1. Mawaziri wasiwe wanateuliwa na rais bali ziwe za kuomba, ili kila wizara iwe na waziri ambaye ana fani husika, kama ni wizara ya Kilimo iwe na waziri pamoja naibu wake ni wataalam wa kilimo hivyo hivyo wizara ya afya, uvuvi, Ulinzi na Usalama.
2. Kiongozi aliye madarakani au amestaafu akiwa amefanya makosa pawe na uwezekano wa kuwajibishwa na kushitakiwa.
3. Ardhi isiwe mali ya serikali bali raia wawe na mamlaka na ardhi ikitokea mwekekezaji, huyo mwekekezaji ataelewana malipo na mwenye ardhi ambaye ni raia.
4. Bidhaa za zinazotoka Zanzibar kuja Tanzania bara au zinazotoka Tanzania bara kwenda Zanzibar zisitozwe kodi hata bidhaa za matumizi ya nyumbani kutoka Zanzibar ushuru uondolewe.
5. Wabunge wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mishahara yao ipungue na posho zao pia, haiwezekani Daktari aliyesomea fani yake miaka saba au wanajeshi wanaolinda nchi kwa jasho, damu na uhai wanazidiwa mishahara na wabunge wengi wao elimu ya la saba au form four.
Pia watozwe kodi kama raia wengine kwenye nchi hii, haiwezekani muuza nyanya atozwe mbunge asikatwe kodi.