Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Dira ya taifa na mambo yote ya kipaumbele kwa nchi na watu wake vitamkwe wazi wazi kwenye katiba. Vyama vya siasa wakati wa uchaguzi, vijinadi jinsi ya kutekeleza vipaombele hivyo vilivyo ndani ya katiba badala ya kila chama kuwa na ilani ya uchaguzi.
 
1.Napendekeza mishahara ya wabunge ikatwe kodi
2,kima cha chini cha elimu ya mgombea ubunge iwe shahada ya kwanza.
3. spika wa bunge asitoke chama tawala,
4. makamu wa raisi atokee kwenye chama kilichishika nafasi ya pili kwa wingi wa kura
5.wananchi wawe na nguvu ya kufukuza wabunge wao wasiowajibika vzuri
6.umri wa kugombea uraisi uwe kuanzia miaka 30
7.Kila baada ya miezi 3 raisi aandae mdahalo utakaokuwa live kupitia social network yeyote inayowafikia zaidi watanzania wawe live kutoa kero zao na yeye azijibu na atoe suluhu yake
8. Kuwe na wagombea binafsi
9. Tuwe na serikali moja tu kama aiwezekan basi muungano huvunjwe
10.huduma ya afya ndio iwe bure na ni haki ya kila mtanzania
11. Kusiwe na mipaka ya ajira na umiliki wa ardhi kusiwe na utanganyika wala uzanzibar kuwe na utanzania tu sote tuwe na haki sawa ya kuajiriwa popote pale hiwe zanzibar au tanga au popote tanzania hiii na sote tuwe na haki sawa ya umiliki wa ardhi popote pale yaani
12 raisi na viongozi wowote wale washitakiwe wakifanya uhalifu hata kama wapo madarakani
Asante, namba moja ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Hata wanunuapo bidhaa pia walipe kodi kama wananchi wengine.
Namba 9 nayo ni muhimu sana, tumekwisha toka kwenye serikali 3 hatuwezi kurudi nyuma, sasa iwe serikali moja.
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
posho za wabunge zikatwe kodi
 
Mapendekezo yangu ni:
1. Vyama vya siasa viwe vitatu tu.
2. Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ihamishiwe TAKUKURU
3. Mikataba yote ya Serikali na haswa ya miradi mikubwa iwekwe wazi kabisa na wahusika walioandaa huo mkataba watangazwe wazi na wawe wameweka sahihi document ya kula kiapo kuwa wako tayari kushtakiwa kama mkataba utabainika kutokuwa n manufaa kwa Taifa
4. Sheria za nchi zipitiwe upya na kuboreshwa ili ziendane na wakati. Zipo sheria nyingi zimepitwa na wakati.
5. ..... nitaendelea baadaye..
Naongeza kidogo;
1. Viongozi wa Mashirika ya umma wafanyiwe "public vetting" ili wachaguliwe kutokana na uwezo wao unaoendana na taaluma aliyosomea na hitaji la shirika lenyewe.
2. Viongozi wa Mihimili yoote wawe wanachaguliwa kwa kupigiwa kura siyo kuteuliwa na Rais. Jaji Mkuu akiteuliwa na Raisi basi sheria lazima itapindishwa. Na iwe marufuku Jaji Mkuu kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.
3. Hata Spika wa Bunge si lazima atoke chama Tawala, kuwepo utaratibu wa kumpata spika ambye hahusiki n chama chochote cha siasa.
4. Wakuu wa Mikoa wawe wanagombea nafasi na wapigiwe kura Mikoani mwao hali kadhalika wakuu wa Wilaya.
5. Wakurugenzi wa Mikoa na Wilaya wapitie public vetting, wachaguliwe kwa uwezo na asiwe mfuasi wa chama chochote cha siasa.

...... huenda nitaendelea
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
Ni vyema ukashukuru kwa neema ya Akili uliyopewa na Mola wako ndugu yangu yohana, hivi kweli mbali na chama chako kupora, kufuja na kutapanya mali za umma kwa kigezo Cha "chama cha Mapinduzi" bado unaweza kuwa na hasadi kwa vyama vichanga ndani ya karne hii ya domo cratia? Viwanja lukuki vya mipira, maeneo ya wazi , majengo ya umma, fadha kutoka kwa mifuko ya umma bado unawaonea gere wanyonge? Ikowapi mantiki ya wazee wetu kupigania uhuru wa Taifa hili? Kwakweli hii Inakuwa kama laana umeni disappoint bwana John
 
Kambaya atuhumiwa kujenga ghorofa kwa Fedha za Ruzuku!

Niishie hapo
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
1. Mawaziri wasiwe wanateuliwa na rais bali ziwe za kuomba, ili kila wizara iwe na waziri ambaye ana fani husika, kama ni wizara ya Kilimo iwe na waziri pamoja naibu wake ni wataalam wa kilimo hivyo hivyo wizara ya afya, uvuvi, Ulinzi na Usalama.

2. Kiongozi aliye madarakani au amestaafu akiwa amefanya makosa pawe na uwezekano wa kuwajibishwa na kushitakiwa.

3. Ardhi isiwe mali ya serikali bali raia wawe na mamlaka na ardhi ikitokea mwekekezaji, huyo mwekekezaji ataelewana malipo na mwenye ardhi ambaye ni raia.
4. Bidhaa za zinazotoka Zanzibar kuja Tanzania bara au zinazotoka Tanzania bara kwenda Zanzibar zisitozwe kodi hata bidhaa za matumizi ya nyumbani kutoka Zanzibar ushuru uondolewe.
5. Wabunge wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mishahara yao ipungue na posho zao pia, haiwezekani Daktari aliyesomea fani yake miaka saba au wanajeshi wanaolinda nchi kwa jasho, damu na uhai wanazidiwa mishahara na wabunge wengi wao elimu ya la saba au form four.
Pia watozwe kodi kama raia wengine kwenye nchi hii, haiwezekani muuza nyanya atozwe mbunge asikatwe kodi.
 
Idadi ya wizara isizidi 15
 
Back
Top Bottom