Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111
amani iliyopo ni woga tu wa watz polisi hawafai hata kupewa hata 0%. May be -20%. Kila kitu kwao ni siasa tu wakingojea kukingiwa kifua na akina lukuvi & co. Polisi gani aweze kulenga shabaha kwa mtu anayemkimbiza muuaji lakini asiweze hata kumvunja miguu huyo muuaji? Uongo mwingine wahitaji kuupima kabla. Wanangojea kupiga tuu. Huko ccp mlifundishwa kupiga tuu?
 
Mimi imani yangu kwao ni sifuri. Nikiwaona naona nipo hatarini zaidi kuliko wasipokuwepo. Tutawaamini vipi wauaji? Kazi waliyopewa na bosi wao ni kupiga na kuua kisha kusingizia raia kuwa wmerusha kitu chenye ncha kali. Hivi polisi wakimuhoji mtu mpaka akafa wataaminika?!

Umenichekesha sana bana. Hata mimi ni hivyo hivyo
 
Kiukweli jeshi letu siyo tu kwamba limekosa heshima bali limebadilishwa kuwa taasisi ya watu binafsi(ccm)ili kulinda maslahi yao na kuwasahau watanzania.mimi binafsi nina imani ya asilimia 0 na jeshi la polisi
 
Ndugu wanaJF,
Naomba maoni yenu juu ya imani yenu kwa jeshi la
polisi kuhusu utendaji kazi wake na mahusiano yake na jamii katika
kudhibiti vitendo vya rushwa,uhalifu sambamba na kuzuia na kupambana na
hali zote zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani.
Lengo la kuomba maoni
yako ni kunisaidia mimi kwenye kuandaa matokeo kutokana na utafiti mdogo
ninaofanya kuhusu "MAHUSIANO BAINA YA VYOMBO VYA DOLA NA RAIA KATIKA
KUSIMAMIA HAKI"
Tayari nimekusanya maoni kutoka kwa wadau
mbalimbali na wananchi kuhusu mahakama na magereza.
Niambie unaliamini jeshi la polisi kwa asilimia ngapi?
100%, 90%, 80%, 70%, 60%, 50%, 40%, 30%, 20%, 10% au 0%
Naomba
umakini (seriousness) uzingatiwe katika kujibu.
Karibuni

Kwa 7bu ya wazalendo wachache sana waliopo imani yangu kwao ni 15%
 
Napendekeza iwekwe poll kwa ajili ya hii topic. Kama mleta maada hujui namna ya kutengeneza muombe mods akusaidie. Wasiliana na Paw.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanaJF, Naomba maoni yenu juu ya imani yenu kwa jeshi la polisi kuhusu utendaji kazi wake na mahusiano yake na jamii katika kudhibiti vitendo vya rushwa,uhalifu sambamba na kuzuia na kupambana na hali zote zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Lengo la kuomba maoni yako ni kunisaidia mimi kwenye kuandaa matokeo kutokana na utafiti mdogo ninaofanya kuhusu "MAHUSIANO BAINA YA VYOMBO VYA DOLA NA RAIA KATIKA KUSIMAMIA HAKI" Tayari nimekusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mahakama na magereza. Niambie unaliamini jeshi la polisi kwa asilimia ngapi? 100%, 90%, 80%, 70%, 60%, 50%, 40%, 30%, 20%, 10% au 0% Naomba umakini (seriousness) uzingatiwe katika kujibu. Karibuni

30% tuuu
 
10% kiutendaji, kimahusiano, kimbinu, na kwa kweli linafanya siasa za chama cha mapinduzi. sina hata punje ya shaka kuwa ni jeshi la chama tawala kukisaidia chama tawala kuendelea kuwepo madarakani.

Si wa kweli, wanachonganisha wananchi maana upelekapo taarifa za uhalifu wanamwambia mhalifu nani amekuja kuwapa taarifa hizo. Halishughuliki na matatizo ya wananchi ila linashughulika na ulinzi wa viongozi...kwa ufupi ni jeshi la viongozi walioko madarakani.
suala la rushwa hapo ndiyo kitovu chake. angalia traffic anakukamata kwa makosa yasiyoweza kusababisha tatizo lolote lakini makosa hasa hawashughuliki nayo. Ni traffic wa daladala maana wanapata chochote huko. Hawana mpango na kusimamia sheria za usalama wa barabarani zaidi ya magari...ukiwatazama usoni kama binadamu vile lakini simuoni binadamu ndani yao.
Ukienda vituo vya polisi huko ndiko vioski vya wakubwa...wanakusanya tu fedha
viongozi wake ...mfano Mwema, anaonyesha wazi yuko kwa maslahi ya Ikulu na ccm. Kova kauli zake ni za kilaghai...anatengeneza mood ya kutaka kuwaaminisha watz kuwa jeshi linafanya kazi tusiyoiona...press conferences zake anatumia nguvu nyingi kuelezea mambo madogo
Nalichukia jeshi la polisi 100%
 
ndugu wanajf, naomba maoni yenu juu ya imani yenu kwa jeshi la polisi kuhusu utendaji kazi wake na mahusiano yake na jamii katika kudhibiti vitendo vya rushwa,uhalifu sambamba na kuzuia na kupambana na hali zote zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Lengo la kuomba maoni yako ni kunisaidia mimi kwenye kuandaa matokeo kutokana na utafiti mdogo ninaofanya kuhusu "mahusiano baina ya vyombo vya dola na raia katika kusimamia haki" tayari nimekusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mahakama na magereza. Niambie unaliamini jeshi la polisi kwa asilimia ngapi? 100%, 90%, 80%, 70%, 60%, 50%, 40%, 30%, 20%, 10% au 0% naomba umakini (seriousness) uzingatiwe katika kujibu. Karibuni

0% sina imani kabisa(vijana wanatumia bangi sana)
 
Policcm sio polisi tena maana mpumbavu ndio anatoa amri ya kupiga badala ya wataalamu wa polisi.....ccm imeliharibu sana
 
Sina imani na jeshila polis hata mahakama zao pia
 
70 asilimia utendaji mzuri.10 asilimia utendaji mbovu.20 asilimia wananchi uwezeshaji mdogo na fikra hasi za kupandikizwa na wanasiasa .
 
Back
Top Bottom