Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Afande Justo wa OLJORO na mkwara wake wa KWATA....Pia shamba almaarufu DUNIA...unaangalia mraba wa kupalilia huoni mwisho........Kuchonga matofali toka mwamba laini kwa Mzee Shabaan.....Hakika ulikuwa mwaka wa aina yake...Pamoja na ukakamavu nilijifunza kuwaza haraka sana hasa katika kutengeneza UONGO kujiokoa kwenye mikono ya maafande pale ukutwapo usipotakiwa kuwa🙂
Thread hii imenikumbusha mbali sana. Kipindi ambacho vijana wa kitanzania tulikutana,tukaishi pamoja,kwa shida na raha na kuliko yote kwa Upendo bila kujali dini,kabila,rangi na hadhi ya ww ni mtoto wa nani! Nlikua Operesheni Kambarage, 832KJ,1Ruvu, F.Coy! Siwezi msahau afande Sanga. Alipendwa ma Kombania nzima. Sijui yuko wapi siku hizi. Siku hizi kila nikiwa napita kwa gari hapo Ruvu darajani mpaka Mlandizi,upata hisia kali.
Mko wapi akina Alex Binde, Warioba, Mercy Fanuel, Anzameni, Urio na wengine wengi?
Mkuu soma heading ya thread kwanza. Haya uliyoleta ni mazuri tu kwa kumbukumbu za utotoni, ungeweka kwenye thread yake. Hapa ni kumbukumbu za JKT(ni kule JKT hawakucheza Tiari bado- hawakuwa watoto) kama heading inavyoonyesha. post yako ni odd kwenye thread hii.Wadau mbona mmebaki jeshini tu! Kumbukeni Mengine
Mmmh!
Mimi Namkumbuka Ezni zile . . .Jeshi lilikuwa hata mashuleni
Mfano nyimbo hizi
1. Jua lileee literemke maama mama ..aiiyah iyaah iyaah mama! Nyota nazo zishuke shuke maama mama aiyah iyah iyaa iyaa maama''
2. Nyerereee yupooo nyerereee yupoooo. ukiona kundi la wazee nyereree yupoooo na Mwinyi yupooo na mwinyi yupooo, ukiona kundi la vijana na mwinyi yupooo, kawawa yupoooo kawawa yupo ukiona kundi la wa baba kawawa yupooooo.
3. Michezo kama kombo lela ''' Mnakumbuka mambo ya (a) Tiari badooo? Tiaari bado ; bado.....
4. Mnakumbuka mchezo wa kupiga kijiwe kwa kidole cha mguu huku mguu mmoja ukiwa umekunjwa ukikivusha katika mistatili iliyochorwa ardhini huku ukisema MA RAIT = I'm right?, MA RAIT = I'm Right?
Ilikuwa inafurahisha sana.
aisee tulikuwa wote Ruvu mwaka huo! nilikuwa danger coy na akina rodrick, gado, kapeya na wengineo. dah ilikuwa poa kishenzi. ila nakumbuka tukio la kusikitisha lilitokea kwenye coy yako F coy. siku yetu ya mwisho jeshini. umepigwa muziki mpaka (nadhani walikuwa JKT Kimbunga stereo enzi hizo) asubuhi. watu tukarudi kulala mida ya alfajiri. jamaa yenu mmoja, abraham maji alikuwa chakari. akalala huku akivuta fegi yake. kutahamaki fegi ikaangukia godoro na godoro likapata moto. jamaa aliungua kuanzia miguuni mpaka mgongoni ndo alipostuka. hanga zima watu wakatoka nje wakikimbia moshi mzito, moto na harufu ya nyama. abraham nae akatoka nje akikimbia huku nyama zikimpukutika. alidondoka baadae na kuzimia. alifariki siku chache baadae. ilisikitisha sana na mpaka leo namkumbuka mshikaji!
Kweli kifo cha Abrahamu Maji kilisikitisha sana. Wengine nawakumbuka ktk kombania yenu ni akina John Mongela na Evarist Mashiba! Kuna mshikaji tulikua nae hapo F coy akiitwa Amir Nondo siku hizi ni Meya wa Manispaa ya Morogoro!
F coy ya mwambingu na Sahani?
Kweli kifo cha Abrahamu Maji kilisikitisha sana. Wengine nawakumbuka ktk kombania yenu ni akina John Mongela na Evarist Mashiba! Kuna mshikaji tulikua nae hapo F coy akiitwa Amir Nondo siku hizi ni Meya wa Manispaa ya Morogoro!