPC wa mkoa wa Dar, Bw.Abdalah Zombe aliorganize mauaji ya wafanya biashara wa madini kutoka Mahenge Morogoro na kusingizia ni majambazi. Akafika mbali zaidi na kudai walikua wanarushiana risasi na Polisi.!

Lakini ripoti ya Tume ya Jaji Kipenka ikawaumbua Polisi maana ripoti ilionesha watuhumiwa wote walikua wamepigwa risasi visogoni. Ikabainika pia si kweli kuwa walikua wakirushiana risasi na polisi.

Huwezi kurushiana risasi na Polisi then upigwe risasi kisogoni.. Jaji Kipenka akawaumbua Polisi kwa kueleza kuwa wafanyabiashara wale walifungwa kamba mikono na miguu, kisha wakafungwa vitambaa vyeusi machoni ndipo wakapigwa risasi.

Halafu baada ya kuhakikisha wameuawa Polisi wakawapora jumla ya sh. mili.200 na madini waliyokua nayo. Kisha Zombe akaita mkutano na waandishi wa habari akasema kuna majambazi yameuawa yakijaribu kurushiana risasi na Polisi.

Ukatili, ukatili, ukatili wa kiwango cha kutisha. Yani uwakamate watu wasio na hatia, uwafunge vitambaa usoni, uwapige risasi, kisha uwapore mali na fedha walizonazo.. halafu bado uwasingizie ujambazi.. Kwa kweli Mungu wetu ni wa huruma sana lakini hii dhambi sijui kama inasameheka.

Mazingira ya kuuawa kwa wafanyabiashara wale yanafanana na mazingira ya kuuawa kwa kijana Yahya Omary anayedaiwa kulipua mabomu Arusha.

Kwanza inadaiwa alikua anakimbia, lakini risasi kapigwa tumboni. How comes? Mtu anayekimbia tulitegemea apigwe risasi mgongoni au maeneo ya nyuma ya mwili lakini si tumboni. Huu ni uongo wa kitoto kabisa.!

Polisi wanadai eti mtuhumiwa alikua mcheza karate na judo, hivyo alitumia mbinu zake za karate ili kuwakimbia Polisi.

Cha ajabu mtuhumiwa alikua hajafungwa Pingu mikononi wala miguuni. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo" halafu umsafirishe bila kumfunga pingu? Hizi ni hekaya za Abunuasi.!

Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu?? Uongo wa kitoto kabisa huu.!

Nashauri Rais Kikwete aunde tume kuchunguza mauaji ya kijana huyu kama alivyounda Tume ya Jaji Kipenka kuchunguza mauaji ya wale wafanya biashara wa Mahenge. Huenda kijana huyu ameuawa ili kupoteza ushahidi.!

Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.

Nimeona vyombo vingi vya habari vikiandika habari hii kwa ushabiki. Vingi vimeonesha kufurahishwa na mauaji ya kijana huyu. Gazeti moja limeandika "ALIYELIPUA MABOMU ARUSHA AUAWA".

Hili gazeti sijui kama lina Mhariri, maana hii si habari. Huwezi kusema "aliyelipua mabomu arusha..." wakati haijadhibitika kama ni kweli alihusika au lah.!

Yahaya alikua mtuhumiwa tu na angefikishwa mahakamani ukweli ndio ungejulikana. Huenda si yeye aliyehusika na mabomu na labda hata hajui lolote kuhusu mabomu.. Labda Yahaya alikua na ugomvi na kiongozi wa serikali ndo akaamua kumbambikia hii kesi.

Na chombo pekee cha kusema ukweli ni mahakama.. Lakini serikali kwa kujua kesi ikienda mahakamani wataumbuka na itajulikana Yahaya hakuhusika na mabomu ya Arusha wakaamua kukatisha maisha.

Wakamuua kikatili kabla kesi haijaenda mahakamani. Wawakamsingizia eti alijaribu kukimbia. Kivipi alijaribu kukimbia wakati kapigwa risasi ya tumbo.?

Lakini magazeti yamemhukumu.. yamemuita muuaji.. mrusha mabomu.. mengine yamemuita jambazi sugu..

Nayaogopa magazeti ya Tanzania. Ni magazeti hayahaya yaliyowahukumu wale wafanyabiashara wa Mahenge waliouawa na Polisi wa Zombe. Magezeti yakaandika "MAJAMBAZI KUTOKA MORO YAUAWA DAR."

Lakini ilipokuja kubainika hawakua majambazi magazeti hayohayo yakaandika "KASHFA NZITO JESHI LA POLISI; WADAIWA KUUA RAIA WASIO NA HATIA NA KUWABAMBIKIZIA KESI YA UJAMBAZI"

R.I.P Yahaya Omary, binafsi siwezi kukuhukumu kama magazeti yanavyofanya, maana sijui kama ni kweli ulihusika na mabomu ya Arusha au lah.

Labda mahakama ingeweza kutuambia ukweli.. lakini kwa kuwa umetangulia MUNGU pekee ndio anajua ukweli.

Pumzika kwa amani Yahaya.. Hata waliokuua ipo siku nao watakufuata. Duniani sote tunapita.. hakuna atakayeishi milele.. ipo siku ukweli utafahamika na itakuwa kilio na kusaga meno kwa wote walioshiriki mauaji haya ya kinyama dhidi yako.!

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.!

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!

attachment.php
 

Attachments

  • 1413889156215.jpg
    1413889156215.jpg
    38.3 KB · Views: 494




Nchi hii ni ya watanzani wote

Kaka kwa baadhi ya wanaCCM na watawala wetu TANZANIA ni ya CCM tu wengine ni wapangaji tu.Na ndiyo maana walipouawa watu ARUSHA hakuna alisyejali kwani waliokufa ni wa KASKAZINI na ni wanachama wa CHADEMA upo?Hebu fikiria wangekuwa wanachama wa CCM unadhani kesi ingeishia hapo?
 
Bora IS inayopigana huko Syria kuliko jeshi la polisi la Tanzania ambalo kazi kubwa ni kusema uongo
 
jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. wizi wa epa, dowans, kagoda, meremeta, tangold nk.;
  2. sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
je nini imani yako kwa jeshi la polisi?


hapana hapana hapana hapana kabisa hapana.
 
TATIZO LA POLISI halipo kwa polisi, ni mfumo wa utawala ukiwa na wazo moja tu, kandamiza aina yoyote ya upinzani! Maandamano uchina ya hongkong yana muda sasa, lakini kazi ya polisi ni kuwalinda wote
 
Malisa Godlisten umeandika kwa uchungu sana...binafsi imeniuma...tena sana!!! Daaahh kwanini hawa binadam wenzangu wamekua hivi???? Ivi kazi yao ni kulinda usalama ama kuhatarisha amani???

Hapa mtaani kuna kituo cha polisi yan kila nikikatiza nahis kama sina aman kabisa!! Sielew kwanin sina imani nao hawa viumbe??? Inaniuma sana...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom