Hakuna aliyejibu hata moja zaid ya kuleta porojo za Kidini. Welete maswali nasubiri majibu sitaki ushabiki
Naomba nikujibu Kama ifuatavyo:
Swali la kwanza, UNO Resolution 181(II) la 1947 tarehe 29th November Tukio lililofanyika lilikuwa linahusu nini?
JIBU: Haya yalikuwa ni maazimio ya Umoja wa Mataifa kuigawanya Palestina kuwa na Dola mbili ya Palestina na Israel. Pia kwenye maazimio hayo, Jerusalem ilibakia kuwa eneo lisilo kuwa na mwenyewe na lilitakiwa kuwa Chini ya usamamizi wa Umoja wa Mataifa. Israel waliiheshimu maazimio haya na kuijitangazia uhuru mwaka 1948. So kwa hapa Israel walikuwa wanatekeleza sheria halali ya maazimio ya Umoja wa Mataifa. Shida ni kwamba baadala ya waarabu au wapalestina kuanzisha taifa lao, wao wakaanzisha Palestinian war dhidi ya Israel.
Swali la pili, 14th may 1948 kulitokea Tukio gani?
JIBU: mwaka 1948 yalitokea matukio mengi ila nitataja manne.
La Kwanza, ni tukio la Israel kuijitangazia uhuru wake mwaka 1948 Mwezi wa tano siku ya tarehe 14. Hii ikiwa ni kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 1947.
La pili, ni tukio la Palestinian war au Vita vya Palestina. Hii ilasababishwa na azimio namba 181 la umoja wa Mataifa kuigawanya Palestina kuwa na nchi mbili, na Israel kukotangazia uhuru wake.ambapo waarabu hawakutaka kabisa, hivyo vikundi vya kipalestina na waarabu vikaanza kupigana na Israel na vikundi vya kiyahudi.
La tatu, Ni Nakba, baada ya vikundi vya Palestina waarabu kuwachokoza wayahudi, ndipo walipopigwa kusukumizwa pembeni, na kuleta kitu kinaitwa Nakba.
La nne , ni vita vya Israel na Mataifa ya kiarabu. Kipindi hicho yakijulokana Kama United Arab Republic, Misri, Jordan na Syria wakisaidiwa na Saudi Arabia. Hivi vita ndivyo vilipelekea mzozo tunaouona Leo, baada ya kichapo, Israel ikachukua baadhi ya maeneo ya Misri na Jordan amabyo ni Gaza na Jordan. kwani iliwashinda kwenye vita.
Kuhusu swali la tatu kwamba 1950s Israel na MAREKANI kwanini walianzisha neno UGAIDI na MAGAIDI?
JIBU: Fahamu kwamba neno gaidi au Terrorism halikianzishwa na Marekani. Neno terrorism lilianza kutumika mwaka 1793 wakati wa mapinduzi ya ufaransa Yani French Revolution na neno Hilo lilitumika kutokana na ukatili wa serikali mpya ya kuwaua kwa kunyongwa watu waliokuwa wakidhaniwa kuwa wanaopinga mapinduzi hayo. Na lilianza kutumika kwenye kamusi mwaka 1840.
Swali la mwisho UKATIRI, UBAGUZI, MAUAJI , UBOMOAJI MAKAZI ,NA UKOLONI WA KUTUMIA JESHI uliofanyika Kuanzia 1948 Hadi leo??
JIBU: Nadhani Kama Palestina nao wangetangaza uhuru wao Kama Israel mwaka 1948, na kuacha kuwavamia waisraeli na kuanzisha vita ya Palestina , wasingepigwa na kivurumushqa maana Israel iliona ikiwaachia Hawa watawasumbua. Ile Nakba ni kisingizio tu lakini uchokozi aliuanza Palestina.