Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

hili ni pendekezo la CDM wakati wa Katiba ya Jaji warioba pamoja na kufuta viti vyote vya upendeleo aka viti maalum.

CDM ni kiongozi wengine daima hufuatia.
 
Elimu ya uhalisia ni muhimu sana kabla ya Mfumo wa sasa tulikuwa na mifumo ya kiuhalisia.

Mtoto mwanaume wa kimasai akifika miaka 14-18 anaenda jando. Hapo anajifunza kuwinda (kazi), kuua simba, kukatwa govi bila ganzi au kulia kuhakikisha ni jasiri. Anaitetea familia jamii.

Baada ya miezi kadhaa anarudi nyumbani kama mwanaume anaoa. Mtu mzima mwenye nyumba, familia chakula, kipato.

Msichana hivyo hivyo kujifunza kulea familia.
 
Elimu yetu inabidi iwe ya kiuhalisia. Tuwaige Watanzania asili, zetu. Ila tuboreshe kwa mazingira ya leo.

Ni elimu ya ajabu mtu wa miaka 25, 30, 40 bado anatafuta ajira. Hajaandaliwa kukabiliana na maisha. Yupo nyumbani kwa wazazi wake. Anaomba pesa ya kunyoa ndevu.
 
Nimeipenda namba 11. ni kweli kwamba wafanyakazi wa TRA hawajui kabisa biashara ndiyo maana tozo wazokadiria ni za kubuni, au za kishabiki au za visasi na/au zinatokana na wivu. Niliwahi kuwaza kuwa ingekuwa vizuri sana kama kabla ya mtu kuteuliwa kuwa msimamizi wa kazi TRA angepewa kwanza mtaji wa kiasi aambiwe akaanzishe biashara, akishafanikiwa ndipo ateuliwe kuongoza TRA.
 
Niliwahi kuwaza kuwa ingekuwa vizuri sana kama kabla ya mtu kuteuliwa kuwa msimamizi wa kazi TRA angepewa kwanza mtaji wa kiasi aambiwe akaanzishe biashara, akishafanikiwa ndipo ateuliwe kuongoza TRA.
Hiyo mbinu italeta tija uhalisia, maamuzi mazuri kwenye maamuzi.
 
Napenda Zanzibar itoke katika makucha ya UKOLONI
 
Baadhi ya hao wawakilishi wa majimbo waliochaguliwa na wananchi wanamchango gani mpaka sasa?
 
Mapendekezo yangu ni:
1. Vyama vya siasa viwe vitatu tu.
2. Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ihamishiwe TAKUKURU
3. Mikataba yote ya Serikali na haswa ya miradi mikubwa iwekwe wazi kabisa na wahusika walioandaa huo mkataba watangazwe wazi na wawe wameweka sahihi document ya kula kiapo kuwa wako tayari kushtakiwa kama mkataba utabainika kutokuwa n manufaa kwa Taifa
4. Sheria za nchi zipitiwe upya na kuboreshwa ili ziendane na wakati. Zipo sheria nyingi zimepitwa na wakati.
5. ..... nitaendelea baadaye..
 
CCM itakufa
 
Napenda Zanzibar itoke katika makucha ya UKOLONI

Wapewe uhuru 100% wa kuchagua nini wanataka. Wakijua pia kuna Wazanzibari wengi Tanganyika labda kuliko Zanzibar.

Muhimu pia kuangalia Historia ya Zanzibar kwa miaka 1500 iliyopita.

Zanzibar ni nini? Hili jina lina maana gani? Watu wa Zanzibar ni akina nani? Wametokea wapi wengi wao? Kwanini kulikuwa na Muungano? Serikali ya mapinduzi? Bila muungano mtawala na serikali yake angekuwa nani?

Walifanya nini kwa Wazanzibari wengi kwa miaka zaidi ya 500? Kusudi hasa ni lipi miaka 60 iliyopita au leo la mapinduzi Demokrasia ni nini?

Kwamba utawala urejeshwe kwa nani? Nani ataathirika, wananchi watanufaika au kuaathirika?

Wanatenganishwa na nini?

Nini itakuwa hatima ya Kutengana, kusafiri, biashara zao ilala, kariakoo, nyumba zao kigamboni, mashamba yao TZ nzima, kupewa uongozi Tanganyika mkubwa popote Tanzania yote?

Pato la Wazanzibar liaathirika vipi?

Huu muungano unaweza kuboreshwa? Kupendwa na pande mbili? Nini kiboreshwe?

Kura ya maoni inaweza kufanyika kuuliza maswali haya yote. Majibu kuzingatiwa kama Scotland Brexit.
 
Natamani sana tume ya uchaguzi wahusika wasiteuliwe na rais lakini sioni jinsi Marais watakavyo shindwa kutia Miko oyao.
 
Ruzuku ya vyama iwemo...
Ruzuku ya kampeni iwemo... (Wagombea wakishapitishwa basi wapewe mafungu yenye masharti kwa ajili ya kampeni). Matumizi yawe sawa!
 
Ruzuku ya vyama vya siasa iko kwenye kifungu kipi cja katiba? sukuma gang na nguruwe wa uvccm ongezeni maarifa ili yawasaidie yani mmekuwa mkiimba ruzuku ruzuku kumbe hata sheria inayoanzisha hiyo ruzuku ya vyama vya siasa hamjui hovyo kabisa.

By the way katiba haianzishi ruzuku ya vyama vya siasa hivyo haiwez kuondolewa kwenye katiba.
 

Wabunge wawe na eleimu kuanzia degree
 
Naunga mkono hoja maana kupitia hizi ruzuku ndo kuna kuwa na wanasiasa wa kufanya biashara na chama kwa mgongo wa kukikopesha chama
 
Wabunge walipwe fixed salary yenye makato yoote kuanzia kodi na mifuko ya hifadhi ya jamii... sitting allowance ziondolewe, mafao walipwe kama wastaafu wengine...
 
Kukitokea kifo kile chama cha pili kichukue madaraka. Nafasi za DC RC, DAS, RAC Jaji zoote zitangazwe, Mawaziri wasiwe wabunge. Tume huru ya uchaguzi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…