samsolo the great
JF-Expert Member
- Jul 9, 2021
- 750
- 1,086
Hiyo number 3 iko poa sana kwani tumeibiwa mno kwa sababu ya maslahi binafsi au ukilazaMapendekezo yangu ni:
1. Vyama vya siasa viwe vitatu tu.
2. Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ihamishiwe TAKUKURU
3. Mikataba yote ya Serikali na haswa ya miradi mikubwa iwekwe wazi kabisa na wahusika walioandaa huo mkataba watangazwe wazi na wawe wameweka sahihi document ya kula kiapo kuwa wako tayari kushtakiwa kama mkataba utabainika kutokuwa n manufaa kwa Taifa
4. Sheria za nchi zipitiwe upya na kuboreshwa ili ziendane na wakati. Zipo sheria nyingi zimepitwa na wakati.
5. ..... nitaendelea baadaye..
Na agombee si zaidi ya two terms kwani kuna wabunge wamefika mahali wamejimilikisha majimbo na kutamka wazi kwamba hili ni jimbo languWabunge wawe na eleimu kuanzia degree
Chadema tumekuangalia muda mrefu, Sasa naona unavuka mipaka, tutakufukuzaWaziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo
Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi
Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa
Karibu
Ni kweli kabisa inakuwaje mbunge analipwa sitting allowance na perdiem jml tsh 320000 kwa siku anayohudhuria kikao na mwisho wa mwezi analipwa mshahara kwani alipogombea hakujua kwamba wajibu wake wa kwanza ni kuhudhuria vikao vya bunge ambavyo vitampatia mshahara mwisho wa mweziWabunge walipwe fixed salary yenye makato yoote kuanzia kodi na mifuko ya hifadhi ya jamii... sitting allowance ziondolewe, mafao walipwe kama wastaafu wengine...
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo
Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi
Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa
Karibu
Ni kweli kwani hiyo dua wanaombewa na viongozi waovu waliotia taifa hili katika mikataba ya kimangungo ambayo imesababisha dhahama na madeni ya ajabu ajabu wakijificha kwenye kivuli cha kuwa na kinga ya kutoshtakiwa
- Wabunge wawe kimikoa no viti maalumu
- Marais wasijengewe majumba wakistaafu hakuna upendeleo watumishi wote wawe sawa
- Maneno Mungu wabariki viongozi kwenye national anthem yafutwe
- Neno waheshimiwa lifutwe na liwe haraam wote tuitane ndugu inatosha
- Viongozi washitakiwe hakuna mtu kuwa juu ya sheria
- Scale za malipo kwa watumishi wote wa umma wakiwepo wabunge na viongozi wote zipangwe na wananchi
Tufute vyama tubaki na Nini ? Au nchi iongozwe na CDF..Vyama kwa Afrika havina umuhimu kwa wananchi ni magenge ya kupiga pesa za wananchi.
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo
Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi
Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa
Umegusa Chaka la chatu hapo ukitaka watu wakupopoe kwa mawe na virungu gusa ruzuku watakuua Mimi naunga mkono hoja Kila chama kitumie aseti na rasilimali zakeKuhusu elimu, vijana mitaala ifundishwe njia za kutatua changamoto kwenye jamii husika na changamoto za kesho kuanzia darasa la kwanza.
Kijana akimaliza hata darasa la saba/ kidato cha nne ana uwezo wa kujiajiri.
Fani kama kilimo bora chenye tija, chakula kizuri kwa afya na jinsi ya kupika, jinsi ya kuzuia magonjwa kutumia chakula, kuishi vizuri.
Jinsi ya kujenga nyumba, ku-repair baiskeli gari, laptops, computers, phone ziwe compursory kuanzia shule za msingi.
Watoto wafundishwe njia sahihi za kutumia pesa (financial literacy) na accounting, biashara.
Elimu iwepo kwa ajili ya kutatua changamoto zinatoitesa jamii. Iende na wakati sio kukariri vitu visivyomsaidia mwanafunzi au jamii.
KabisaaaNi kweli kwani hiyo dua wanaombewa na viongozi waovu waliotia taifa hili katika mikataba ya kimangungo ambayo imesababisha dhahama na madeni ya ajabu ajabu wakijificha kwenye kivuli cha kuwa na kinga ya kutoshtakiwa