Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi siliamini kabisa kwa hiyo weka 0%Ndugu wanaJF, Naomba maoni yenu juu ya imani yenu kwa jeshi la polisi kuhusu utendaji kazi wake na mahusiano yake na jamii katika kudhibiti vitendo vya rushwa,uhalifu sambamba na kuzuia na kupambana na hali zote zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Lengo la kuomba maoni yako ni kunisaidia mimi kwenye kuandaa matokeo kutokana na utafiti mdogo ninaofanya kuhusu "MAHUSIANO BAINA YA VYOMBO VYA DOLA NA RAIA KATIKA KUSIMAMIA HAKI" Tayari nimekusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mahakama na magereza. Niambie unaliamini jeshi la polisi kwa asilimia ngapi? 100%, 90%, 80%, 70%, 60%, 50%, 40%, 30%, 20%, 10% au 0% Naomba umakini (seriousness) uzingatiwe katika kujibu. Karibuni