Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Naomba hii thread musiiondoe kwani inafurahisha na kukumbusha mambo ambayo leo hayapo. Pili najiuliza jkt ingekuwepo bado na huu ukimwi uliopo sijui ingekuwaje kwa wasomiwetu hawa.
 
Thread hii imenikumbusha mbali sana. Kipindi ambacho vijana wa kitanzania tulikutana,tukaishi pamoja,kwa shida na raha na kuliko yote kwa Upendo bila kujali dini,kabila,rangi na hadhi ya ww ni mtoto wa nani! Nlikua Operesheni Kambarage, 832KJ,1Ruvu, F.Coy! Siwezi msahau afande Sanga. Alipendwa ma Kombania nzima. Sijui yuko wapi siku hizi. Siku hizi kila nikiwa napita kwa gari hapo Ruvu darajani mpaka Mlandizi,upata hisia kali.
Mko wapi akina Alex Binde, Warioba, Mercy Fanuel, Anzameni, Urio na wengine wengi?
 
haaaa umeniamsha banaa.japo sijawahi kupata hayo maswaibu
lakini nakumbuka nilisoma kibosho girls kulikuwa kuna mambo
ya kimagumashi kama haya.by the way umenikumbusha machungu kimtindo:A S cry:
 
Nilikuwa makutupora kombania C. Siku ya kwanza tukaambiwa tutaenda disco nikafurahi kweli kuwa kumbe huku nako kuna disco. Nikashangaa usiku tunakalishwa chini tukafundishwa wimbo unasema hivi "Mwaka mmoja - amba- si mbali sana" Du siku ya kwanza halafu tunaambiwa si mbali sana!! Nilitamani kufa. Hapo mchana tumepokelewa kwa kurushwa vichura na walipojua tumetoka dsm ikawa balaa!! Bahati nzuri tulikuwa kama saba hivi wote tumetoka shule moja. Ila tuliienjoy baada ya kujua mazingira. Siku moja nilipewa adhabu ya kwenda kutafuta kuni na wenzangu. Tukaenda tukalala huko na kurudi jioni na mzigo mmoja tu wa kuni. Nilikuwa mtaalamu wa vitu vingi sana. Maisha ni mazuri sana ukiyachukulia jinsi yalivyokuwa. Maafande waonevu na wewe unatafuta mbinu tu ya kuwakwepa au unakuwa mjanja kuwapita. Unaishi vizuri tu.
 
Nilikuwa Makutupora Danger Coy wakati wa Canal Matingas. Nilikuwa nakula sehemu mbili 812 na makutu. Naanza 812 ujenzi narudi kumalizia makutu. Siku moja nikiwa 812 nikijulikana kama wa huko ikaitwa foleni bila kujua tukapelekwa madenge kupakua sementi, sikuweza kukataa kwasababu siri ingeifichuka, nilirudi makutu 6 usiku nikapambana na kibano cha kukosa disco siku iliyofuata nilikuwa taabani, nikakoma double share!

Siku nyingine nikapangwa kwa Dr Salim.A kurudi asubuhi nikakuta bogi limekatwa chita, duh bahati, nikapigwa bogi mbweni kwa captain mawazo. nilikuwa nakwenda mgulani kukiwa na magwaride.
Wimbo ninaoukumbuka, makutu mbali........, Kasimbago kaabuka.....
Lah nakumbuka ilikuwa raha. Mnakumbuka kichele! makutu upepo lazima uwe na kikopo cha rays kwenye kombati midomo isikauke ha ha ha.
 
Afande Justo wa OLJORO na mkwara wake wa KWATA....Pia shamba almaarufu DUNIA...unaangalia mraba wa kupalilia huoni mwisho........Kuchonga matofali toka mwamba laini kwa Mzee Shabaan.....Hakika ulikuwa mwaka wa aina yake...Pamoja na ukakamavu nilijifunza kuwaza haraka sana hasa katika kutengeneza UONGO kujiokoa kwenye mikono ya maafande pale ukutwapo usipotakiwa kuwa🙂

Hii ilikuwa mitaa ya afande Mlimba,Maduma, Masabo,Tyetyetye,Bahati,Bandeke.Mirudy,Chilumba aka Chiluba n.k..Kule kwenye shamba la dunia tumekula sana bisi kabla hujaja usawa wa gudulia.Week end mnachomokea Mirongo Inne kula konyagi mwitu na kuku wa kienyeji.Raha ajabu.
 
