Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Haka kanyegere kanaitwa honey badger kwa Kiingereza kanapiga Cobra au black Mamba kama hakana akili nzuri...nyoka zote hatari kanaziua haraka sana huwezi amini...kana ukuda sana haka kadude..kanajiamini kwelikweli ukikaona kanamvimbia Simba utashangaa sana...kitu cha kujifunza kwa haka kadude ni ile hali ya kujiamini sana.

Kanaweza kuingia vitani bila kujali hali na hilo linasaidia sana...
 
Uwiiiiiiiiii nimeogopa sana [emoji27] [emoji27] [emoji27] [emoji27]
 
Nimeenda Google, nimesoma sentensi hii, du! nimemuogopa huyu mnyama mdogo. The only sure way of killing them quickly is through a blow to the skull with a club or a shot to the head with a gun, as their skin is almost impervious to arrows and spears.
Ni kweli kabisa mimi kuna siku aliwahi kuingia nyumbani usiku kufuata kuku mimi sikujua huyo ni nyegere nilichukua mpini mfupi na kupambana naye kila alipokuja miguuni kunifuata nilikuwa nampiga kichwani nilicheza naye kama dakika 20 nikafanikiwa kumuua nikamfunga kamba shingoni na kumtupa nje ya nyumba wala sikujua nimeua mnyama gani mpaka kesho yake asubuhi walipopita wapita njia ndiyo wakasema ni nyegere hapo ndipo nikapata uonga kumbe nilipambana na mnyama hatari hivyo lakini nikagundua uonga saa nyingine hufanya mtu asiwe na ujasiri kwani pengine ningekuwa nimejua tangu awali kuwa nyegere kaingia ndani pengine ningeshikwa na woga hivyo mnyama huyo angenidhuru
 
Kuna jiran yangu ntaanza kumwita jina nyegera maana ana wivu kupitiliza.
 
Nitajie jina lako nikuingize kwenye guiness book of records,,,
 
  1. Mkuu Mkereketwa haina haja ya kuniita muongo,ungeweza kutoa usahihi ya maelezo yako ya "kitaalamu" bila kunipa hilo jina.
    Mimi nimefundishwa kwa kurithishwa na mababu zangu wawindaji tabia za mnyama huyu na jinsi ya kukabiliana nae,Wazee hawakuwa wameenda shule kusomea mambo ya wanyama,wao walikuwa wanajuwa mashuzi ya Nyegere si tu kujilinda na maadui kwa harufu kali,bali pia kuwapumbaza nyuki kila wanapokuwa wanakwenda kuvamia asali

    Naahukuru kuwa hujapinga kuwa nyengere hujamba mashuzi yanayonuka,maana hii ndio sifa yake moja wapo kubwa,hizo sababu nyingine ni za elimu darasa ambazo babu zetu hawakupitia.Hata leo ukienda kijijini kwangu ukawaambia mashuzi ya nyegere hayaleweshi nyuki hawatakuelewa na huo "utaalamu" wako
 
Daaah mkuu maalon basi ulikaotea sana haka kajamaa,haka huwa akakubali kushindwa,ni king'ang'anizi sana huyu mdudu...Ama hakika ulikuwa shujaa,vinginevyo kangekuondolea serikali yako yoooote bila huruma,maana kenyewe huwa kanavizia hukohuko "ikulu" kubwa
 
Kwa kimombo anaitwaje? nataka nimfuatilie zaidi kwenye google
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…