Je, unakubali ndoa au unakataa?

Je, unakubali ndoa au unakataa?

Je ni MSHANA JR au ROBERT HERIEL?


  • Total voters
    136
🤣🤣kwa kifupi unaenda kuwaomba wazazi wa mwanamke ruhusa wakupe mwanao are kula pesa zako
hahahahaha, na unalipa hao wazazi kumchukua mwanao, aje ale pesa zako

dunia haiishi maajabu
 
Kwa wanaume na wanawake. Hivi inakuaje kama ulilelewa na mama tu, na hujisikii vibaya yaan uko kwa Robert, nashauri usipitishe watoto Wako njia ambazo wewe ulipitia. Na kama ulilelewa na baba yaani ulikulia kwa bibi au ndugu wa baba, fikiria vitu ambayo ulikosa ili Mtoto/watoto wako wasikose.
Changamoto ambazo wazazi Wako wanapitia zisikutishe, kama umezalishwa au umeachwa jaribu kuangalia MTU mwingine usiweke chuki kwa kila me au ke, waza juu ya watoto zaidi.
 
Ndoa zilikua zamani sasa hivi ni utapeli tu, yaani nimlipie mahari pesa kibao binti aliyebikiriwa kwa chips mayai za buku jero.

Na bado aniletee jeuri mimi ninayemtunza kwa kila kitu, wakati wahuni walikua wanajipigia bila gharama.

KIJANA KATAA NDOA
 
Ni vizuri ungesoma nyuzi zote mbili ungegundua na yeye alikuwa na point
Wewe upo sahihi kwa mtazamo na fikra zako.
Nakuuliza tena umenielewa?
Pia wewe unamtafasiri kama hatred of, contempt for, or prejudice against women. It is a form of sexism that is used to keep women at a lower social status than men, thus maintaining the societal roles of patriarchy.
Hii ni sababu nyuzi zake nyingi zina mlengo unao fanana.
 
I've come across Mshana's comments,
He's about love, fairness, spirituality...I love him.

Robert is a male chauvinist, narcissistic, I try to avoid reading his contents hasa kuhusu mahusiano ili nisikwazike!!!
 
Ndoa ni muhimu Kwa wanaofuata mfumo wa zamani.
Ila ndoa Kwa upande wa pili, ndoa sio muhimu na sio lazima kuoa Kwa kizazi cha sasa kinachofuata mfumo wa Usasa.

Wanaokataa ndoa wanahoja za msingi na KUBWA.
Wanaokubali ndoa wanahoja lakini sio hoja nzito nzito
 
Ndoa ni muhimu Kwa wanaofuata mfumo wa zamani.
Ila ndoa Kwa upande wa pili, ndoa sio muhimu na sio lazima kuoa Kwa kizazi cha sasa kinachofuata mfumo wa Usasa.

Wanaokataa ndoa wanahoja za msingi na KUBWA.
Wanaokubali ndoa wanahoja lakini sio hoja nzito nzito
HUKOSEAGI
 
Ndoa ni muhimu Kwa wanaofuata mfumo wa zamani.
Ila ndoa Kwa upande wa pili, ndoa sio muhimu na sio lazima kuoa Kwa kizazi cha sasa kinachofuata mfumo wa Usasa.

Wanaokataa ndoa wanahoja za msingi na KUBWA.
Wanaokubali ndoa wanahoja lakini sio hoja nzito nzito
Hoja sio nzito kivip?

Better unakedefend upande tambua wengi wanalelewa na sio wapiga kelele na watunga stori.

Angalia poll mpaka dakika za mwisho utakuja gundua mko wachache sana na utoto ndo unawasumbua.
 
Wakubwa shikamoni kuna debate inaendelea hapa jamii Forum baina ya team mbili
1) KATAA NDOA
2)KUBALI NDOA

Kwa upande kataa ndoa muwakilishi
ROBERT HERIEL aliandika uzi huu

"Hakuna umuhimu wa ndoa karne hii kwa sababu hizi"​


Kwa upande wa kubali ndoa ni MSHANA JR
Kaandika uzi huu

"Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa"​

Haya mambo kwa mara ya kwanza wakubwa wa JF waliyaanzisha humu lakini WAKAINGIA MITINI NA KURA ZA WANANCHI ( YAANI KAMA VILE CCM INAVYOKIMBIA NA MABOX YA KURA )

Matokeo yake huwa siyo mepesi , msianzishe tu haya mambo , binafsi nilishtushwa sana kwa JF kuanzisha jambo lile , maana nilijua ngoma ile mwishoni itabuma .

Hakuna haja ya kushindanisha watu ambao hawagombei vyeo vya kisiasa
 
Back
Top Bottom