Je, unakubali ndoa au unakataa?

Je, unakubali ndoa au unakataa?

Je ni MSHANA JR au ROBERT HERIEL?


  • Total voters
    136
Wakubwa shikamoni kuna debate inaendelea hapa jamii Forum baina ya team mbili
1) KATAA NDOA
2)KUBALI NDOA

Kwa upande kataa ndoa muwakilishi
ROBERT HERIEL aliandika uzi huu

"Hakuna umuhimu wa ndoa karne hii kwa sababu hizi"​


Kwa upande wa kubali ndoa ni MSHANA JR
Kaandika uzi huu

"Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa"​

Víp? Ambao hawajaingia kwenye hizo ndoa tunaluhusa ya kushaur chochote hapo au wengine ni kupost maoni tu pasipo kufikilia
 
Hii ishu ya kushinda ukitafuta mtu sahihi wakati Satan yupo road ni uongo ipo siku atamfikia tu. Pick any akijifaragua weka yeye chini pick anaza
Hapana, inategemea unamtafutaje huyo Mtu sahihi

Ukimwomba Mungu na kutulia hakika unampata Mtu atakayekuwa Baraka kwako na sio Mwiba, hatakuwa Mkamilifu at 100% lakini hatakusumbua na atakutii

Amini hilo.
 
Bwana wa majeshi bariki neno lako. Neno lako ni la kweli na linadumu milele
1 Timotheo 4

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3 wakiwazuia watu wasioe,
Jesus!. Ikabidi nikasome hilo neno kujihakikishia. Kumbe yalishatabiriwa. Mungu tusaidie
 
Hapana, inategemea unamtafutaje huyo Mtu sahihi

Ukimwomba Mungu na kutulia hakika unampata Mtu atakayekuwa Baraka kwako na sio Mwiba, hatakuwa Mkamilifu at 100% lakini hatakusumbua na atakutii

Amini hilo.
Shida ni kwamba Mungu Hakuletei Umekaa Unatafuta mwenyewe.
 
Sasa kweli issue ya kutungisha mimba ba ndoa wapi na wapi ndugu? Ndoa ni Ngono ilionoga tu hamna Cha Maana.
Lini mliacha kuwasimanga ni single mothers. Sasa nao wanaamua kua nyie mnakataa ndoa na wao wanakataa kuzaa ni kula ujana tu. Dunia mnayotaka iwe itakua ya hovyo sana.
 
Robert Heriel is a Misogynist Racist Twaat.

Huwezi kumuweka Haramia na kumfananisha au kumlinganisha na Mtanzania/Mwafrika au mwanasayansi yeyote yule ambaye amejikita katika masuala ya Jamii.

Robert Heriel haijali Tanzania, hajali Jamii na wala sio mtu wa Kweli. Wekeni C.V yake Leteni picha zake.

Hakuna Tapeli mkubwa ambaye ameshatokea kama huyo mdudu.

Hao wanaojifanya wanajadiliana ni midubwasha yake tu, wengine wanaingia kichwa kichwa.
Kikubwa yeye huwa anaacha ujumbe kafiir(usioe n.k)basi. mengine ni makele tu yakukupumbaza ....Yaani meseji zake sio za kujadiliana ikitoka imetoka. Mada peke yake ndio meseji zake.

Angalieni nyuzi zake zinavyoanza....kati ya wapili au watatu lazima ataanza "nakukubali" au "Unasema ukweli mtupu" katikati unakuta mtu anamwekea "amebarikiwa"

Nakukubali, unasema ukweli mtupu na umebarikiwa ni sehemu moja yapo ya hadaa hiyo....kwenye mazingira kama ya humu unaingia kusoma chap chap ni rahisi kuingia mkenge! kwa maneno yake anasema "unasoma kikasuku"



Nani ambaye hajacheza upatu/mtaani? Lazima kunakuwa na matapeli watatu au zaidi. Mmoja anayechezesha, mmoja anaye kukuaminisha- kwa kupata hela n.k na mwingine wa kuzubaisha aidha kwa makelele n.k ili usione utapeli unavyofanyika.... ni genge!

kwenye uzi zake mpingaji(huyu ndie anakuwaga wa kuhadaa).Robert atajifanya anamuelimisha naye anafika sehemu anakubali na ndio hao wanaopewa likes... wewe mwenye hoja ambayo ni tofauti na anayotaka kamwe hakujibu badala yake...anakuja dubwasha lake....kwa wale matapeli wa mtaani huyu ndie anaegawana hela walizokwapua baadae

ukimpinga anajichekesha halafu anakuja dubwasha lake aidha kukutukana au kukuyumbisha na hoja zako, na nina wasiwasi hayo ma id mengine ni yeye!

Kwasababu majibu mengine yanakuwa kama vile amejisahau msomeni kwa uangalifu sana.

Kifupi huyu ni Tapeli wa hali ya Juu. Agenda yake ni kubwa. Yaani kinamna namna anataka kubadilisha mtazamo, fikra za 'mwafrika/mtanzania au kwa lugha nyingine kufanya maboresho. Ni hatari kwa Jamii. Ni sumu kwenye fikra.

Nilinena.
 
Back
Top Bottom