Nakumbuka Mafinga Kukatangazwa master parade ya CO Mlay. Basi watu wakakesha kufanya usafi wa kombati na kung'arisha boots na alfajiri kutandika vitanda na ndama unaikunja kama cassette. Kwenye Parade CO kaamrisha haya wote toa boots zenu, Duu acha tupate perfume za soksi.
 
Thread hii imenikumbusha mbali sana. Kipindi ambacho vijana wa kitanzania tulikutana,tukaishi pamoja,kwa shida na raha na kuliko yote kwa Upendo bila kujali dini,kabila,rangi na hadhi ya ww ni mtoto wa nani! Nlikua Operesheni Kambarage, 832KJ,1Ruvu, F.Coy! Siwezi msahau afande Sanga. Alipendwa ma Kombania nzima. Sijui yuko wapi siku hizi. Siku hizi kila nikiwa napita kwa gari hapo Ruvu darajani mpaka Mlandizi,upata hisia kali.
Mko wapi akina Alex Binde, Warioba, Mercy Fanuel, Anzameni, Urio na wengine wengi?

aisee tulikuwa wote Ruvu mwaka huo! nilikuwa danger coy na akina rodrick, gado, kapeya na wengineo. dah ilikuwa poa kishenzi. ila nakumbuka tukio la kusikitisha lilitokea kwenye coy yako F coy. siku yetu ya mwisho jeshini. umepigwa muziki mpaka (nadhani walikuwa JKT Kimbunga stereo enzi hizo) asubuhi. watu tukarudi kulala mida ya alfajiri. jamaa yenu mmoja, abraham maji alikuwa chakari. akalala huku akivuta fegi yake. kutahamaki fegi ikaangukia godoro na godoro likapata moto. jamaa aliungua kuanzia miguuni mpaka mgongoni ndo alipostuka. hanga zima watu wakatoka nje wakikimbia moshi mzito, moto na harufu ya nyama. abraham nae akatoka nje akikimbia huku nyama zikimpukutika. alidondoka baadae na kuzimia. alifariki siku chache baadae. ilisikitisha sana na mpaka leo namkumbuka mshikaji!
 
kwa kweli umenikumbusha mbali sana nakumbuka ilikuwa julai 1987 tulienda makuyuni jkt wakati huo tumetokea oljoro tulienda kuvuna mahindi na maharage. tukachapa kazi kweli kweli hadi maafande wakafurahi wakaamua kutufanyia sherehe tukala tukashiba na mchana tukapellekwa mto wa mbu tukanywa tukawa hoi. basi alfajiri saa 11.00 tukaamshwa bado tuna uchovu na usingizi mwingi. afande akatuamsha amkeni amkeni starehe zenu hazihusiani na ratiba ya jeshi. ikabidi tukurupuke hatukua na jinsi
 
Wadau mbona mmebaki jeshini tu! Kumbukeni Mengine
Mmmh!

Mimi Namkumbuka Ezni zile . . .Jeshi lilikuwa hata mashuleni
Mfano nyimbo hizi

1. Jua lileee literemke maama mama ..aiiyah iyaah iyaah mama! Nyota nazo zishuke shuke maama mama aiyah iyah iyaa iyaa maama''
2. Nyerereee yupooo nyerereee yupoooo. ukiona kundi la wazee nyereree yupoooo na Mwinyi yupooo na mwinyi yupooo, ukiona kundi la vijana na mwinyi yupooo, kawawa yupoooo kawawa yupo ukiona kundi la wa baba kawawa yupooooo.
3. Michezo kama kombo lela ''' Mnakumbuka mambo ya (a) Tiari badooo? Tiaari bado ; bado.....
4. Mnakumbuka mchezo wa kupiga kijiwe kwa kidole cha mguu huku mguu mmoja ukiwa umekunjwa ukikivusha katika mistatili iliyochorwa ardhini huku ukisema MA RAIT = I'm right?, MA RAIT = I'm Right?
Ilikuwa inafurahisha sana.
 
