Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111
Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
  2. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?

Mkuu mbona imani yangu kwa hawa viumbe hai wenzangu ishatoweka toka long taimu?
 
Sina pa kuanzia kuwaamini, leave alone kuwaamini kwenyewe... Hawa wanaobambikia kesi ya kichwa cha mtu ili wapate rushwa, hawa wanaosafirisha bangi kwa gari ya polisi halafu wanatoroshana niwaamini..!!?? we moshingi sijui unapata wapi ujasiri wa kuwateta kwenye post yako namba 13...
Cheki hapa...
- walimuua Kombe..
- Walimuua Mwangosi.....
- Walitaka kumuua Mwakyembe.......
- Walimbambikia mfanyabiashara kichwa cha mtu kutaka wapewe rushwa.......... Na sijui hicho kichwa walimuua nani
- Waliwauwa wafanyabiashara wa Madini toka mahenge
- POLISI WAUA MTOTO WA MIAKA 9 KWA RISASI TARIME ~ Shommi B
- POLISI WAUA RAIA WANNE NA WAJERUHI-SONGEA | Sundayshomari's Blog
- Mkally Blog: Power of Information: Polisi waua Raia Dar
- ZANZIBAR NI KWETU: POLISI WAUA RAIA TENA!!!
- Polisi ilimuua fundi Pikipiki ngara
- Polisi wakamatana wakisafirisha bangi
- Watumishi wa serikali, polisi watajwa kuwa wezi wakubwa wa dawa

Na mengine mengi
 
kwakweli mie imani na polisi iliisha kitambo sana
wapo kifedha zaidi bora liwe tu shirika la biashara linalopata faida
polisi hawalindi na hawana uchungu na wanaichi sie wa kawaida
polisi wanawabeba sana watoa pesa (matajiri) kwa ufupi wanaume suruale/wanawake ovyo
polisi wanafanya kazi kwa hisia na visasi na nguvu za ziada

ingawa nina rafiki polisi LOL
 
Hivi Chagonja ni askari wa kusomea au ndiyo wale makanjanja?!
 
Nawaamini na kuwakubali coz bila wao tusingepata muda wa kukaa katika mitandao na kuanza kujadili mada mbali mbali chukulia mfano Darfuu, kongo watu hawana utulivu kama tulionao sisi hii kutokana na kazi za vyombo vya dola najua mtaviponda lakini ukweli utabaki palepale vyombo vya dola vyote vinafanya kazi kubwa na vinastahili pongezi. hongera Polisi TZ, hongeara JW, magereza, uhamiaji mahakama endeleeni kuwabana wavunja sheria mwanzo mwisho msirudishwe nyuma na maneno maneno kwani hayana msaada katika ulinzi na usalama wa TZ.
 
Nimekaa nikatafakari sana kuhusu jeshi letu la polisi na matukio ya kinyama na mabaya kwa jamii yanayoripotiwa kuwahusisha. kwa matukio haya machache ninayoyajua mimi na kuyasikia nipe sababu ya mtanzania kuliamini jeshi la polisi
  1. pasaka walimteka mfanyabiashara kwa defender magomeni akitoka kwenye biashara zake jino akiwa mauzo yake sh.15,000,000/= wakamzungusha kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa mbili wakamtupa mburahati wakiwa wamemfunga kitambaa kuziba macho na kutokomea na hela zake. mpaka leo hakuna aliyekamatwa
  2. Mauwaji ya kinyama ya mwandishi wa habari mwangosi
  3. juzi tu polisi wa pikipiki (TIGO) wamekwapua mkoba wa mama aliyetoka benki ya CRDB mikocheni na kukimbia na pikipiki na baadae kuanguka kwenye mtaro kisha kukimbia tena wakasahau bunduki iliyowezesha kupata kidhibitisho
  4. nilikuwa mwanza siku moja hotelini wakakamata mwizi askari wameitwa kuja kumchukua wanataka walipwe

najua yake mengine mengi ambayo na nyinyi mtayaongezea hapo ila kwa kweli imani na jeshi la polisi imepotea kabisa kiasi kwamba hata kama umevamiwa unaogopa kuwapigia coz hawatakuwa msaada wowote badala yake watakutoa chochote.

my take: Jeshi letu linaitaji restructuring kwani tunakoelekea sio kuzuri.
 
Ndugu wanaJF, Naomba maoni yenu juu ya imani yenu kwa jeshi la polisi kuhusu utendaji kazi wake na mahusiano yake na jamii katika kudhibiti vitendo vya rushwa,uhalifu sambamba na kuzuia na kupambana na hali zote zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Lengo la kuomba maoni yako ni kunisaidia mimi kwenye kuandaa matokeo kutokana na utafiti mdogo ninaofanya kuhusu "MAHUSIANO BAINA YA VYOMBO VYA DOLA NA RAIA KATIKA KUSIMAMIA HAKI" Tayari nimekusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mahakama na magereza. Niambie unaliamini jeshi la polisi kwa asilimia ngapi? 100%, 90%, 80%, 70%, 60%, 50%, 40%, 30%, 20%, 10% au 0% Naomba umakini (seriousness) uzingatiwe katika kujibu. Karibuni
 
20% waaminifu kwa kazi yao (they are ethical), 30% wanatii wanachoagizwa (kwa kulazimishwa) na 50% wala rushwa, policcm,majambazi wauawaji..THEN 20% ni imani yangu...
 
jeshi la polisi kwasasa limejikita zaidi kwenye siasa na kujisahau kwamba wajibu wao ni wakuwalinda raia na malizao nguvu wanayo tumia kwenye sisi imekua kubwa sana ukilinganisha na nguvu wanayo tumia kuwalinda raia na malizao? vitendo vya uhalifu vimezidi kuogezeka kila kukicha kutoka na jeshi letu kutumiwa zaidi na wanasiasa kwahiyo sina imani hata kidogo(0%)
 
Deshmo; abdul 28; na Mzalendo 80 naombeni maoni yenu mnaliamini jeshi la polisi kwa asilimia ngapi maana mfano, ukiniambia wanalinda magaidi nashindwa kujua hapo ni grade asilimia ngapi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom