2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).
Hovyo.
Sio kufuata mkumbo kama ulivyoliweka hapa.
Huu ni udhaifu mkubwa sana aliouonyesha, pengine unaokaribiana na uvunjaji wa HAKI.
Dunia haikuwa inafuata mkumbo. Dunia ilifuata taratibu za kisayansi zinazojulikana katika kukabiri janga la ugonjwa wa mlipuko.
Huwezi kujipangia/kujichagulia njia zako juu ya kitu usichokifahamu, huku ukihatarisha maisha ya watu wako.
Bahati yetu ni kwamba kwa sababu zisizojulikana bado, corona huku Afrika haikushambulia kwa nguvu kama ilivyoshambulia kwingine. Ingekuwa hivyo toka mwanzo hali yetu ingekuwa mbaya sana.
Huu uamzi wa kujifanyia lake, eti kutofuata mkumbo, ulikuwa ni moja ya uamzi wa hovyo sana kwa kiongozi wa nchi.
Alichotakiwa kufuata juu ya hili, angekaa na wataalam na kujadili njia bora kufuatana na hali yetu.
Kwa mfano: msukumo mkubwa wa uamzi wa kutofuata 'guidelines' za WHO ni kulinda uchumi, hasa kutokana na madhara ya LOCKDOWN.
Basi angeshauriana na wataalam wake, wafuate yaliyomo kwenye 'guideline' hiyo, na kurekebisha kwa kiasi walichoona hayo matakwa ya 'Lockdown'.
Kutofuata mkumbo?, unapingana na sayansi? Chanjo unazikataa eti hufuati mkumbo?
Acha Bhwaanah!
Kuna mambo kadhaa ninayompa hongera juu yake kwa kuyafanya, hata kama wakati mwingine njia alizotumia kuyafanya hazikuwa sahihi.