Je unadhani Tundu Lissu ni Zaidi ya Julius Nyerere?

Kazi ipo
 
Kwahiyo unataka tumlinganishe tundu lissu na huto tutako twako kama skonzi na tuna ukurutu sugu usiokoma hata kwa dawa gani
Kumbe unaumwa kiasi hicho na inahitaji dawa? Nenda kanunue mafuta na maji ya Mwamposa! Utapona haraka sana huo ukurutu!
 

..watawala kuuwa wapinzani wao sio sawa.

..Na watawala wakishaonja damu huwa hawaachi.

..watawala wakishauwa tu, lazima watalazimika kujilinda.

..Na mara nyingi watawala kujilinda hulazimika kuuwa mara kwa mara.

..Msidhani utawala wa Mama Abduli ataacha kuuwa.

..Kuna wanaoamini maridhiano ni pamoja na kumshawishi Mama Abduli na genge lake kuwa watakuwa salama pamoja na mauaji wanayohusishwa nayo.
 
Tanganyika haikuwa koloni la nchi yoyote ile wakati tunapata Uhuru mwaka 1961, mwaka 1960 Tanganyika ilipata Madaraka(mock), hii ilitolewa na UNO ambayo ndiyo iliimiliki Tanganyika na kuikabidhi kwa Uingereza kama mlezi na si mtawala ndiyo sababu Nyerere alikuwa anakwenda UNO kujieleza(kuomba Uhuru) kwani sharti la UNO lilikuwa kuona tuna elimu ya kutosha kuweza kujiongoza kama nchi mpaka pale UNO iliporidhika kuwa angalau tunaweza kujiongoza wenyewe hata hivyo nafasi za juu serikalini ziliendelea kuwa chini ya waingereza na kupunguzwa taratibu kulingana na ujuzi, hivyo kusema Nyerere alipambana na wakoloni weupe ni kujipamba vinginevyo tusingekuwa kama tulivyo maiti, alijisemea mzee jomo Kenyatta.
 
kwa nini huwa unapata aleji usomapo Tundu Lissu? hujui siasa wewe
mbona unakasirikia maoni yangu huru gentleman?

si utoe maoni yako huru jukwaani kwa amani tu bila makasiriko dhidi ya maoni ya wengine na itapendeza zaidi?🐒
 
Nyerere yupi sasa? Kama ni Nyerere mpigania Uhuru basi Tundu Lissu ni zaidi yake. Ingawa wote waliwahi kushitakiwa kwa uhaini

Tundu Lissu anatakiwa kufananishwa na akina Jomo Kenyatta, siyo Nyerere
 
Tundu Lissu ni zaidi. Nyerere hakuwahi kupigwa risasi hata moja na wakoloni weupe. Tundu Lissu ana risasi mwilini aliyopigwa na wakoloni weusi.

Concludion: Lissu ni zaidi ya Nyerere.
 
Joyce Mukya katika ubora wako
 
Kutekwa kwa raia nchi hii hakujaanza wakati wa Magufuli, umezaliwa lini kijana?
 
Sifa ulizokuwa ukimmiminia msaliti Mbowe mpaka watu wakaanza kudhani kuwa wewe ni mke wa Mbowe naona umezihamishia kwa Lissu. Wewe na Mwashambwa hamna tofauti - wote machawa tu!
 
Nyerere alikosea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…