Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
- Thread starter
- #21
SwadaktaHilo nimekuwa nikilisema sana bahati mbaya watu wamekuwa waki catch feelings wakidhani namkosea adabu Nyerere.
Nyerere ni legend hilo wote tunalikubali lakini mapito yake ya harakati hayakuwa na vizingiti vigumu kama tunavyoona utawala wa miaka hii.
Utawala wa kikoloni kuna namna ulikuwa na hali ya kuthamini utu. Hiyo kwa utawala wa sasa haipo.
Katika mapambano ya Nyerere hakuwahi kupigwa mabomu, hakuwahi kuwekwa jela na kubwa zaidi hayajui maumivu ya risasi.
Wafuasi waliokuwa wakimuunga mkono Nyerere hawakuwa victims wa kutekwa, kuuwawa wala kupotezwa.
Labda mnisahihishe leo kwa kunitajia fulani na fulani waliowahi kutekwa, kuuawa au kupotezwa maybe I got it wrong.
Miaka ya sasa kuna wanasiasa wengi walitaka kutuongopea kwamba kuwa na roho ngumu kama Lissu ni jambo rahisi.
Walikuwa wanajaribu kutunisha muscles kuonesha nao wana balls kama za Lissu lakini mwisho wa siku the last man standing amebakiwa kuwa Lissu.
Utawala wa sasa una approach 3 za kudili na wapigania demokrasia. Ukiwa mtu mwenye ushawishi sana kwa jamii watakuja na approach ya rushwa.
Kipengele hiki cha rushwa kimepita na wanasiasa wengi sana ambao huko nyuma wananchi waliwahi kuamini kama wawakilishi sahihi wa sauti zao.
Lakini kama mwanasiasa au mwana harakati hana ushawishi mkubwa kwa wananchi huwa anapewa onyo la kitisho aache mara moja kutingisha hiyo meza.
Asipofanya hilo ndio hapo jina la wasiojulikana linapoanza kutajwa kwenye whereabout yake.
Lissu kapitia mateso makubwa pengine hata waliowahi kuonja kifo wakifufuliwa leo wanaweza kutoa ushuhuda "wakati tunakufa hatukuwahi kupata maumivu ambayo amepata"
Mazingira haya katika kipindi cha harakati za Nyerere hayakuwepo kabisa.