Mkuu soma heading ya thread kwanza. Haya uliyoleta ni mazuri tu kwa kumbukumbu za utotoni, ungeweka kwenye thread yake. Hapa ni kumbukumbu za JKT(ni kule JKT hawakucheza Tiari bado- hawakuwa watoto) kama heading inavyoonyesha. post yako ni odd kwenye thread hii.
 
duh ... pale Makutupora 1993 operesheni vyama vingi ..... tuliiba zabibu nyeupe nakwenda kuzila mitunduruni ....

very interesting and uncovered now .....rais wa DRC Hon. Joseph kabila alikuwa Combania D....... wala hatukuwahi kujua yeye ni nani ..alikuwa mpole and very social
 
aisee tulikuwa wote Ruvu mwaka huo! nilikuwa danger coy na akina rodrick, gado, kapeya na wengineo. dah ilikuwa poa kishenzi. ila nakumbuka tukio la kusikitisha lilitokea kwenye coy yako F coy. siku yetu ya mwisho jeshini. umepigwa muziki mpaka (nadhani walikuwa JKT Kimbunga stereo enzi hizo) asubuhi. watu tukarudi kulala mida ya alfajiri. jamaa yenu mmoja, abraham maji alikuwa chakari. akalala huku akivuta fegi yake. kutahamaki fegi ikaangukia godoro na godoro likapata moto. jamaa aliungua kuanzia miguuni mpaka mgongoni ndo alipostuka. hanga zima watu wakatoka nje wakikimbia moshi mzito, moto na harufu ya nyama. abraham nae akatoka nje akikimbia huku nyama zikimpukutika. alidondoka baadae na kuzimia. alifariki siku chache baadae. ilisikitisha sana na mpaka leo namkumbuka mshikaji!

Kweli kifo cha Abrahamu Maji kilisikitisha sana. Wengine nawakumbuka ktk kombania yenu ni akina John Mongela na Evarist Mashiba! Kuna mshikaji tulikua nae hapo F coy akiitwa Amir Nondo siku hizi ni Meya wa Manispaa ya Morogoro!
 
Nimefurahi sana hapa kwani umenikumbusha Vibwende na kwa babu.

Afande wangu Mazani, Chenga, Basekana, Urasa, Nyundo,kibuyu na wengine.

Hakika mambo yalikuwa bambam ingawa nilikaa kwa miezi mitatu tu kisha nikaja mgulani Shuleni kwa masawe, Mtibwela, Kipingu, na wengine.

Jeshi lilikuwa tamu sana. Mimi nilikuwa operasheni vyama vingi
 
Kweli kifo cha Abrahamu Maji kilisikitisha sana. Wengine nawakumbuka ktk kombania yenu ni akina John Mongela na Evarist Mashiba! Kuna mshikaji tulikua nae hapo F coy akiitwa Amir Nondo siku hizi ni Meya wa Manispaa ya Morogoro!

F coy ya mwambingu na Sahani?
 
Niliku kombania c almaarufu kama chale coy kikosi cha Ruvu,wakati huo oc we2 ni shengena na sir major ni medard,ilikuwa ni opareshen mkapa.kulikuwa na shida ya maji sana kambini,tulikuwa tukiteka maji kwa dosa,vibwende,kwa babu n.k,ilimradi tu ufikishe usawa wa kombania ndoo yako1 kwa ukaguzi.swala hili lilikuwa kero ndipo 2lipoamua kuwateka wafanyakazi wa idara ya maji ruvu juu na kuwaamrisha wafungulie maji kuelekeza kikosini.makuruta wenze2 walifurahi kwani hapakuwa na aza tena ya maji.
 
Kweli kifo cha Abrahamu Maji kilisikitisha sana. Wengine nawakumbuka ktk kombania yenu ni akina John Mongela na Evarist Mashiba! Kuna mshikaji tulikua nae hapo F coy akiitwa Amir Nondo siku hizi ni Meya wa Manispaa ya Morogoro!

yes amiri nondo nilimwona kawa meya! alikuwa na mshokaji wake madenge. nadhani nilisikia madenge amefariki. sijui kama ni kweli, dah!
 
Back
Top Bottom