Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?
- Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
- Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
- Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
- Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
- Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
- Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Mkuu mbona imani yangu kwa hawa viumbe hai wenzangu ishatoweka toka long taimu?