Ni muda mrefu sasa tangu kuwe na malalamiko mbalimbali kutoka kwa raia wa nchi hii juu ya utendaji na uadilifu wa jeshi la polisi. Jeshi la polisi limekuwa likituhumiwa kwa mambo mengi sana kama vile RUSHWA, UKANDMIZAJI WA HAKI ZA RAIA, KUSINGIZIA KESI, KUUA RAIA BILA HATIA na KUSHABIKIA SIASA kinyume na maadili ya jeshi hilo.Tuna mifano mingi sana ya ukiukwaji wao wa sheria na maadili yao ya kazi wenzetu hawa, ikiwa ni pamoja na ile ya jumla ambayo imeweza kuripotiwa na vyombo vya habari vya ndani na nchi na mifano mingine ikiwa hairipotiwi hata kwenye vyombo vya habari lakini tukiyaona, yakitutokea kwetu au kwa ndugu au jamaa zetu.
Kwa mfano, ndani ya mwaka huu pekee, jeshi la polisi limelalamikiwa kwa mambo makubwa katika maeneo mbalimbali kama vile, Mauaji yaa raia aliyesemekana alikuwa anauza magazeti wakati wa maandamano ya CHADEMA kule morogoro, mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, kashfa ya Babarini Dar. mauaji ya wamachinga mwanza, Rushwa, na sakata lingine la ngara.
Lakini lilonisukuma ni hili jipya kabisa la majuzi kariakoo ambapo majambazi walivamia gari lililokuwa na watu waliokuwa wakipeleka fedha benki kiasi cha shlilng. milioni 150, ambapo jambazi mmoja alikamtwa aliwa na majeraha kidogo lakin jana tunaambiwa kafariki, na kwa mujibu wa raia walioshuhudia tukio wanadai kuwa kifurushi cha pesa kilidondoshwa chini na askari mmoja mnene alikiokota na kukiweka kwenye gari la polisi ambalo kwa wakati huo raia wanasema hawakutilia maanani kunukuu namba zake.Cha ajabu hadi sasa tunaambiwa zile pesa polisi hawajui zilipo.
Swala hili linaibua maswali mengi, na habari za chinichini zinadai kuwa polisi walienda kujawana pesa hizo maeneo ya jangwani, kwa haya na mengine mengi je polisi kwa nini sisi raia tuendelee kuwaamini? Je yule jambazi ambaye tulimuona akiwa na majeraha kidogo haiwezekani ikawa nyie mlimpe mateso makali ili afariki na kupoteza ushahidi wa ni wapi hasa pesa zimekwenda?
Na imekuwa ni kwaida kwa viongozi wa jeshi hilo kukanusha ukweli wa mambo na kuwa na ripoti za uongo, kaa mkijua haiwezi tokea ukweli ukashiundwa kwa uongo japo hata kama itachukua muda, imefika mahala imjisafishe raia tuanze kuwaamini tena, hebu fikiria raia waliojitokeza kupambana na majambazi wale halafu manafanya uhuni huu je tuendelee kuwapa ushirikiano, kiufupi polisi wamegeuka majambazi, wapolaji hata ukikamatwa na kitu chako wakaenda polisi kukifanyia uchunguzi hata ukupeleka ushahidi kudhibitisha umiliki wako wakikipenda kitu hicho utakiacha tu!